Radio
Vatican, Mama wa Radio zote duniani, tarehe 12 Februari 2014
imeadhimisha kumbu kumbu ya Miaka 83 tangu ilipoanzishwa. Inajivunia
kuwa ni kati ya wadau wakuu wa Shirikisho la Watangazaji Barani Ulaya,
EBU ambalo tarehe 13 Februari 2014 linaadhimisha Siku ya Radio Duniani.
Kwa namna ya pekee, Jumuiya ya Kimataifa kwa mwaka huu, inajielekeza
zaidi katika kuangalia mchango wa wanawake katika medani mbali mbali za
maisha.
Watangazaji wanawake kutoka Radio Vatican wamekuwa
mstari wa mbele kwa kuwa ni sauti ya wanawake wasiokuwa na sauti kutoka
sehemu mbali mbali za dunia. Radio Vatican katika mtandao wake imeandaa
programe mbali mbali zinazoonesha mchango wa Radio Vatican katika
kuwawezesha wanawake Barani Afrika, Asia na Amerika.
Hizi ni
programme zinazoonesha ujasiri wa wanawake katika kukabiliana na
changamoto mbali mbali za maisha: katika masuala ya maendeleo endelevu,
haki na amani duniani. Ukitaka kufaidi zaidi unaweza kutembelea katika
tovuti rasmi ya Radio Vatican kwa anuani ifuatayo: www.radiovaticana.va Unaweza pia kuwashirikisha jirani zako.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni