Billy
Saro Harrison is the second-born of the Harrison brothers who form Them
Mushrooms. They are a Nairobi-based band which hails from Mombasa.
Harrison made a very interesting observation on television last week
when he asked to explain the difference between music making now and in
the past. Saro, the bass guitarist, flanked by elder brother Teddy
Kalanda Harrison (Tenor saxaphone, percussion, composer, vocals),
younger brothers George Ziro Harrison (playing guitar on the TV set) and
John "Bishop" Katana Harrison (keyboards, composer and vocals), said
the kids coming into music today are making music for now.They have little
thought about what comes next or much care as to how they can make music
that will stand the test of time and still be relevant in 10 or more
years. In short he seemed to suggest the nature of the industry has been
changed by those in charge of it.
Serikali ya
Uingereza imeanzisha uchunguzi wa dharura kufuatia ufichuzi kuwa
wachezaji nyota wa kandanda nchini Uingereza wamekuwa wakitumia madawa
yaliyopigwa marufuku ya kuongeza nguvu mwilini.Gazeti la Sunday
Times limechapisha ripoti ya uchunguzi iliyothibitisha kuwa sio tu
wasakataji dimba bali hata waendesha baiskeli, wachezaji Kriketi na hata
wachezaji wa tenisi wamekuwa wakipokea matibabu kutoka kwa daktari
mmoja ambaye anajulikana kwa kupeana madawa hayo yaliyopigwa marufuku ya
kututumua misuli.
Daktari Mark Bonar ambaye anazahanati yake
mjini London Uingereza amekuwa akiwatoza wachezaji nyota maelfu ya pauni
za Uingereza kwa matibabu hayo fiche ambayo imegunduliwa kuwa ni
matibabu ya madawa yaliyopigwa marufuku na shirikisho la kupambana na
madawa haramu WADA.
Wateja wakuu wa Dkt Bonar yasemekana ni wachezaji wa timu kuu katika ligi maarufu zaidi duniani ligi ya Uingereza.Uchunguzi
pia umebaini kuwa dkt Bonar amekuwa akiwapa wachezaji nyota 150 dawa
aina ya EPO Steroids na hata homoni zinazokua kwa haraka ambazo ni
haramu katika michezo katika kipindi cha miaka 6 sasa.
Serikali ya Uingereza imeanzisha uchunguzi dhidi ya taasisi ya kupambana na kuenea kwa madawa hayo haramu kufuatia ufichuzi huo.
Hakuna ushahidi kuwa timu za ligi kuu ya Uingereza zilifahamu mbinu za Dkt Bonar.
Aidha Sunday Times linasema kuwa halina ushahidi
'huru' kuwa dkt Bonar aliwapa madawa hayo ya kututumua misuli wachezaji
wangapi wanaochezea vilabu vya ligi kuu ya Uingereza EPL.Hata
hivyo wachezaji kadhaa walioulizwa iwapo walipewa madawa hayo ya
kututumua misuli na dkt Bonar walikataa kujibu na wengine wakakanusha
madai hayo ya daktari huyo.
Dkt Bonar hata hivyo anasema kuwa
hakuwapa wachezaji hao madawa hayo kwa nia ya kuimarisha uwezo wao
uwanjani ila anadai aliwapa madawa hayo ilikuwatibu dhidi ya maradhi
mbali mbali waliokuwa wanaugua.
Uchunguzi huu unatokana na
ufichuzi wa mchezaji mmoja aliyekwenda kwa idara ya serikali kumshtaki
dkt Bonar kwa kumpa dawa iliyopigwa marufuku.
Mchezaji huyo ambaye
ametaka jina lake libanwe anasema alipigwa na butwaa dkt Bonar
aliposisitiza kuwa anastahili kumeza dawa hiyo haramu.
Sunday
Times lilitumia mwanariadha chipukizi kumrekodi daktari huyo akijigamba
jinsi alivyowatibu wachezaji wengi tu nyota akitumia mbinu zizo hizo
japo ni marufuku.
Almighty God, my Eternal Father, from the fullness
of my soul I adore You. I am deeply grateful that You have made me in
Your image and likeness, and that You ever hold me in Your loving
embrace. Direct me to love You with all my heart, with all my soul, and
with my whole mind. Direct me to love all Your children as I love
myself. O, my Father, my soul longs to be united to You, and to rest in
You forever. Have the Holy Spirit touch my soul so that I may love You
as He does, and as Your Beloved Son Jesus does. Amen.
Mji
wa Nazareti ukionekana hapo juu,Mat 2:23, watu wengi walikuwa wakulima,
Yesu na Josefu walikuwa maseremala, hivyo ilikuwa rahisi kufahamika. Jangwa la Yudea, linatukumbusha safari ya waisrael, Kujaribiwa kwa Yesu na maisha ya Yohana kuna wakati alikaa Jangwani. MEGIDO,Armageddoni mahali ambapo vita ya mwisho itapiganwa, this is real, bible haijaficha kitu. Hili kaburi la Yesu hata sasa yapo mti aliopanda Zakayo wakati anataka kumwona Yesu ''live'' Yesu
lipoingia nyumbani mwa Zakayo akasema ''wokovu umeingia nyumbani mwa
Zakayo''
Kwa
kawaida mwanachama wa chama au kikundi chochote kile anakuwa na
kitambulisho maalumu na anaona fahari kutangaza sera za chama au za
kikundi chake. Leo tutakiona kitambulisho cha Kristu mfufuka
anachotakiwa kukivaa mfuasi wake. Injili ya leo inaeleza awamu mbili
ambazo Yesu mfufuka anakutana na wanafunzi wake.
Awamu ya kwanza ilikuwa
jioni ya siku ile aliyofufuka (Jumapili), “Ikawa jioni, siku ile ya kwanza ya juma, pale walipokuwapo wanafunzi, milango imefungwa kwa hofu ya Wayahudi.” Awamu ya pili ilikuwa siku nane baadaye. Katika awamu zote mbili
kikundi hiki kidogo cha wanafunzi kilijitenga na kujifungia ndani ya
chumba kwa hofu ya Wayahudi. Mandhari hii inawakilisha hali halisi
ya mahusiano yaliyoko kati ya vyama na vikundi vingi, ambapo wanachama
wake hujifungia katika ulimwengu wa itikadi zao tu na kuwaogopa walio
nje kama wapinzani. Hapo inazuka hofu inayomgeuza mtu hadi kuwa wa
siasa kali, yaani kukereketwa kunapitiliza mipaka. Kama mkereketwa huyo
ni mkristo basi atajifungia katika akili na utashi wake bila kutaka
majadiliano na yeyote asiyefuata itikadi za dini yake. Mtu wa aina hiyo
atanadisha sera za imani yake kwa kupandisha majini na kupaza sauti,
hata kuwadhulumu wengine. Hizo ni alama wazi za hofu iliopitiliza. Katika historia ya Ukristo, kumewahi
kuwa na vipindi vya hofu kama hiyo. Kumekuwa na hofu ya elimu ya
sayansi, kwamba ingeweza kuharibu imani ya kikristo. Kadhalika hofu ya
elimu ya mambo ya kale na teknolojia hasa ya nadharia ya mvuvumko
iliyoonekana kupingana na nadharia ya uumbaji. Kanisa likahofu kuwa
ulimwengu huo ungeangamiza na kuharibu dini ya kikristo. Kumbe mkristo
hatakiwi kuuhofu ukweli, kwani akili ya binadamu imeumbwa na Mungu ili
kuujua na kutafuta ukweli.
Yesu alitangaza Injili ya ukweli na akataka
ukweli wa Injili uenee ulimwenguni.“Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli; tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.” (Yoh 8:30-31). Kujitenga na kujifungia ndani ni hofu
itokanayo na kutojua kitambulisho cha Yesu Kristo mfufuka. Hofu
iliyosababishwa na kutomjua Kristo mfufuka kwamba maisha yake ya upendo
na huruma yasingeweza kufa tu basi, bali yanadumu milele. Katika
mazingira ya hofu, Yesu ajitokeza katikati ya wanafunzi wake na
kuwaonesha kitambulisho vyake. “Akaja Yesu, akasimama katikati, akawaambia, Amani iwe kwenu. Naye akiisha kusema hayo, akawaonesha mikono yake na ubavu wake.” Kitambulisho cha mfufuka ni mikono na ubavu wake. Mikono iliyotobolewa misumari na kusulubiwa ni alama ya nguvu. “Mkono wa kuume wa Bwana umetenda makuu.” (Zab 118:15).
Kwa hiyo, Yesu anaonesha mikono aliyotumia kutenda matendo ya huruma
kama vile kuwaponya wakoma, kuwaponya vipofu na viziwi, kumwokoa Petro
alipotaka kuzama majini, kuwabeba watoto, mikono iliyoosha miguu ya
mitume nk. Kitambulisho hiki cha Yesu chatakiwa kiwe cha kila mbatizwa,
yaani kutumikia na kutenda matendo ya huruma. Kadhalika ubavuni
ilikotoka damu na maji baada ya kuchomwa moyo uliojaa upendo na huruma.
Mkristo asukumwe na moyo wa huruma na upendo katika kutumikia na kutenda
mema.
Mapato ya Yesu kuwa katikati yao,“Wanafunzi walifurahi kumwona Bwana.”
Hapa wanafunzi wanayo furaha ya kweli anapokutana na kuona kuona
vitambulisho vya aliyetoa maisha yake kwa ajili wengine. Hivi wafuasi wa
Kristu wanafurahi kukutana na yule anayefahamu uzuri wa kutoa maisha
kwa ajili ya wengine. Baada ya kufurahiana huko, Yesu anawaingiza
wanafunzi wake katika ufuasi.“Yesu
anawatuma mitume wake akasema: Kama Baba alivyonituma mimi nami nawatuma
ninyi. Kisha akawavuvia na kusema: Pokeeni roho mtakatifu.” Kuvuvia
ni kuingiza roho, yaani kutia nguvu ya Mungu ndani ya mitume. Zawadi ya
nguvu za Mungu iliyomfanya Yesu kuleta maisha duniani sasa
wanashirikishwa wote na kutumwa kwenda ulimwenguni bila hofu kama kondoo
kati ya mbwa mwitu. Wanaagizwa, “Wowote mtakaowasamehe wamesahemewa, wale mtakaowafungia watakuwa wamefungiwa”
yaani kila mmoja anao wajibu wa kuwatoa watu toka njia mbovu ya dhambi
na kuwaongoza katika njia iliyo sawa inayoelekea kwenye utakatifu wa
maisha! Baada ya mitume kuingizwa uanachama
wa kundi la Kristu, sasa awamu ya pili inahusu kupewa vitambulisho
wafuasi wengine tuliobaki. Ndiyo maana katika awamu hii tunaambiwa
ilikuwa ni siku nane baadaye. Maana yake siku ya kwanza baada ya kwisha
siku saba rasmi za uumbaji, Sasa hufuata maisha ya kawaida ya binadamu.
Sisi waanzaji wenye mashaka tunawakilishwa na Tomaso. “Baada
ya siku nane, wanafunzi wake walikuwamo ndani tena, na Tomaso aitwaye
Pacha pamoja nao. Akaja Yesu, na milango imefungwa, akasimama katikati
yao.”
Tomaso anaitwa Pacha (Didimo) maana yake mawingu. Kwa hiyo huo ni
mwito kwetu wa kujitambua kuwa ni mawingi au pacha wa Tomaso. Tunafanana
na Tomaso katika mahusiano yetu na Yesu. Yaonekana Tomaso hakuuogopa
ulimwengu kama wale mitume waliojifungia chumbani. Aidha isieleweke
kwamba alikuwa mpinzani na Yesu. Tomaso hakuwa mpinzani wala hakuwa na
hofu ya Wayahudi bali alipeta tu nje. Lakini kwa vyovyote alifanana na
mitume katika kuona mashaka juu ya ufufuko. Hali ambayo mara nyingi Yesu
anawagombeza mitume kwa kutokusadiki kwao (Marko). Tomaso alianza
kulifanya kosa hilo kwa kujitenga na jumuiya yake. Hivyo ndivyo
inavyotokea katika maisha ya kila siku katika vikundi mbalimbali.
Hebu tuone ni katika kipengele gani mkristu ni mawingi au pacha,
yaani analingana na kutokulingana na Tomaso aitwaye Pacha (Didimo).
Pacha asiyelingana na Tomaso Didimo ni yule aliyejitenga na jumuiya yake
na kuwadharau wote waliomo humo kuwa hawafai. Huyo ni sawa na anayehama
chama cha siasa na kukidharau wakati kimlea na kumkuza hadi kufikia
ujiko alionao kwa sasa!. Mwanachama wa kweli ni yule anayebaki imara
katika chama hata kama baadhi ya wanajumuyia wake wana makwazo, kwa
sababu kuna sera na mambo mema yaliyomo humo; ni mtu anayethubutu kuleta
mageuzi kwa kubaki ndani ya chama! Ndivyo inavyotokea katika Ukristo,
kuna wale wanaoasi dini na kujiunga na dini nyingine kwa sababu tu
wanajisikia kukatishwa tamaa kutokana na makwazo yanayofanyika humo,
kama vile mfumo mbovu wa uongozi, utajiri uliokithiri au kanisa
kushindwa kutoa majibu sahihi kwa maswali na shida mbalimbali za
waamini. Kumbe, pacha anayelingana na Tomaso ni yule baada ya kuona
makwazo hayo, hata kama anashawishika kujitenga na ukristu kwa muda ili
kuona ukweli utakaoibuka kutokana na muda unavyopita lakini anarudi
tena. Mtu huyo anafanana na yule anayekwepa moshi ili kuweza kuona
vizuri ukweli ulipo. Tomaso hakuasi kundi, ndiyo maana
anarudi kundini kuhakikisha kwa akili yake kama upepo umebadilika. Hapo
ndipo anapokosa imani pale anapotaka kuuelewa tena kwa kugusa ufufuko wa
Kristo. Ufufuko wa wafu hauwezi kufahamika kwa akili ya kibinadamu.
Tomaso hakufahamu kwamba binadamu tunayo mang’amuzi ya kimwili tu, kumbe
ukweli na mang’amuzi yaliyo ndani ya kaburi unajulikana na yule tu
aliye ndani ya vuguvugu zake, yaani mfu peke yake kwani “Adhabu ya kaburi aijuaye maiti.” Kumbe
siri ya kaburi anaijua Yesu peke yake mwenye mang’amuzi ya ya kufa na
kufufuka. Kwa njia ya Mungu peke yake binadamu tunaweza kuuelewa
ufufuko. Kwa hiyo Pacha wetu Tomaso kama
binadamu asingeweza kupata jibu alilolitegemea. Ndiyo maana Kristo
mfufuka akamtaka asiendelee kutosadiki bali awe na imani na kusadiki. “Wewe, kwa kuwa umeniona, umesadiki; wa heri wale wasioona wakasadiki.” Mapato yake, Tomaso akabaki tu kuinamisha kichwa na kusema: “Bwana wangu na Mungu wangu.”
Inatosha kwetu kujua kwamba kitambulisho cha mfuasi wa kweli wa Kristo
Mfufuka ni mikono inayohudumia na moyo (ubavu) alama ya upendo. Leo
tunafundisha kutafakari fumbo hili la ufufuko tunapotenda matendo ya
huruma. Tunapokuwa na mashaka tumwige pacha wetu Tomaso na kusali: “Bwana wangu na Mungu wangu.”
"Amoris Laetitia" "Furaha ya Upendo"
ndani ya familia ni Wosia wa kitume utakaozinduliwa hapo tarehe 8 Aprili
2016, tayari waamini kutangaza na kushuhudia Injili ya familia!
Padre
Federico Lombardi Msemaji mkuu wa Vatican, Alhamisi tarehe 31 Machi 2016
ametangaza rasmi kwamba, Waraka wa Wosia wa Kitume wa Baba Mtakatifu
Francisko kuhusu Injili ya familia, utazinduliwa rasmi hapo tarehe 8
Aprili 2016. Waraka huu unajulikana kwa lugha ya Kilatini kama “Amoris
Laetitia” “Furaha ya Upendo” ndani ya familia. Waraka
huu ni matunda ya maadhimisho ya Sinodi mbili za Maaskofu kuhusu
familia. Sinodi ya kwanza iliadhimishwa kunako mwaka 2014 na awamu ya
pili kunako mwaka 2015, kuonesha jinsi ambavyo Kanisa linatoa uzito wa
juu kabisa kuhusu wito na utume wa familia ndani ya Kanisa na ulimwengu
mamboleo!
