Wakizungumza kwa nyakati tofauti juzi na jana, wadau hao wameelezea
kufurahia kufikiwa na tamasha hilo la kimataifa ambalo litapambwa na
waimbaji wa ndani na nje ya Tanzania.
Kwa upande wake, Matata Ndizi, kati ya wadau wakubwa wa muziki wa
Injili, alisema angependa kumuona muimbaji Edson Mwasabwite katika
tamasha hilo.
“Kwanza tunashukuru kutuletea tamasha hilo mkoani Morogoro, lakini
kati ya waimbaji ambao tungependa kuwaona ni Edson Mwasabwite,” alisema
Matata.
Alisema amekuwa akibarikiwa sana anapomsikiliza mwimbaji huyo anayetamba na albamu yake ya ‘Ni Kwa Neema.’
“Mbali ya ukali wa kibao chake, Mwasabwite ni mwimbaji mpya, hivyo
wengi wangependa kumuona ‘live’ siku hiyo ya tamasha,” alisema.
Mwasabwite, mzaliwa wa Mbeya amekuwa aking’ara na albamu hiyo yenye
nyimbo nyingine saba, ambazo ni ‘Tarajia’, ‘Mujiza’, ‘Asante Yesu’,
‘Usiwe Mbali Nami’, ‘Bwana Yesu’, ‘Atanifuta Machozi’, ‘Milele
Usifiwe’ na ‘Mungu Wetu Anaweza’.
Mwingine aliyempendekeza Mwasabwite ni Innocent Kobelo wa Mafisa
mkoani humo, ambaye amekiri kuwa amekuwa akivutiwa naye hivyo angefurahi
kumwona ‘live’
.
Waandaaji wa Tamasha la Krismasi, wamebainisha kuwa wamepania
kulifanya liwe la aina yake tofauti na mengineyo kwa kualika waimbaji
maarufu ndani ya nje ya nchi, ambako tayari wamemtangaza Upendo Nkone
kuwemo katika tamasha hilo litakaloanza kukata utepe Desemba 25 jijini
Dar es Salaam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni