Mwandishi wa habari wa Kituo cha Televisheni cha ITV, Ufoo Saro
akisoma somo kwenye biblia wakati wa ibada maalumu ya shukrani kwenye
Kanisa la (KKKT ) Usharika wa Kibamba nje kidogo ya Jiji la Dare Salaam
jana. Picha na Sanjito Msafiri.
Jumapili
iliyopita tarehe 17 Novemba 2013 wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana,
kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro, waamini na mahujaji
waliokusanyika ili kuungana na Baba Mtakatifu Francisko kwa Tafakari na
Sala ya Mchana, walipewa tiba ya maisha ya kiroho, itakayowasaidia
katika kumwilisha mafanikio ya Mwaka wa Imani.
Mama
Kanisa anajiandaa kufunga rasmi Mwaka wa Imani, uliotangazwa na
kuzinduliwa na Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto wa kumi na sita na
kuendelezwa kwa ari na moyo mkuu na Papa Francisko hapo tarehe 24
Novemba 2013, wakati wa Sherehe ya Kristo Mfalme. Ibada hii inatarajiwa
kuongozwa na Baba Mtakatifu Francisko, kuanzia saa 4:00 asubuhi kwa saa
za Ulaya. Maadhimisho ya kufunga Mwaka wa Imani yataanza rasmi kwa