Kurasa

Kurasa

Tamasha la Pasaka kuja kivingine

TAMASHA la Pasaka la mwaka huu litakalozinduliwa rasmi Aprili 20 jijini Dar es Salaam likibeba kaulimbiu ya ‘Tanzania Kwanza Haki Huinua Taifa’, litaendeshwa kwa staili mpya ya wadau wenyewe kuamua na kupanga. Hayo yalibainishwa jijini Dar es Salaam jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Msama Promotions, waandaaji wa tamasha, Alex Msama, akisema wapenzi wa muziki huo ndio watawachagua waimbaji hao kwa kutuma ujumbe mfupi kupitia namba 15327 kwa kutumia mitandao yote ya simu.
“Tamasha la mwaka huu linakuja kwa staili mpya, ambapo wapenzi wa muziki wa injili watakuwa na fursa ya kuwachagua wanamuziki watakaopenda waje kutoa burudani na mikoa litakapofanyika tamasha hilo, tofauti na miaka mingine na wale wote watakaopendekezwa tutawaleta kutoa burudani,” alisema Msama.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni