Wakizungumza kwa nyakati tofauti juzi na jana, wadau hao wameelezea
kufurahia kufikiwa na tamasha hilo la kimataifa ambalo litapambwa na
waimbaji wa ndani na nje ya Tanzania.
Kwa upande wake, Matata Ndizi, kati ya wadau wakubwa wa muziki wa
Injili, alisema angependa kumuona muimbaji Edson Mwasabwite katika
tamasha hilo.
“Kwanza tunashukuru kutuletea tamasha hilo mkoani Morogoro, lakini
kati ya waimbaji ambao tungependa kuwaona ni Edson Mwasabwite,” alisema
Matata.
Alisema amekuwa akibarikiwa sana anapomsikiliza mwimbaji huyo anayetamba na albamu yake ya ‘Ni Kwa Neema.’
“Mbali ya ukali wa kibao chake, Mwasabwite ni mwimbaji mpya, hivyo
wengi wangependa kumuona ‘live’ siku hiyo ya tamasha,” alisema.
Mwasabwite, mzaliwa wa Mbeya amekuwa aking’ara na albamu hiyo yenye
nyimbo nyingine saba, ambazo ni ‘Tarajia’, ‘Mujiza’, ‘Asante Yesu’,
‘Usiwe Mbali Nami’, ‘Bwana Yesu’, ‘Atanifuta Machozi’, ‘Milele
Usifiwe’ na ‘Mungu Wetu Anaweza’.
Mwingine aliyempendekeza Mwasabwite ni Innocent Kobelo wa Mafisa
mkoani humo, ambaye amekiri kuwa amekuwa akivutiwa naye hivyo angefurahi
kumwona ‘live’
.
Waandaaji wa Tamasha la Krismasi, wamebainisha kuwa wamepania
kulifanya liwe la aina yake tofauti na mengineyo kwa kualika waimbaji
maarufu ndani ya nje ya nchi, ambako tayari wamemtangaza Upendo Nkone
kuwemo katika tamasha hilo litakaloanza kukata utepe Desemba 25 jijini
Dar es Salaam.
Week Hot newz
-
Neno Kwaresima linatokana na neno la lugha ya kilatini Quadragesima ; maana yake, namba arobaini. Kwa hiyo, Kwaresima ni kipindi cha siku ...
-
T upo pamoja tena nawe katika jiji la upendo wa Mungu, yaani Neno lake ambalo daima latupatia uzima na pia latufanya tuwe huru katika mai...
-
Kwa kawaida mwanachama wa chama au kikundi chochote kile anakuwa na kitambulisho maalumu na anaona fahari kutangaza sera za chama au za...
-
Mpendwa mwana wa Mungu, tuko tena pamoja katika ile habari ya furaha ndiyo kushirikishana mapendo ya Mungu kwa njia ya meza y...
-
Machachari is a children comedy/ adventure series that depicts the friendship bet...
-
Kumsadiki Roho Mtakatifu ni kukiri Nafsi ya tatu ya Fumbo la Utatu Mtakatifu, atokaye kwa Baba na Mwana na anayeabudiwa na kutu...
-
Mpendwa msikilizaji wa Radio Vatican kipindi cha tafakari, ninakuleteeni tafakari ya Neno la Mungu Dominika ya tatu ya Majilio. Mas...
-
MAANDALIZI ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka huu ni ya kipekee kutokana na kupambwa na mbwembwe nyingi ikiwamo misafara na maandamano m...
-
MKUU wa msafara wa timu ya taifa ya wanawake ya Afrika Kusini chini ya miaka 20, Peter Manchonyane, ameelezea wasiwasi wa kikosi chake ku...
-
Tunaendelea kama kawaida katika kipindi chetu, tafakari masomo Dominika, na leo tunatafakari masomo Dominika ya 33 ya mwaka C wa Kanisa...


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni