Kocha Mkuu wa timu ya soka ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars), Kim Poulsen, amesema timu yake mesto wa yosso na wazoefu, iko tayari kuikabili Zambia (Chipolopolo) katika mechi yake ya kwanza ya kuwania ubingwa wa mashindano ya Kombe la Chalenji itakayofanyika kesho kwenye Uwanja wa Nyayo jijini hapa.
Akizungumza jana, Poulsen alisema wachezaji wake wote wako tayari na wamejiandaa kufanya vizuri katika mechi hiyo ya kwanza ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kusonga mbele.
Poulsen alisema mechi dhidi ya Chipolopolo inatarajiwa kuwa ngumu kwa sababu wachezaji wengi wa Zambia ni wauzoefu tofauti na kikosi chake ambacho mwaka huu ni mseto kutokana na kujumuisha yosso wengi aliowaita kwa mara ya kwanza, lakini anaamini watafanya vizuri.
"Tuko tayari, tumejiandaa kwa mashindano na tunaamini tutaanza vyema mechi yetu," alisema Kocha huyo raia wa Denmark.
Aliongeza kuwa, katika kundi lao ambalo linajumuisha timu ya Somalia na Burundi, hakuna mechi nyepesi kwa sababu kila moja imekuja kushindana na si kushiriki.
Naye mshambuliaji mahiri wa timu hiyo, Mrisho Ngasa, aliliambia blogu hili kuwa wamekuja Nairobi kushindana na watajituma ili kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania Bara.
Ngassa alisema anajua Watanzania wamewatuma kuiwakilisha vyema na hicho ndicho wamepanga kukitekeleza.
"Tunajua jukumu letu na tunamuomba Mungu tufanye vizuri, tuombeeni ili tufanye kile ambacho kocha ametuelekeza," alisema Ngasa.
Kilimanjaro Stars iliyoko Kundi B, ilitua jijini hapa juzi usiku na itacheza mechi yake ya pili Desemba Mosi dhidi ya Somalia huku ikimaliza hatua ya makundi kwa kuivaa Burundi hapo Desemba 4, mwaka huu.
Uganda ndiyo mabingwa watetezi wa mashindano hayo yanayofanyika kila mwaka kwa kushirikisha nchi wanachama wa Cecafa na timu alikwa.
Week Hot newz
-
Utafiti mpya umeonesha watu wazima wengi duniani ni wanene kupita kiasi na kwamba hakuna matumaini ya kufikia lengo la kupunguza idadi...
-
November 13 Patron of immigrants Died: 1917 St. Frances Xavier Cabrini, Virgin (Feast day November 13) St. Frances was born in Lombar...
-
Reading 1, First Corinthians 15:35-37, 42-49 35 Someone may ask: How are dead people raised, and what sort of body do the...
-
1.1. NDUGU WADOGO KUPAMBANA HADI KUTENGANISHWA (1226-1517) 1.1.1. MWANZO WA MAPAMBANO (1226-1318) Mt. Fransisko...
-
DUNIA leo inaadhimisha Siku ya Kisukari. Ni ukweli usiokuwa na chembe ya shaka kuwa katika miaka ya karibuni ugonjwa wa ki...
-
Machachari is a children comedy/ adventure series that depicts the friendship bet...
-
Reading 1, Sirach 47:2-11 2 As the fat is set apart from t...
-
Mpendwa mfuatiliaji wa blogu hii endelea kusoma tuhekimishane kuhusu yale yahusuyo maisha ya ndoa na familia. Kwa vipindi k...
.jpg)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni