MWENYEKITI wa Simba SC, Ahaj Ismail Aden Rage amewasili Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dares Salaam usiku huu akitokea Sudan na kusema kwamba;
“Mimi bado Mwenyekiti wa Simba SC,”.
Rage aliwasili kwa ndege ya shirika la Kenya saa 1:40 usiku na kutokea mlango wa Watu maalum (VIP) ambako alilakiwa na wanachama zaidi ya 200, waliokuwa kwenye mabasi sita aina ya Coaster.
“Umati huu uliokuja hapa ni kielelezo tosha sana kwamba kiasi gani wanachama wa Simba wana imani na Mwenyekiti wao, sasa leo sitasema mengi, nitakuwa na Mkutano na Waandishi wa Habari kesho saa saba mchana makao makuu ya klabu(Msimbazi),”alisema Rage.
Alipoulizwa kuhusu kikao cha Kamati ya Utendaji kilichofanyika Jumatatu na kutangaza kumsimamisha, Rage alisema;
“Kwa mujibu wa Katiba ya Simba, Kamati ya Utendaji haina uwezo wa kumsimamisha Mwenyekiti, usinimalizie utamu njoo kesho mchana Msimbazi,”alisema.
Watu zaidi ya 200 walifika Uwanja wa ndege tangu saa 11 na ushei jioni ya leo kumsubiri Rage wakiimba nyimbo mbalimbali za kumbeza Kaimu Makamu Mwenyekiti, Joseph Itang’are ‘Kinesi’ na kumpamba Rage huku wakicheza ngoma.
Week Hot newz
-
Matumizi haramu ya dawa za kulevya ni janga kwa vijana we...
-
A Prayer for a Family O dear Jesus, I humbly implore You to grant Your special graces to our family. May ou...
-
Mpendwa msikilizaji wa Radio Vatican kipindi cha tafakari, ninakuleteeni tafakari ya Neno la Mungu Dominika ya tatu ya Majilio. Mas...
-
Viongozi wa Jumuiya ya Kimataifa pamoja na wananchi wa Afrika ya Kusini wameanza kutoa heshima zao za mwisho kwa Tata Madiba kwa sala kut...
-
Baba Mtakatifu Francisko wakati akirejea kutoka Armenia a...
-
Watawa wa Mama Theresa wa Calcutta waliouwawa huko Yemen ni mashuhuda wa upendo na wahanga wa utandawazi usiojali wala kuguswa na maha...
-
MOROGORO,TANZANIA. MSANII wa bongo fleva na mkali wa kurap kwa lugha 31 Batarokota, amesema tangu alipofariki mke wake mpendwa mwaka ...
-
Siku ya kumbukumbu ya kukumbuka ajali ya MV Bukoba tareehe 21/05/2016 katika jijini la mawe Mwanza (Rocky City) kutakuwa na burudani kabam...
-
Pichani juu msanii wa nyimbo za asili ya Kitanzania Batarokota akiwa katika Hoteli ya Misana aliyofikia jijini Mwanza.. MSANII wa ny...
-
KUNA changamoto nyingi ambazo wagonjwa wa saratani wanakutana nazo hasa kwa wanawake ambao wana saratani ya titi. Changamoto hizo zimes...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni