Wosia wa kitume: "Furaha ya Upendo" kuzinduliwa tarehe 8 Aprili 2016
"Amoris Laetitia" "Furaha ya Upendo"
ndani ya familia ni Wosia wa kitume utakaozinduliwa hapo tarehe 8 Aprili
2016, tayari waamini kutangaza na kushuhudia Injili ya familia!
Padre
Federico Lombardi Msemaji mkuu wa Vatican, Alhamisi tarehe 31 Machi 2016
ametangaza rasmi kwamba, Waraka wa Wosia wa Kitume wa Baba Mtakatifu
Francisko kuhusu Injili ya familia, utazinduliwa rasmi hapo tarehe 8
Aprili 2016. Waraka huu unajulikana kwa lugha ya Kilatini kama “Amoris
Laetitia” “Furaha ya Upendo” ndani ya familia. Waraka
huu ni matunda ya maadhimisho ya Sinodi mbili za Maaskofu kuhusu
familia. Sinodi ya kwanza iliadhimishwa kunako mwaka 2014 na awamu ya
pili kunako mwaka 2015, kuonesha jinsi ambavyo Kanisa linatoa uzito wa
juu kabisa kuhusu wito na utume wa familia ndani ya Kanisa na ulimwengu
mamboleo!
Uzinduzi wa Wosia wa kichungaji wa Baba Mtakatifu Francisko “Amoris
Laetitia” “Furaha ya upendo” ndani ya familia utafanywa na Kardinali
Lorenzo Baldisseri, Katibu mkuu wa Sinodi za Maaskofu; Kardinali
Christoph Shonborn, Askofu mkuu wa Vienna pamoja na Professa Francesco
Miano na mkewe Professa Giusephina De Simone.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni