Week Hot newz

Taharuki ya Mtakatifu Yosefu! Mtu wa haki!



“Kuzaliwa kwa Yesu Kristo kulikuwa hivi. Maria mama yake, alipokuwa mchumba wa Yosefu, kabla hawajakaa pamoja alionekana na mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Mumewe Yosefu akiwa mtu mwadilifu, hakupenda kumwaibisha hadharani. Basi akanuia kumwacha kwa siri.”
(Mt 1:18-19)

Moja ya kifungu cha maneno

Nyumba ya Papa ni mali ya Wakatoliki wote!

Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi, tarehe 16 Januari 2014 amekutana na kuzungumza na wafanyakazi wanaotekeleza dhamana na utume wao kwenye Makazi ya Papa mjini Vatican. Baba Mtakatifu amewashukuru kwa huduma na ukarimu wanaowashirikisha wageni mbali mbali wanaofika mjini Vatican kwa ajili ya kukutana na kuzungumza na Khalifa wa Mtakatifu Petro.

Baba Mtakatifu anasema kwamba, Nyumba ya Papa ni mali ya Waamini wote wa Kanisa Katoliki; mahali ambapo wanaonja tone la upendo na moyo wa ukarimu wa kifamilia pamoja na msaada wa kulinda na kudumisha imani ambayo ni zawadi kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Mmiliki mkuu wa Nyumba ya Kipapa ni Yesu mwenyewe na wengine wote ni wafuasi na wahudumu wa Injili.

Baba Mtakatifu anasema kutokana uelewa huu, kuna haja kwa wafanyakazi hao kukuza na kudumisha majadiliano ya kina kwa njia ya sala, ili kuimarisha urafiki na uhusiano wa ndani kabisa, tayari kutolea ushuhuda wa upendo na huruma ya Mungu kwa watu wake. Wafanyakazi hawa anasema Baba Mtakatifu wanapotekeleza utume wao, kazi inaweza kuwa ni fursa ya kuwashirikisha wengine furaha ya kuwa ni sehemu ya Fumbo la Mwili wa Kristo, yaani Kanisa.

Baba Mtakatifu anawaalika kuwa makini katika kuisikiliza sauti ya Mwenyezi Mungu inayowaita kila siku, kumtumikia kwa ukomavu na moyo wa ukarimu. Baba Mtakatifu amewatakia wafanyakazi hawa pamoja na familia zao, kheri na baraka kwa Mwaka Mpya 2014.

Ujumbe wa Papa Francisko kwa ajili ya Siku ya Wakimbizi na Wahamiaji Duniani kwa Mwaka 2014



Hali ya wakimbizi, wahamiaji na watu wasiokuwa na makazi maalum inahitaji kuangaliwa kwa usawa na ukamilifu zaidi, kwa njia ya ushirikiano wa kimataifa unaosimikwa katika mshikamano na huruma.

Hiki ndicho kiini cha ujumbe wa Siku ya 100 ya Wakimbizi na Wahamiaji inayoadhimishwa na Mama Kanisa kila mwaka ifikapo tarehe 19 Januari. Ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko kwa Mwaka 2014 unaongozwa na kauli mbiu “Wahamiaji na wakimbizi: kuelekea ulimwengu bora zaidi”.

Tafakari ya Neno la Mungu, Sherehe za Ubatizo wa Bwana



Mpendwa mwana wa Mungu, tuko tena pamoja katika ile habari ya furaha ndiyo kushirikishana mapendo ya Mungu kwa njia ya meza ya Neno lake.

Leo ndipo tunahitimisha kipindi cha Noeli kwa Sikukuu ya Ubatizo wa Bwana na tunaanza kipindi cha kawaida cha mwaka wa Kanisa. Kumbe leo pia ni Dominika ya kwanza ya kipindi cha kawaida cha mwaka wa Kanisa.

Katika somo la kwanza Nabii Isaya anatupeni habari juu ya mtumishi wa Mungu ambaye anapokea Roho wa Mungu na kazi

Vatican kujieleza kuhusu kashfa za ngono


Papa Francis
Maafisa katika Vatican makao makuu ya kanisa katoliki, wanatarajariwa kuhojiwa na maafisa wa Umoja wa Mataifa kuhusu dhuluma za kingono ambazo makasisi wa kanisa hilo waliwatendea maelfu ya watoto.
Maafisa hao walikataa ombi la awali ambapo Umoja wa Mataifa ulikuwa unataka taarifa za kina kuhusu dhuluma za kingono wakisema kuwa visa hivyo vinapaswa kushughulikiwa na idara ya mahakama katika mataifa ambako visa hivyo vilitokea

Idadi ya waamini na mahujaji waliokutana na Papa Francisko kwa Mwaka 2013 imeongezeka!

Takwimu zinaonesha kwamba, tangu Baba Mtakatifu Francisko alipochaguliwa kuliongoza Kanisa Katoliki hapo tarehe 13 Machi 2013, zaidi ya watu millioni sita wamekutana na kushiriki katika matukio mbali mbali yaliyoendeshwa na Baba Mtakatifu katika kipindi hiki hadi kufikia mwanzo mwa Januari 2014. Waamini, mahujaji na wageni walioshiriki katika katekesi zake zinazotolewa kila Jumatano walikuwa ni1, 548, 500.


Baba Mtakatifu alifanikiwa kukutana na kuzungumza na watu 87, 400 kwa faragha. Waamini na mahujaji wapatao 2, 282, 000 walishiriki katika Ibada mbali mbali zilizoongozwa na Baba Mtakatifu Francisko kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro na ndani ya Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican. Waamini zaidi ya 2, 706, 000 wameshiriki katika Sala ya Mchana na Baba Mtakatifu Francisko.

Takwimu hizi ni zile tu zilizokusanywa mjini Vatican na wala hazihusishi matuko kama: Maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani kwa Mwaka 2013yaliyofanyika nchini Brazil, kule Rio de Janeiro; wala safari zake za kichungaji ndani ya Italia, Lampedusa, Cagliari na Assisi hata katika baadhi ya Parokia zilizoko katika Jimbo kuu la Roma.

Kwa ujumla waamini na watu wenye mapenzi mema wapatao 6, 623, 000 wamekutana na kushiriki katika Ibada, Katekesi na Sala zilizokuwa zinaongozwa na Baba Mtakatifu Francisko. Itakumbukwa kwamba, idadi hii ya watu ni ile tu ambayo ni rasmi kwa wale watu walioomba tiketi kutoka Vatican. Kumekuwepo na umati mkubwa wa watu wanaomiminika kwenye matukio mbali mbali anayoshiriki Baba Mtakatifu Francisko, hii inatokana na mvuto alionao kwa watu!


Uraibu wa sigara wawavutia wengi


Athari za uvutaji sigara
Idadi ya wavutaji wa sigara duniani imeongezeka kwa karibu bilioni moja kwa mujibu wa takwimu mpya.
Watafiti walioandika katika jarida la Shirika la madaktari la Marekani wanasema hata hivyo kuwa idadi hiyo ni ndogo ikilinganishwa na ongezeko la watu kwa ujumla duniani na kuelezea haja ya juhudi zaidi kufanyika kuwazuia watu kuwa na tabia hiyo.
Idadi ya watu wanaovuta sigara kila siku duniani imepanda kwa kiwango cha watu takriban milioni 250 million kati ya mwaka 1980 na 2012, kwa mujibu wa ripoti .

Matumaini ya kupata chanjo dhidi ya Malaria kwa Mwaka 2014?



Kuna matumaini makubwa kwa Bara la Afrika katika kipindi cha Mwaka 2014 kuweza kupata kinga dhidi ya ugonjwa wa Malaria ambao umekuwa ni tishio kwa maisha na maendeleo ya wananchi wengi Barani Afrika. Majaribio ya chanjo yaliyofanywa kwa watoto 15, 500 yanaonesha kwamba, ugonjwa wa Malaria ulipingua kwa kipindi cha miezi 18 ya majaribio ya chanjo hii mpya. 


Kampuni ya GlaxosmithKline inatarajiwa

مجلة لا شيفيلتا كاتوليكا تنشر نص الحوار بين البابا فرنسيس واتحاد الرؤساء العامين





نشرت مجلة لا شيفيلتا كاتوليكا يوم أمس الجمعة نص الحوار الذي أقامه البابا فرنسيس مع اتحاد الرؤساء العامين في التاسع والعشرين من تشرين الثاني نوفمبر الماضي، وأعلن الحبر الأعظم في ختام هذا اللقاء أن العام 2015 سيكون عام الحياة المكرسة. استغرق هذا الحوار قرابة الثلاث ساعات وتمحور حول أبرز التحديات المطروحة اليوم أمام الحياة الرهبانية والكنيسة بصورة عامة. قال البابا إن الرهبان والراهبات يتبعون الرب بطريقة خاصة ونبوية، وينبغي بالتالي أن يكونوا رجالا ونساء قادرين على إيقاظ العالم. وحض على تفادي التطرف الأصولي والنظر إلى الواقع

Epifania ya Bwana: Dhahabu, Uvumba na Manemane! Kazi kwako!

Sikukuu ya Epifania inayoitwa pia Tokeo la Bwana ni sherehe kubwa sana kwa wakristu. Kwa bahati mbaya siku hii imegeuzwa kuwa kama ya maigizo ya watoto wanaopita kuimba nyumba hadi nyumba na kupata zawadi. Kwa hiyo badala ya kuwa Epifania tungeweza kuiita kwa kiingereza Happy-funny.
 

Sikukuu ya leo inayo mafundisho ya maisha yanayoweza kumtosha kila mtu. Ukifaulu kutanguzana kidhati na wasafriri wanaotajwa katika sikukuu ya leo watakufikisha kwenye uhondo wa maisha. Wasafiri hao wanaitwa majusi. Wametokea mashariki ya mbali wakielekea Betlehemu. Wasafiri hao hawatajwi idadi wala majina kama tunavyosadikishwa kuwa walikuwa watatu. Tunaambiwa tu Kulikuwa majusi kutoka mashariki ya mbali.

Jubilee ya Miaka 50 tangu Papa Paulo VI alipotembelea Yerusalem!


Ilikuwa ni tarehe 4 Januari 1964, takribani miaka 50 iliyopita, Baba Mtakatifu Paulo wa sita alikuwa anaanza hija ya kichungaji Nchi Takatifu na kuhitimisha safari hii ya kihistoria, jioni baada ya Maadhimisho ya Siku kuu ya Tokeo la Bwana, maarufu kama Epifania ya Bwana.

Baraka kwa Mwaka Mpya 2014



".. Bwana akubarikie, na kukulinda. Bwana akuangazie nuru za uso wake, na kukufadhili; Bwana akuinulie uso wake, na kukupa amani.." (Hesabu 6:22-27).


Mwaka mpya 2014 umeanza. Tushukuru Mungu kama tuliuanza katika mazingira ya kanisani kwa Ibada au hata kwa sala fupi na familia zetu. Kuna waliouanza, kwa bahati mbaya katika bar au fukwe za bahari. Hujachelewa bado, fanya hima katika juma hili ufanye ibada fupi na familia yako ili uanze na Mungu Baba.

Waisraeli walitamani sana kuanza kila kitu kwa baraka. Na ndio maana Mungu alimpa Musa "formula" hii ya baraka ili kuzima kiu yao. Tuone umuhimu wa baraka katika Maisha yetu. Tusikurukupe kwa cho chote Mwaka huu. Tuwe na unyenyekevu
wa kuomba baraka. Omba misa kanisani kwa lo lote unalonuia kufanya. Usifanye kwa akili na karama yako tu. Ujue wazi, Bwana asipoujenga mji waujengao wafanya kazi bure.

Tuombe :

Baba twaingojea kwa hamu sana kila Baraka utakayotukirimia kwa Mwaka huu mpya 2014. Baba uwe faraja na kimbilio la kila mmoja ndani ya familia zetu, kazi zetu, watoto wetu na rafiki zetu. Nyoosha mkono wako kwa kila familia zetu.

