Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amemteua
Dokta Asha-Rose Migiro, aliyekuwa Naibu Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa
kuwa Mbunge.
Taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar Es Salaam, Jumanne,
Desemba 3, 2013, na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Dokta. Florens Turuka
inasema kuwa uteuzi huo umeanza Desemba 2, 2013. Dr. Asha-Rose Migiro
ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Idara ya Siasa na Uhusiano wa
Kimataifa katika Chama cha Mapinduzi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni