Papa mstaafu Benedikto XVI apata chakula cha mchana na Baba Mtakatifu Francisko
Baba
Mtakatifu mstaafu Benedikto XVI, Ijumaa, tarehe 27 Desemba 2013
amemtembelea Papa Francisko na kupata chakula cha pamoja kwenye Hosteli
ya Mtakatifu Martha iliyoko mjini Vatican.
Hivi karibuni, Baba
Mtakatifu Francisko alimtembelea Papa mstaafu Benedikto XVI ili kumtakia
kheri na matashi mema ya Siku kuu ya Noeli na kutumia fursa hii
kumkaribisha kwa chakula cha mchana, kwenye Hosteli ya Mtakatifu Martha,
iliyoko mjini Vatican.
Makatibu muhtasi pamoja na Askofu mkuu
Dominique Mamberti, Katibu mkuu wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano
wa kimataifa mjini Vatican alialikwa kushiriki pamoja na Monsinyo Bryan
Wells mratibu wa shughuli za mjini wa Vatican.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni