Vita,
kinzani na migogoro inayoendelea kujitokeza Barani Afrika imekuwa ni
chanzo kikubwa cha taabu na mahangaiko ya watu wasiokuwa na hatia. Kuna
watu wanalazimika kuyakimbia makazi yao, wanateseka kwa njaa na magonjwa
kutokana na ukosefu wa amani na utulivu.
Baba Mtakatifu
Francisko kwa kuguswa na mahangaiko ya wananchi wa Jamhuri ya Afrika ya
Kati, anawaalika watumiaji wa mitandao ya kijamii, kumuunga mkono katika
kusali kwa ajili ya kuombea amani na utulivu huko Jamhuri ya Watu wa
Afrika ya Kati na Sudan ya Kusini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni