Ijumaa kuu Kanisa linakumbuka mateso na
kifo cha Kristo Msalabani, chemchemi ya upendo na huruma ya Mungu kwa
waja wake! - REUTERS
Kardinali
Leonardo Sandri, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Makanisa
ya Mashariki anasema kuna haja ya kujenga na kudumisha utamaduni wa watu
kukutana na kusaidiana ili kuondokana na mantiki ya ubinafsi na kuta za
utengano ambazo hazina mashiko wala tija kwa watu wanaoishi huko
Mashariki ya Kati. Misaada inayotolewa na Jumuiya ya Kimataifa haina
budi kuwafikia walengwa huko: Mashariki ya Kati hasa Syria na Iraq.