Uzinduzi wa Wosia wa kichungaji wa Baba Mtakatifu Francisko “Amoris
Laetitia” “Furaha ya upendo” ndani ya familia utafanywa na Kardinali
Lorenzo Baldisseri, Katibu mkuu wa Sinodi za Maaskofu; Kardinali
Christoph Shonborn, Askofu mkuu wa Vienna pamoja na Professa Francesco
Miano na mkewe Professa Giusephina De Simone.
Utafiti mpya
umeonesha watu wazima wengi duniani ni wanene kupita kiasi na kwamba
hakuna matumaini ya kufikia lengo la kupunguza idadi ya watu wanene
duniani.
Wanasayansi waliofanya utafiti huo ambao walitoka Chuo
cha Imperial cha London, wakiandika katika jarida la kimatibabu la
Lancet la Uingereza, wanasema miongo minne iliyopita, kuwa na uzani wa
chini kupita kiasi lilikuwa tatizo kubwa kuliko unene.
Wanasema idadi ya wanaume wanene imeongezeka mara tatu, nayo ya wanawake ikaongezeka mara dufu.
Profesa Majid Ezzat, aliyeongoza utafiti huo, anasema ni kana kwamba kuna "mkurupuko wa unene".
Wanasayansi
hao wanaonya kwamba tatizo hilo ni kubwa sana kiasi kwamba haliwezi
kutatuliwa kupitia njia za kawaida za matibabu au kutenga maeneo ya
kuendeshea baiskeli.
wanandoa wanene Duniani ni awa.
Baada
ya kuchunguza takwimu kutoka nchi 186, watafiti hao walibaini kwamba
idadi ya watu wanene duniani imeongezeka kutoka 105 milioni mwaka 1975
hadi 641 milioni mwaka 2014.Idadi ya watu walio na uzani wa chini ya kuwango imeongezeka kutoka 330 milioni hadi 462 milioni katika kipindi hicho.
Viwango
vya unene miongoni mwa wanaume kilipanda kutoka 3.2% mwaka 1975 hadi
10.8%, na miongoni mwa wanawake viwango vya unene vilipanda kutoka 6.4 %
mwaka 1975 hadi 14.9%.
Hii ina maana kulikuwa na wanaume wanene 266 milioni na wanawake wanene 375 milioni mwaka 2014.
MSANII wa Bongo Fleva na nyimbo asili ya Kitanzania, Paskal Linda ‘Batarokota’, amesema kukithiri kwa
matumizi ya dawa za kulevya, utoaji mimba, ufisadi, choyo, dhuruma, kutosamehana katika jamii zinazo tuzunguka kunatukosesha na huruma ya Mungu.
“Mimi binafsi nashindwa kuelewa kwanini jamii inayotuzunguka tunajitumbukiza
kwenye matumizi ya dawa za kulevya, utoaji mimba, utumiaji dawa wa kuzuia mimba, utumiaji wa kondomu, ufisadi, choyo, dhuruma,uuaji, uzinzi, uasherati, na kila siku tunafanya lakini tumeshindwa kumrudia Mungu wa huruma kwa kuomba toba kwa Mungu wa huruma, inabidi
tupigane kwa pamoja kwa nguvu moja kukataa uibilisi kwa kutumia hata mitandao ya facebook, blogu,tovuti twitter, au kutumiana sms za mafundisho kwa simu, huku tukishirikishana sisi kwa sisi kumuomba Mungu toba kila siku na upendo wake wa Kimungu ili uwe nasi” alisema Batarokota.
Batarokota akizungumza leo na mwandishi wa blogu hii leo asubuhi baada ya kuudhuria misa katika kanisa la St Josephine Bakhita Oilcom nane nane Morogoro, aliongeza kwa wanajamii ya Mungu na watoto wa baba mmoja, wana nafasi kubwa kwa kutumia mitandao kukemea uovu na mambo yasiyo kuwa na utukufu wa Mungu.
“Kinachotakiwa kwa sasa, wanajamii wote tumie fursa za kushirikishana kwa njia ya mitandao ya kijamii kutangaza habari njema, siyo kujiingiza katika matumizi au uuzaji
wa dawa za kulevya,utoaji mimba, uchoyo, ulevi wa chakula, pombe na madaraka, ’’ alifafanua Batarokota.