Kurasa

Kurasa

Kardinali Parolin aongoza Ibada ya Misa ya Shukurani kwa ajili ya Mtakatifu Mama Tereza


Kardinali Pietro Parolin akisalimiana na Masista wa Upendo baada ya Ibada ya MIsa ya Shukurani , katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Vatican 05.08.2016 - OSS_ROM

(Vatican Radio) Jumatatu hii majira ya saa nne za asubuhi, katika Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Jimbo Takatifu ,aliongoza  Maadhimisho ya Misa ya Shukurani , kwa ajili ya Mama Tereza wa Calcutta kutangazwa Mtakatifu na Papa Francisko Jumapili iliyopita
Katika homilia yake, Kardinali  Parolin alikumbuka mambo kadhaa muhimu katika maisha ya Mtakatifu Mama Tereza, hasa  kiu yake kwa Mungu, kiu iliyoongoza kila hatua ya utendaji wake. 'Caritas Christi urget nos”: " Upendo wa Kristo" unaotuchochea sisi sote , yalikuwa ni maneno yaliyorudiwa mara kwa mara na Kardinali Parolini katika mahubiri yake, kwenye ibada hii ya Misa ya Shukurani.