Padre
Federico Lombardi, msemaji mkuu wa Vatican, wakati wa hija ya Baba
Mtakatifu Francisko nchini Cuba na Mexico, Ijumaa tarehe 12 Februari
2016, kwa niaba ya waandishi wa habari 76 walioko kwenye msafara wa Baba
Mtakatifu, amemtakia heri na mafanikio mema katika hija hii ya
kihistoria. Kundi kubwa la waandishi wa habari ni wale wanaotoka Mexico
ambao wamepewa upendeleo wa pekee ili kuhakikisha kwamba, ujumbe wa Baba
Mtakatifu unawafikia walengwa.
Baba Mtakatifu amewashukuru waandishi
wa habari kwa kazi kubwa wanayoifanya hasa kwa kuzingatia kuwa hija hii
ni ndefu na ya kihistoria, kwani anapenda kukutana na kuzungumza na
ndugu yake Patriaki Kirill wa Moscow na Russia nzima. Anapenda kwenda
kusali na kumsalimia Bikira Maria wa Guadalupe, ili kushangaa Fumbo la
upendo wa Mungu linalofumbatwa katika maisha ya wengi.
Baba Mtakatifu amechukua nafasi hii
kwa namna ya pekee kumshukuru Dr. Albeto Gasbarri ambaye kwa muda wa
miaka 47 amejisadaka kwa kazi na utume mbali mbali mjini Vatican. Kwa
muda wa miaka 37 ameratibu hija za kitume za viongozi wakuu wa Kanisa
sehemu mbali mbali za dunia. Tangu wakati huu, Monsinyo Mauricio Rueda
atakuwa mratibu mpya wa hija za kitume za viongozi wa Kanisa mjini
Vatican. Dr. Gasbarri anatarajiwa kung’atuka rasmi kutoka katika uongozi
hapo tarehe 29 Februari 2016.
Waandishi wa habari kutoka Mexico
wamemzawadia Baba Mtakatifu kofia ya kitamaduni kutoka Mexico kama
walivyofanya kwa Mtakatifu Yohane Paulo II miaka 37 iliyopita na kwa
Papa Mstaafu Benedikto XVI na sasa kwa Baba Mtakatifu Francisko. Baba
Mtakatifu amewashukuru na kuwatakia wote kazi na utume mwema wakati huu
wa hija yake ya kitume nchini Mexico.
Week Hot newz
-
Mpendwa msikilizaji wa Radio Vatican kipindi cha tafakari, ninakuleteeni tafakari ya Neno la Mungu Dominika ya tatu ya Majilio. Mas...
-
Tafakari masomo Dominika, ninafurahi tena kuwa nawe katika safari yetu ya Majilio tukijiandaa kwa ajili ya ujio wa Mwana wa Mungu. Ni wak...
-
Freeman Mbowe MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amesema maandamano na mikutano itakayofa...
-
NA OSCAR ASSENGA, TANGA-Tanzania.Gazeti Mtanzania. KATIBU wa Chama cha Watu Wenye Albino Mkoa wa Tanga (TAS), Mah...
-
Baba Mtakatifu Francisko Alhamis hii 14.11.2014 majira ya saa nne, kwa mara ya kwanza tangu kuwa Papa mwezi March mwaka huu, alifanya ziar...
-
Na Paskal Linda Ninakuletea ujumbe wa Neno la Mungu, Dominika ya 25 ya mwaka B wa Kanisa. Mama Kanisa anatufundisha wajibu wa Jumuiya ...
-
Klabu za Ligi ya Premia zilitumia zaidi ya £155m siku ya mwisho ya kuhama kwa wachezaji kipindi cha majira ya joto na kufikisha jumla y...
-
Reading 1, First Corinthians 15:35-37, 42-49 35 Someone may ask: How are dead people raised, and what sort of body do the...
-
Tafakari ya Neno la Mungu Jumapili ya 32 ya Mwaka B wa Kan...
-
Kardinali Pietro Parolin akisalimiana na Masista wa Upend...
