Kila mmoja wetu anafahamu kwamba Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson
Rolihlahla Mandela
amefariki dunia jana December 6, 2013. Rais JM
Kikwete pia akatangaza siku 3 za maombolezo kuanzia leo Dec 6 mpaka Dec 8
na
bendera ya Tanzania itapepea nusu mlingoti siku zote hizo.
Lakini kesho jumamosi Dec 7, 2013 ile timu yetu ya Wadada iliyowabugiza
Msumbiji bao KUMI BILA uwanja wa Taifa inatakiwa kucheza na wadada
wenzao wa Afrika Kusini (Basetsana) kwa ajili ya mechi ya mchujo ya
Kombe la Dunia kwa wasichana wenye umri chini ya miaka 20 katika Uwanja
wa Taifa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni