Jengeni
matumaini kwa Bwana, hata katika hali ngumu, Papa amehimiza wakati wa
Ibada ya Misa ya asubuhi Jumatatu hii katika Kanisa dogo la Mtakatifu
Marta mjini Vatican. Papa alisisitiza kwamba Wakristo wameitwa kufanya
maamuzi thabiti , kama yanavyo fundisha maisha ya mashahidi wa dini wa
kila wakati. Hata leo, alibainisha, kuna wake kwa waume wanao teseka kwa
sababu ya imani yao kwa Kristu. Na hivyo wao ni mfano kwetu wa kuiga,
kwa ajili ya kupata nguvu za kujikabidhi kwa Bwana bila kujibakiza.
Papa
aliendelea kufundisha kwamba, kumchagua Kristu, hakuna ukomo. Alieleza
hilo akingalisha katika somo la Kitabu cha Nabii Daniel, na Injili :
ambamo vijana Wayahudi watumwa katika mahakama ya Nebukadreza na mjane
aliyekwenda katika hekalu kumwabudu Bwana. Katika kesi zote, Papa
anaona, hapakuwa na ukomo wa hali. Mjane katika hali ya umaskini na
vijana katika hali ya utumwa, wote walijikabidhi kwa Bwana . Mjane
aliweka vyote alivyokuwa navyo katika hazina ya Hekalu, ambapo kwa
vijana walibaki aminifu kwa Bwana, hata katika hatari ya maisha.
Papa
aliendelea kusema, katika hali za wote, mjane na vijana – hawakujali
hatari za maisha zilizokuwa mbele yao. Walimchagua Bwana kwa moyo moja,
bila wasiwasi na bila upungufu. Kwao Bwana alikuwa ni juu ya yote juu.
Walitambua Bwana wao ni Mungu na kwake walijikabidhi wenyewe. Na hii
hawakufanya kwa sababu za kujitafutia sifa bandia , lakini walifanya
hivyo kwa kutambua kwamba, Bwana ndiye mkuu wa yote. Walijua kwamba
Bwana ni mwaminifu. Na ndivyo tunavyotakiwa nasi pia kufanya.
Ni
kumtegemea Bwana kwa uaminifu na imani kwamba daima yupo, kwa sababu
Bwana hawezi kubadilika kubadilika na kujikana mwenyewe. Imani hii
katika Bwana Papa Francisko aliongeza, huongoza katika maamuzi thabiti
ya kumchagua Yeye kuwa ndiye Bwana wa Yote, Yeye ni mwaminifu, katika
katika mambo yote madogo , makubwa na hata magumu.
Papa alieleza
na kuitazama historia ya kanisa kwamba, historia yake inaonyesha
wanaume, wanawake, wazee, vijana, waliofanya uchaguzi huu, kama tunavyo
sikia katika vyombo vya mawasiliano au kusoma katika magazeti juu ya
maisha ya mateso yanayokabili hata leo hii, Wakristo katika maeneo
mbalimbali duniani.
Wakristu hao wanaoishi nasi katika wakati
huu, ni mfano hai kwetu, wenye kutuhimiza pia sisi, kuiweka hazina
yetu ndani ya kanisa, ili kwamba, ambamo Bwana yumo ndani mwake.
Ushuhuda wa Wakristu hawa wateswa, unashuhudia neema ya ujasiri wa
kusonga mbele katika maisha ya Kikristo , katika hali ya kawaida ,
maisha magumu na hata katika mazingira hatarishi . Ni kuwa na Maamuzi
thabiti kwa Bwana.
Week Hot newz
-
Mpendwa msikilizaji wa Radio Vatican kipindi cha tafakari, ninakuleteeni tafakari ya Neno la Mungu Dominika ya tatu ya Majilio. Mas...
-
Tafakari masomo Dominika, ninafurahi tena kuwa nawe katika safari yetu ya Majilio tukijiandaa kwa ajili ya ujio wa Mwana wa Mungu. Ni wak...
-
Freeman Mbowe MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amesema maandamano na mikutano itakayofa...
-
NA OSCAR ASSENGA, TANGA-Tanzania.Gazeti Mtanzania. KATIBU wa Chama cha Watu Wenye Albino Mkoa wa Tanga (TAS), Mah...
-
Baba Mtakatifu Francisko Alhamis hii 14.11.2014 majira ya saa nne, kwa mara ya kwanza tangu kuwa Papa mwezi March mwaka huu, alifanya ziar...
-
Na Paskal Linda Ninakuletea ujumbe wa Neno la Mungu, Dominika ya 25 ya mwaka B wa Kanisa. Mama Kanisa anatufundisha wajibu wa Jumuiya ...
-
Klabu za Ligi ya Premia zilitumia zaidi ya £155m siku ya mwisho ya kuhama kwa wachezaji kipindi cha majira ya joto na kufikisha jumla y...
-
Reading 1, First Corinthians 15:35-37, 42-49 35 Someone may ask: How are dead people raised, and what sort of body do the...
-
Tafakari ya Neno la Mungu Jumapili ya 32 ya Mwaka B wa Kan...
-
Kardinali Pietro Parolin akisalimiana na Masista wa Upend...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni