Week Hot newz

Papa kuadhimisha Siku ya Watawa Duniani!



Baba Mtakatifu Francisko katika Maadhimisho ya Siku kuu ya Kutolewa Bwana Hekaluni sanjari na Siku ya Watawa Duniani, Jumapili ijayo tarehe 2 Februari 2014, kuanzia saa 4:00 asubuhi kwa saa za Ulaya anatarajiwa kuadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican.


Tiketi za kuingilia kwenye Ibada hii zinapatikana kwenye Ofisi za Baraza la Kipapa la Mashirika ya Kitawa na Kazi za Kitume iliyoko mjini Roma kuanzia Alhamisi tarehe 30 hadi Ijumaa tarehe 31 Januari 2014, kuanzia saa 2:30 hadi saa 7: 00 Mchana

Masalia ya Mwenyeheri Yohane Paulo II yaibwa mjini Aquila!



Askofu mkuu Giuseppe Petrocchi wa Jimbo kuu la Aquila, Italia amewaandikia waamini wake barua kuonesha masikitiko makubwa baada ya watu wasiojulikana kuvunja Madhabau ya Mtakatifu Petro della Jenca na kuiba masalio ya damu ya Mwenyeheri Yohane Paulo II na kufanya kufuru ndani ya Kanisa,