Kocha Mkuu wa timu ya soka ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars), Kim Poulsen, amesema timu yake mesto wa yosso na wazoefu, iko tayari kuikabili Zambia (Chipolopolo) katika mechi yake ya kwanza ya kuwania ubingwa wa mashindano ya Kombe la Chalenji itakayofanyika kesho kwenye Uwanja wa Nyayo jijini hapa.
Akizungumza jana, Poulsen alisema wachezaji wake wote wako tayari na wamejiandaa kufanya vizuri katika mechi hiyo ya kwanza ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kusonga mbele.
Poulsen alisema mechi dhidi ya Chipolopolo inatarajiwa kuwa ngumu kwa sababu wachezaji wengi wa Zambia ni wauzoefu tofauti na kikosi chake ambacho mwaka huu ni mseto kutokana na kujumuisha yosso wengi aliowaita kwa mara ya kwanza, lakini anaamini watafanya vizuri.
"Tuko tayari, tumejiandaa kwa mashindano na tunaamini tutaanza vyema mechi yetu," alisema Kocha huyo raia wa Denmark.
Aliongeza kuwa, katika kundi lao ambalo linajumuisha timu ya Somalia na Burundi, hakuna mechi nyepesi kwa sababu kila moja imekuja kushindana na si kushiriki.
Naye mshambuliaji mahiri wa timu hiyo, Mrisho Ngasa, aliliambia blogu hili kuwa wamekuja Nairobi kushindana na watajituma ili kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania Bara.
Ngassa alisema anajua Watanzania wamewatuma kuiwakilisha vyema na hicho ndicho wamepanga kukitekeleza.
"Tunajua jukumu letu na tunamuomba Mungu tufanye vizuri, tuombeeni ili tufanye kile ambacho kocha ametuelekeza," alisema Ngasa.
Kilimanjaro Stars iliyoko Kundi B, ilitua jijini hapa juzi usiku na itacheza mechi yake ya pili Desemba Mosi dhidi ya Somalia huku ikimaliza hatua ya makundi kwa kuivaa Burundi hapo Desemba 4, mwaka huu.
Uganda ndiyo mabingwa watetezi wa mashindano hayo yanayofanyika kila mwaka kwa kushirikisha nchi wanachama wa Cecafa na timu alikwa.
Week Hot newz
-
Tunaendelea kama kawaida katika kipindi chetu, tafakari masomo Dominika, na leo tunatafakari masomo Dominika ya 33 ya mwaka C wa Kanisa...
-
MOROGORO,Tanzania NYOTA wa muziki wa Bongo fleva na Mziki wa Asili ya Kitanzania nchini Tanzania,Batarokota, amesema alianza kumpend...
-
Neno Kwaresima linatokana na neno la lugha ya kilatini Quadragesima ; maana yake, namba arobaini. Kwa hiyo, Kwaresima ni kipindi cha siku ...
-
Freeman Mbowe MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amesema maandamano na mikutano itakayofa...
-
Mpendwa msikilizaji wa Radio Vatican kipindi cha tafakari, ninakuleteeni tafakari ya Neno la Mungu Dominika ya tatu ya Majilio. Mas...
-
Utafiti mpya umeonesha watu wazima wengi duniani ni wanene kupita kiasi na kwamba hakuna matumaini ya kufikia lengo la kupunguza idadi...
-
Klabu za Ligi ya Premia zilitumia zaidi ya £155m siku ya mwisho ya kuhama kwa wachezaji kipindi cha majira ya joto na kufikisha jumla y...
-
Tafakari masomo Dominika, ninafurahi tena kuwa nawe katika safari yetu ya Majilio tukijiandaa kwa ajili ya ujio wa Mwana wa Mungu. Ni wak...
-
Papa Francisko akihutubia kabla ya sala ya Malaika wa Bwa...
.jpg)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni