Uchunguzi ulifanyika siku ya Ijumaa alasiri matokeo yake yamethibitisha kwamba ni kifo cha kawaida, kilichotokana na mapigo ya moyo kusimamisha. Mara kilipotokea kifo hiki, Ofisi ya utetezi wa Sheria, ilitaka kupata matokeo ya vipimo vya uchunguzi wa maabara uliofanywa na Tume hiyo.
Marehemu Józef Wesolowski alizaliwa Julai 15, 1948 Poland. Baada ya kukamilisha masomo yake ya kikuhani, alilitumikia Kanisa katika ngazi mbalimbali, na mwaka 2008 aliteuliwa na Papa Bendikto XVI, kuwa Mjumbe wa Kitume wa Papa katika Jamhuri ya Kisiwa cha Domenicani hadi Agosti 13, 2013, alipoachishwa kazi hiyo na Vatican kufuatia tuhuma za kudhulumu watoto kinjisia. Mwaka 2014, alivuliwa cheo cha Askofu Mkuu na kinga ya kidiplomasia ili Mamlaka katika Jamhuri ya Domenicani iweze kuchunguza madai ya unyanyasaji wa watoto yaliyotolewa dhidi yake. Hivyo vyombo vya kisheria vya Vatican vilikuwa bado vikifuatilia kesi yake.