Baba
Mtakatifu Francisko mara baada ya maadhimisho ya Ibada ya Misa Takatifu
kwenye Uwanja wa
Huruma ya Mungu, Jimbo kuu la Cracovia Jumapili tarehe
31 Julai 2016 kama sehemu ya maadhimisho ya kufunga rasmi maadhimisho ya
Siku ya XXXI ya Vijana Duniani kwa mwaka 2016, kabla ya kusali Sala ya
Malaika wa Bwana na vijana kutoka sehemu mbali mbali za dunia,
aliwashukuru wadau mbali mbali waliojisadaka kwa ajili ya kuandaa na
hatimaye kufanikisha maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani.
Baraza la Maaskofu Katoliki Panama limepewa dhamana ya kuandaa Siku ya Vijana Duniani kwa mwaka 2019.Baba Mtakatifu anasema, maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani yaliyoanzishwa kunako mwaka 1985 na Mtakatifu Yohane Paulo II yanaendelea kushika kasi na baada ya maadhimisho ya Siku ya Vijana kwa ngazi ya Kijimbo katika kipindi cha miaka miwili, maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani yatafanyika kunako mwaka 2019 huko nchini Panama. Baba Mtakatifu pamoja na Maaskofu katoliki kutoka Panama wametoa baraka zao kwa ajili ya maandalizi ya maadhimisho haya.
Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni