Week Hot newz
-
Neno Kwaresima linatokana na neno la lugha ya kilatini Quadragesima ; maana yake, namba arobaini. Kwa hiyo, Kwaresima ni kipindi cha siku ...
-
Takwimu zinaonesha kwamba, tangu Baba Mtakatifu Francisko alipochaguliwa kuliongoza Kanisa Katoliki hapo tarehe 13 Machi 2013, zaidi ya w...
-
Kwa kawaida mwanachama wa chama au kikundi chochote kile anakuwa na kitambulisho maalumu na anaona fahari kutangaza sera za chama au za...
-
Machachari is a children comedy/ adventure series that depicts the friendship bet...
-
Ijumaa Kuu Baba Mtakatifu Francisko majira ya saa tatu na nusu za usiku, ataongoza Ibada ya njia ya Msalaba katika ene...
-
Baba Mtakatifu mapema Jumatano, ametoa Katekesi kwa mahujaji na wageni waliokuwa wamekusanyika katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mta...
-
“Katika Waraka Uso wa huruma, maalum kwa ajili ya kuzindua Maadhimisho ya Mwaka Mtakatifu wa Jubilei ya huruma ya Mungu niliwaomba kwamb...
-
Baba Mtakatifu Francisko hivi karibuni ameridhia kuchapwa kwa nyaraka mbali mbali zinazowahusu watumishi wa Mungu na wenyeheri ...
-
MAKAO Makuu ya Kanisa Katoliki Duniani, yamekanusha vikali uvumi ulioenea kwamba Baba Mtakatifu, Francis, yuko hatarini kwa kuwa kundi l...
Vatican: Papa Francis hayuko hatarini
MAKAO Makuu ya Kanisa Katoliki Duniani, yamekanusha vikali uvumi ulioenea kwamba Baba Mtakatifu, Francis, yuko hatarini kwa kuwa kundi la kimafia linamuwinda kumfanyia uhalifu kwa kile kilichoelezwa kuhusu uamuzi wake wa kufanya mageuzi katika kanisa hilo.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari wa Vatican, Frederico Kardinali Lombard, alikiambia kituo cha habari cha ABC kwamba hakuna sababu za wazi zinazoweza kuwafanya kuwa na wasiwasi.
“Tuna utulivu wa kutosha, hakuna haja ya kuanza kuwekeana mashaka,” alisema.
Habari zilizonukuliwa hivi karibuni zilimtaja Nicola Gratteri anayeheshimika nchini Italia kwa msimamo wake kinyume na kundi hilo la Mafia akisema kuwa uamuzi wa Baba Mtakatifu kutaka kulifanyia marekebisho kanisa ulilikasirisha kundi hilo la kijasusi.
“Siwezi kusema kama Mafia wanaweza kufanya kitendo hiki, tunawajua kuwa ni watu hatari,” aliongeza Lombard.
Gratteri alilianyia uchunguzi wa kutosha kundi hilo lenye nguvu duniani lenye makazi yake Calabria, Kusini mwa Italia katika sehemu inayoitwa Ndrangheta.
Aliyaongea hayo kwenye kipindi cha televisheni alipokuwa anazindua kitabu chake cha maji matakatifu, kinachohusu Kanisa Katoliki na vikwazo linavyopata katika eneo hilo la Ndrangheta.
Grateri ananukuliwa akisema kuwa uamuzi wa Papa utaangusha nguvu ya kibiashara iliyoko katika mamlaka za Vatican ikiwemo Benki ya Vatican iliyokuwa inafanya biashara zilizolaumiwa kama ni za kiukoo kati ya makleri wa eneo hilo.
Ingawa kwa kiasi kikubwa mauaji yaliyokuwa yanapangwa na Mafia yamepungua kwa kiasi kikubwa tangu miaka ya 1990, matendo ya kihalifu bado yanafanywa na vikundi vinavyojihusisha na ukahaba na watumiaji wa dawa za kulevya, hayo ndio makundi hatari kwa ukuaji wa uchumi wa Italia.
Koo kubwa zinazopatikana Italia kwa sasa zinahusisha, Wasisili wa Cosa Nostra, Wakamora wanaotoka mji wa Napoli, na Kalabrian maarufu kama Ndrangheta, ambao unasadikiwa kuwa wenye nguvu katika matendo ya kihalifu, hii ni kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa.
Tayari Baba Mtakatifu ameshatangaza kufanya mabadiliko makubwa katika kanisa, akitaka kanisa la kimaskini kwa ajili ya maskini, na ndani ya wiki hii ameshazungumza mara mbili katika misa zake za asubuhi akikemea vitendo vya rushwa na fedha chafu.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni