Asamoah Gyan mshambuliaji wa Ghana
Ghana na Algeria jumanne
zimeungana na timu za Nigeria, Ivory Coast na Cameroon kukamilisha nchi
tano zitakazowakilisha bara la Afrika katika fainali za kombe la dunia
nchini Brazil mwaka 2014.
Ghana wakicheza ugenini dhidi ya Misri pamoja na
kufungwa magoli 2 - 1 walifanikiwa kufuzu kucheza fainali za kombe la
dunia kwa vile katika mechi ya awali Ghana iliifunga Misri magoli 6 - 1


