Jumuiya ya Kimataifa inaomboleza Kifo cha Tata Madiba!
Viongozi
wa Jumuiya ya Kimataifa pamoja na wananchi wa Afrika ya Kusini wameanza
kutoa heshima zao za mwisho kwa Tata Madiba kwa sala kutoka kwa
viongozi mbali mbali wa kidini nchini Afrika ya Kusini. Mvua iliyokuwa
inanyeesha imewazuia wananchi wa kawaida kufika uwanjani ili kutoa
heshima zao za mwisho kwa Mzee Nelson Mandela, lakini mvua ni kielelezo
cha baraka kwa makabila mengi Barani Afrika. Katibu mkuu wa
Umoja wa Mataifa, Bwana Ban Ki-Moon katika salam zake za rambi rambi
amesema, Afrika ya Kusini imempoteza shujaa wake; imempoteza Baba na
muasisi wa taifa la Afrika ya Kusini. Jumuiya ya Kimataifa imempoteza
kiongozi mashuhuri na mfano bora wa kuigwa katika kutetea na kulinda
haki msingi za binadamu.
Amepambana kufa na kupona kupinga
ubaguzi wa rangi, akawa ni mfano na kielelezo cha kiongozi anayetambua
na kuthamini msamaha. Amesimamia usawa, uhuru, haki, amani na demokrasia
ya kweli.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni