Kocha mkuu wa timu
ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa ametangaza
kikosi cha wa wachezaji 25 kwa ajili ya mchezo wa kuwania kufuzu kwa
fainali za mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya Chad.
Mechi hiyo imeratibiwa kusakatwa tarehe 23 Machi mjini Djamena.
Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa
Akiongea na waandishi wa habari wakati akitangaza
kikosi hicho, Mkwasa, amewaomba wachezaji aliowaita katika kikosi hicho,
kujiweka katika hali nzuri ya mazoezi katika vilabu vyao, kwani
hakutakua na muda wa kufanya mazoezi kwa ajili ya mchezo huo wa ugenini.
Wachezaji
walioitwa Taifa Stars ni magolikipa Aishi Manula (Azam FC), Ally
Mustapha (Young Africans) na Shaban Kado (Mwadui FC), walinzi ni Juma
Abdul, Haji Mwinyi, Kelvin Yondani (Young Africans), Shomari Kapombe,
Erasto Nyoni, David Mwantika (Azam FC) na Mohamed Hussein (Simba SC). Viungo Himdi Mao (Azam FC), Ismail Juma (JKU), Jonas
Mkude, Said Ndemla, Mwinyi Kazimoto (Simba SC), Mohamed Ibrahim, Shiza
Kichuya (Mtibwa Sugar), Farid Mussa (Azam FC), Deus Kaseke (Young
Africans).Washambuliaji ni Nahodha Mbwana Samatta (KRC Genk),
Thomas Ulimwengu (TP Mazembe), John Bocco (Azam FC), Elias Maguri (Stand
United), Jeremia Mgunda (Tanzania Prisons) na Ibrahim Hajibu (Simba
SC).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni