Baba
Mtakatifu Francisko ametuma salam za rambirambi kwa Rais Jacob Zuma wa
Afrika ya kusini na wananchi wa Afrika ya Kusini kwa ujumla wao kutokana
na kifo cha Mzee Nelson Mandela. Anaiombea roho ya Mzee Mandela iweze
kupata huruma ya Mungu pamoja na kuendelea kuwaimarisha wote walioguswa
na msiba huu mzito!
Baba Mtakatifu Francisko anasema, Mzee
Nelson Mandela alisimama kidete kulinda na kutetea utu na heshima ya
raia wake; akajenga na kuimarisha umoja wa wananchi wa Afrika ya Kusini
pasi na vita, wakitembea katika njia ya upatanisho na ukweli.
Ni
matumaini ya Baba Mtakatifu kwamba, mchango wa Mzee Mandela utakuwa ni
changamoto kwa wananchi wa Afrika ya Kusini kusimama kidete kulinda haki
na mafao ya wengi; wanasiasa wakiwa mstari wa mbele. Baba Mtakatifu
anawapatia wananchi wote wa Afrika ya Kusini baraka zake za kitume,
wakati huu wa maombolezo ya kitaifa!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni