Baba
Mtakatifu Francisko, Jumatatu jioni alikamilisha hija yake Mashariki
ya Kati na wito wa amani. Hija hii ya siku ya tatu 24-26 Mei 2014
kutembelea maneneo Matakatifu katika Nchi Takatifu aliikamilisha, akiwa
mjini Jerusalem ambako hatua ya mwisho aliongoza Ibada ya Misa akiwa na
Maaskofu wa Nchi Takatifu, katika jengo lenye Chumba cha Juu ambako
Kristo, alifanya karamu ya mwisho, kinachojulikana kama “cenacolo”.
Baada
ya Ibada, alielekea uwanja wa ndege wa Monte Scopes , ambako alipanda
helkoputa hadi uwanja wa Ndege wa Ben Gourion wa mjini Tel Aviv,
ambako aliagana na wenyeji wake, viongozi wa kanisa na serikali
wakiongozwa na Rais wa Israel, Shimon Peres. Mahali hapo Papa pia
kulifanyika gwaride la heshima la wanajeshi. Na kabla ya kupanda ndege
alitoa salaam zake za mwisho kwa wote.