Kilimanjaro Stars iliyotwaa kombe hilo mara ya mwisho 2010 chini ya Kocha Mdenmark, Jan Poulsen, na ambayo imepangwa Kundi B katika michuano ya mwaka huu, itacheza mechi yake ya kwanza Novemba 28, mwaka huu dhidi ya Zambia kwenye Uwanja wa Machakos nje kidogo ya Jiji la Nairobi.
Wachezaji wanaounda kikosi hicho cha Tanzania Bara ni makipa Deogratius Munishi 'Dida' (Yanga), Ivo Mapunda (Gor Mahia, Kenya) na Aishi Manula (Azam). Mabeki ni Erasto Nyoni (Azam), Himid Mao (Azam), Ismail Gambo (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Michael Pius (Ruvu Shooting) na Said Moradi (Azam).
Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd 'Chuji' (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Chanongo (Simba), Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Ramadhan Singano 'Messi' (Simba) na Salum Abubakar 'Sure Boy' (Azam).
Safu ya ushambuliaji inaundwa na Elias Maguli (Ruvu Shooting), Faridi Musa (Azam), Joseph Kimwaga (Azam), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngasa (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).
Kwa mujibu wa Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Boniface Wambura, Kilimanjaro Stars inatarajia kuondoka Jumatatu kwenda Nairobi kushiriki michuano hiyo itakayoanza Novemba 27 na kumalizika Desemba 13, mwaka huu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni