Kardinali Pietro Parolin akisalimiana na
Masista wa Upendo baada ya Ibada ya MIsa ya Shukurani , katika uwanja wa
Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Vatican 05.08.2016 - OSS_ROM
(Vatican Radio) Jumatatu hii majira ya saa nne za asubuhi, katika Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Jimbo Takatifu ,aliongoza Maadhimisho ya Misa ya Shukurani , kwa ajili ya Mama Tereza wa Calcutta kutangazwa Mtakatifu na Papa Francisko Jumapili iliyopita
Katika homilia yake, Kardinali Parolin alikumbuka mambo kadhaa muhimu katika maisha ya Mtakatifu Mama Tereza, hasa kiu yake kwa Mungu, kiu iliyoongoza kila hatua ya utendaji wake. 'Caritas Christi urget nos”: " Upendo wa Kristo" unaotuchochea sisi sote , yalikuwa ni maneno yaliyorudiwa mara kwa mara na Kardinali Parolini katika mahubiri yake, kwenye ibada hii ya Misa ya Shukurani.