Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya kwa kushirikiana na Serikali linaendelea kuwahamasisha wananchi wa Kenya na Afrika kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kumpokea na kusali pamoja na Baba Mtakatifu Francisko wakati wa hija yake nchini Kenya kuanzia tarehe 25 hadi tarehe 27 Novemba 2015.
Week Hot newz
-
Matumizi haramu ya dawa za kulevya ni janga kwa vijana we...
-
A Prayer for a Family O dear Jesus, I humbly implore You to grant Your special graces to our family. May ou...
-
Mpendwa msikilizaji wa Radio Vatican kipindi cha tafakari, ninakuleteeni tafakari ya Neno la Mungu Dominika ya tatu ya Majilio. Mas...
-
Viongozi wa Jumuiya ya Kimataifa pamoja na wananchi wa Afrika ya Kusini wameanza kutoa heshima zao za mwisho kwa Tata Madiba kwa sala kut...
-
Baba Mtakatifu Francisko wakati akirejea kutoka Armenia a...
-
Watawa wa Mama Theresa wa Calcutta waliouwawa huko Yemen ni mashuhuda wa upendo na wahanga wa utandawazi usiojali wala kuguswa na maha...
-
MOROGORO,TANZANIA. MSANII wa bongo fleva na mkali wa kurap kwa lugha 31 Batarokota, amesema tangu alipofariki mke wake mpendwa mwaka ...
-
Siku ya kumbukumbu ya kukumbuka ajali ya MV Bukoba tareehe 21/05/2016 katika jijini la mawe Mwanza (Rocky City) kutakuwa na burudani kabam...
-
Pichani juu msanii wa nyimbo za asili ya Kitanzania Batarokota akiwa katika Hoteli ya Misana aliyofikia jijini Mwanza.. MSANII wa ny...
-
KUNA changamoto nyingi ambazo wagonjwa wa saratani wanakutana nazo hasa kwa wanawake ambao wana saratani ya titi. Changamoto hizo zimes...
Kenya na Afrika kwa ujumla wajiandaa kumpokea Papa Francisko
Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya kwa kushirikiana na Serikali linaendelea kuwahamasisha wananchi wa Kenya na Afrika kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kumpokea na kusali pamoja na Baba Mtakatifu Francisko wakati wa hija yake nchini Kenya kuanzia tarehe 25 hadi tarehe 27 Novemba 2015.
Vatican na Zambia waadhimisha Jubilei ya miaka 50 ya mahusiano ya kidiplomasia
Zambia na Vatican zinaadhimisha Jubilei ya miaka 50 ya uhusiano wa kidiplomasia. - ANSA
Akiwa nchini Zambia, Askofu mkuu Gallagher amepata nafasi ya kukutana na kuzungumza na viongozi wa Kanisa, Serikali ya Zambia chini ya uongozi wa Rais Edgar Chagwa Lungu pamoja na Mabalozi na wawakilishi wa Jumuiya ya Kimataifa nchini Zambia. Askofu mkuu Gallagher amebahatika kuadhimisha Ibada ya Misa Takatifu katika Makanisa kadhaa kwa kukazia umuhimu wa Zambia kuendelea kuwa ni udongo mzuri kwa ajili ya kupandikiza Habari Njema ya Wokovu. Akiadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwa Majandokasisi wa Seminari kuu ya Mtakatifu Dominiko, Askofu mkuu Gallagher amewataka Waseminari hao kufanya tafakari ya kina kuhusu maisha na wito wao, daima wakilenga juu zaidi kwa kuonesha upendo na uaminifu.
Akizungumza na Rais Edgar Chagwa Lungu, wakati wa kumbu kumbu ya Jubilei ya Miaka 50 ya mahusiano ya kidiplomasia kati ya Zambia na Vatican, Askofu mkuu Galagher amepongeza mahusiano mazuri ya kidiplomasia kati ya Vatican na Zambia pamoja na mchango mkubwa unaotolewa na Kanisa katika ustawi na maendeleo ya wananchi wote wa Zambia. Kanisa kwa namna ya pekee, limekuwa mstari wa mbele katika huduma kwa maskini na wote wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii. Mahusiano ya kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili yanalenga kwa namna ya pekee kudumisha na kuimarisha huduma kwa familia ya binadamu, kwa kujikita katika mchakato wa maendeleo endelevu, haki na amani. Serikali ya Zambia kwa namna ya pekee, inalipongeza Kanisa Katoliki kwa mchango wake katika maendeleo ya wananchi wengi wa Zambia, lakini zaidi katika sekta ya elimu na afya.
Askofu mkuu Gallagher, amepata pia nafasi ya kutembelea nchini Malawi, huku akiongozana na Askofu mkuu Julio Murat, Balozi wa Vatican nchini Zambia na Malawi, ambako amepokelewa na viongozi wa Kanisa na Serikali ya Malawi. Viongozi hawa katika mazungumzo yao wamegusia kwa namna ya pekee, mambo msingi katika mchakato wa maendeleo endelevu ya wananchi wa Malawi, ambao kwa sasa wanakabiliwa na changamoto nyingi, lakini kwa namna ya pekee baa la njaa na umaskini.
Askofu mkuu Tarcisius Zizaye, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Zambia, amemshukuru kwa namna ya pekee kabisa Baba Mtakatifu Francisko kwa kuijali Familia ya Mungu nchini Malawi katika shida na mahangaiko yake; wakati wa raha na machungu. Kwa upande wake, Askofu mkuu Richard Paul Gallagher amewasilisha salam za Baba Mtakatifu Francisko anaendelea kuonesha moyo wake wa upendo na sala kwa wale wote walioathirika kutokana na mafuriko pamoja na ukame wa kutisha nchini Malawi. Askofu mkuu Gallagher katika Ibada ya Misa Takatifu, akiwa Malawi, amewataka waamini kuwa ni mashuhuda wa mwanga wa Injili ya Kristo, kwa kuonesha mshikamano na huduma kwa maskini na wagonjwa, hasa wale wanaoteseka kutokana na ukimwi. Maaskofu wa Malawi wamemshirikisha Askofu mkuu Gallagher maisha na utume wa Kanisa nchini Malawi pamoja na changamoto wanazoendelea kukabiliana nazo.
Askofu mkuu Gallagher akiwa nchini Malawi amekutana na kuzungumza na Rais Peter Mutharika wa Malawi aliyekuwa ameambatana na viongozi wa Serikali pamoja na Kanisa. Kwa muda wa miaka arobaini na tisa, Malawi imekuwa na uhusiano wa kidiplomasia na Vatican. Katika kipindi cha miaka yote hii, Kanisa limekuwa mdau wa pekee kabisa katika ustawi na maendeleo ya wananchi wa Malawi: kiroho na kimwili. Kanisa limesaidia kudumisha mchakato wa utawala bora na demokrasia nchini Malawi.
Rais Mutharika amelishukuru kwa namna ya pekee kabisa Kanisa Katoliki kwa msaada mkubwa lililotoa kwa wananchi wa Malawi walipokumbwa na mafuriko pamoja na ukame wa kutisha. Askofu mkuu Gallagher ametumia nafasi hii kuwasilisha pia salam na matashi mema kutoka kwa Baba Mtakatifu Francisko kwa wananchi wa Malawi. Kabla ya kuondoka kutoka Malawi, Askofu mkuu Gallagher alipata nafasi ya kuadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwa Watawa wa ndani wa Mtakatifu Clara kwa kuwataka kuwa kweli ni mashuhuda amini wa maisha ya kuwekwa wakfu, kwa kufuata mfano wa karama na moyo wa Mtakatifu Clara wa Assisi. Askofu mkuu Paul Richard Gallagher tayari amerejea mjini Vatican na anaendelea “kudunda mzigo kama kawa”.
Magufuli atua Dodoma na jina la Waziri Mkuu!
RAIS John Magufuli amewasili mkoani Dodoma kwa mara ya kwanza tangu
achaguliwe kuongoza Tanzania akiwa ametumia njia ya barabara huku akiwa
na siri moyoni ya nani atakuwa Waziri Mkuu wake. Njia aliyotumia kufika
Dodoma imewashangaza wengi kutokana na ukweli kwamba marais
waliotangulia wamekuwa wakitumia usafiri wa ndege.
Baada ya kuwasili Ikulu Ndogo ya Rais iliyopo Wilaya ya Chamwino
mkoani Dodoma akitokea jijini Dar es Salaam, alipokewa na viongozi
mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kijiji cha Chamwino Ikulu, Joseph Seganje, wananchi wamefarijika kuona Rais huyo akiishi kwenye Ikulu hiyo kama alivyokuwa ameahidi. “Tayari tumempokea Rais wetu na wananchi wana furaha isiyo na kifani,” alisema Seganje.
Wakizungumza mapema wiki iliyopita, baadhi ya wakazi wa Chamwino Ikulu walisema itakuwa ni faraja kubwa kwa Rais kuishi kijijini hapo. Alice Chidong’oi alisema Dk Magufuli ni kiongozi anayeonesha nia ya dhati ya kuwatumikia watu wake kwa kujali zaidi wanyonge kama ilivyokuwa kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
“Tunaamini akiishi hapa atakuwa sehemu ya jamii ya Wana Chamwino na hilo litasaidia hata kuboreshwa kwa huduma za jamii ikiwemo maji,” alisema Chidong’oi. Alisema hiyo itakuwa fursa nzuri kwa wakazi wa eneo hilo kufanya biashara, kwani uwepo wake ndani ya wilaya hiyo utaongeza idadi ya wageni.
Mkazi mwingine, Stanley Richard, alisema vijana wa Chamwino wanapenda kazi na Dk Magufuli akiwa hapo itakuwa ni kazi tu. “Ni mtu ambaye anapenda kazi na sisi vijana tunapenda kufanya kazi, tutampa ushirikiano mkubwa katika kipindi chote atakachokuwa madarakani,” alisema.
Alisema alifurahi alipochaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwani alijua nchi imepata kiongozi ambaye yuko tayari kuwaletea wananchi wake mabadiliko. Tayari Serikali mkoani hapa imepiga marufuku kufanyika kwa mikutano ya hadhara na maandamano wakati wa vikao vya Bunge vikiendelea.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa, alisema amri hiyo ya kuzuia mikutano ya hadhara na maandamano ya vyama vya siasa bado inaendelea ili kuweka utulivu muda wote wa vikao vya Bunge.
Kwa mujibu wa ratiba ya vikao vya Bunge, kesho Alhamisi, Bunge litapokea na kuthibitisha kwa kupiga kura jina la Waziri Mkuu wa 11 wa Tanzania ambalo Dk Magufuli atakuwa ameliwasilisha kwa Spika Job Ndugai.
Kwa hiyo, Dk Magufuli atakuwa ametua mjini hapa akiwa na siri yake moyoni ya nani atakuwa Waziri Mkuu wake kwa miaka ya mwanzo ya utawala wake inayokoma mwaka 2020.
Mbali ya kutoa jina la Waziri Mkuu, Dk Magufuli anatarajia kulihutubia Bunge, Ijumaa alasiri baada ya kuwa amemwapisha Waziri Mkuu asubuhi. Hotuba yake itakuwa dira ya utawala wake kwa miaka mitano ijayo.

Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)