Kurasa

Kurasa

Batarokota: Tusimsimange Chid Benz mitandaoni

MKURUGENZI wa Batarokota Daily Gospel Newz pia msanii wa nyimbo za bongo fleva nchini Tanzania, Paskal Linda ‘Batarokota ’, amewataka wadau wa muziki, wasanii na Watanzania kwa ujumla kuacha kumsimanga msanii, Chid Benz ambaye ameathirika na matumizi ya dawa za kulevya kwa kuwa ni mambo yanayoweza kumtokea mtu yeyote.

Batarokota alisema kwa sasa msanii huyo yupo mikono salama chini yake akiwa chini ya uangalizi wa kituo cha Life And Hope Rehabilitation Organization, kilichopo Ukuni huko Bagamoyo akipambana kuachana na matumizi ya dawa za kulevya.

Batarokota alisema yeye kama mdau wa muziki wa Bongo Fleva na  anasaidia wasanii wengi ili wapate mafanikio kupitia muziki na kwenye matatizo pia anawasaidia.
“Nimechukua jukumu la kumsaidia Chid Benz, naomba Watanzania tumuombee aweze kupona na si kumchafua kupitia mitandao,” alieleza Batarokota.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni