Baba Mtakatifu Francisko anawaambia watumiaji wa mitandao ya kijamii kwamba, Ufalme wa mbinguni ni kwa ajili ya watu wanaojiaminisha kwenye upendo wa Mungu na wala si katika mambo ya kidunia.
Katika kilele cha Mwaka wa Imani, Baba Mtakatifu anatarajiwa, Jumamosi jioni kuongoza Ibada ya kuwapokea Wakatekumeni kama kielelezo cha kuvuka Mlango wa Imani, tayari kumpokea Kristo katika hija ya maisha yao ya Kikristo. Ibada hii inatarajiwa kuhudhuriwa na wakatekumeni kutoka sehemu mbali mbali za dunia kama kielelezo cha Ukatoliki wa Kanisa la Kiulimwengu.
Jumapili asubuhi, kwa mara ya kwanza waamini watapata fursa ya kutolea heshima kwa masalia yanayosadikiwa kuwa ni ya Mtakatifu Petro, Mwamba wa Imani, aliyeyamimina maisha yake kwa ajili ya Kristo na Kanisa lake. Ilikuwa ni Mwaka 1971, Papa Paulo VI alipopewa masalia haya yanayohifadhiwa kwenye Kikanisa cha Papa na kila mwaka ifikapo tarehe 29 Juni, Siku kuu ya Watakatifu Petro na Paulo miamba wa imani masalia haya hupelekwa kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican.
Katika Sherehe ya Kristo Mfalme wa Dunia, Baba Mtakatifu Francisko anatarajiwa kuongoza Ibada ya Misa Takatifu kama kilele cha kufunga Mwaka wa Imani, Ibada inayotarajiwa kuanza saa 4:30 kwa saa za Ulaya. Katika Ibada hii, Baba Mtakatifu atawagawia baadhi ya waamini Waraka wake wa kichungaji baada ya Maadhimisho ya Mwaka wa Imani unaojulikana kama "Furaha ya Injili" "Evangelii Gaudium", itakayozinduliwa rasmi, Jumatatu ijayo hapa mjini Vatican.
Walcot amekuwa akiigua kwa kwaribu miezi miwili
Theo Walcott huenda akaichezea
Arsenal siku ya jumamosi ikiwa kwa mara ya kwanza katika kipindi cha
zaidi ya miezi miwili baada ya kupona kutokana na majeruhi ya tumbo.
Walcott yumo katika kikosi cha kupambana na klabu yake ya zamani Southampton siku ya Jumamosi.
Walcott mwenye umri wa miaka
24-aliumia katika pambano la ligi dhidi ya Stoke September 22 baada ya
kutegua maumivu aliyopata katika pambano la siku nne zilizotangulia
dhidi ya Marseille.
"hajachezea hata kikosi cha akiba lakini nitamjumuisha katika kikos ikamili cha Jumamosi '' alisema kocha Arsene Wenger.
"yuko mzima kabisa."
Awali Wenger alimtumia Serge Gnabry kuchezea nafasi iliyoachwa na Walcott, lakini tangu wakati huo safu yake ya kiungo ilimaarishwa na kurejea kwa Mikel Arteta naJack Wilshere.
"Theo ana sifa tofauti na wachezaji wengine na nimefurahi sana kwamba amerejea" alisema Wenger
"hajachezea hata kikosi cha akiba lakini nitamjumuisha katika kikos ikamili cha Jumamosi '' alisema kocha Arsene Wenger.
"yuko mzima kabisa."
Awali Wenger alimtumia Serge Gnabry kuchezea nafasi iliyoachwa na Walcott, lakini tangu wakati huo safu yake ya kiungo ilimaarishwa na kurejea kwa Mikel Arteta naJack Wilshere.
"Theo ana sifa tofauti na wachezaji wengine na nimefurahi sana kwamba amerejea" alisema Wenger