Imeandaliwa na
Padre Beno Michael Kikudo
Jimbo kuu la Dar es Salaam

Unene kupindukia katika nchi zinazostawi


Unene kupinduikia ni tatizo
Kunenepa kupindukia ni tatizo ambalo sasa linatishia zaidi maisha ya wengi katika mataifa yanayostawi duniani kuliko katika mataifa tajiri ambako mambo yana afadhali.
Sasa serikali nyingi zinaombwa kuongeza Ushuru vyakula hivyo vinavyosababisha watu kunenepa kupindukia kama njia ya kuokoa maisha ya watu kutokana na mshutoko wa moyo, kisukari na kiarusi.

THANK`S GOD 2014

Mkurugnzi wa Paskal Linda Blog akiwa na wafanyakazi wake kwa pamoja anawatakiwa heri ya mwaka mpya 2014.

Paskal Linda Blog itakuwa kila siku na vitu vipya mwaka 2014 mnakaribishwa sana kuangalia leo ni mwanzo tu wa mwaka.

Kwa mawasiliano zaidi piga simu +255 492623 au tembelea ofisini kwetu Morogoro- Msamvu (Neema Hotel).

Thank`s God


Njooni tumwabudu Mtoto Yesu! Mwaka 2014



Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii anawakumbusha kwamba, wanapotafakari sura ya Mtoto Yesu, wanatafakari pia uso wa Mwenyezi Mungu. Mwaliko wa kwenda kumwabudu! na kukaribisha Mwaka 2014.

Padri atahadharisha ndoa za jinsia moja, uzazi wa mpango


Geita
Imeelezwa kuwa kuna hatari ya familia kwa nchi zinazoendelea ikiwamo Tanzania kufikia ukomo wa ustawi na furaha na pamoja na kujenga taifa lisilo na uhai wa nguvu kazi na lenye maadili kutokana na ndoa za jinsia moja zinazoshika kasi katika mataifa ya Ulaya na Amerika.

Padri wa Kanisa Katoliki nchini amesema kuwapo kwa mazingira hayo matokeo yake ni watu kukoma kuzaa watoto na kukosa familia.

Familia ina dhamana kubwa kwa Kanisa na Jamii, ingawa inakabiliwa na changamoto nyingi!



Maadhimisho ya Siku kuu ya Familia Takatifu ya Yesu, Maria na Yosefu ni kielelezo cha upendo mkuu ambao Mwenyezi Mungu amemwonesha mwanadamu kwa kutaka Mwanaye wa Pekee, Yesu Kristo azaliwe katika familia ya binadamu, akiwa na Baba na Mama kama binadamu mwingine yoyote yule!

Liturujia ya Neno la Mungu inaonesha jinsi ambavyo Familia Takatifu ilivyoteseka hadi kukimbilia uhamishoni Misri ili kuokoa maisha ya Mtoto Yesu

Sherehe ya Familia Takatifu ya Yesu, Maria na Yosefu



Mpendwa mwana wa Mungu, leo tunasherehekea na kushangilia sherehe ya familia Takatifu. Masiha amezaliwa ndani ya familia hii. Ndani ya familia hii kuna majukumu ya kutekeleza ili Mwana wa Mungu akae mahali stahili na kwa namna hiyo atufundisha namna ya kutenda na kuishi kwenye familia zetu.

Somo la kwanza toka kitabu cha Hekima ya Yoshua bin Sira linaweka mbele yetu fahari na heri ya kuwaheshimu wazazi na kuwatunza katika uzee wao. Heri ambazo ziko wazi kadiri ya somo hili ni kuwa na uzao, na si uzao tu bali kufurahia uzao huo. Kuwa na maisha marefu na uzee wa kusifika. Kwa kuwatunza wazazi na kuwapa heshima stahili mmoja afanya malipizi ya dhambi zake. Kwa hakika somo hili lasisitiza na kuweka mkazo juu ya amri ya nne ya Mungu. Waheshimu baba na mama upate miaka mingi na heri duniani

Viongozi wa serikali waombewa msamaha kwa Mungu

28th December 2013

Waumini wa huduma ya Mtakatifu Prince Mission yenye Makao Makuu yake Sinza jijini Dar es Salaam, wameomba msamaha wa Mungu kwa baadhi ya viongozi  wa umma kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni kuusaliti umma wanaoungoza.

Hatua hiyo inatokana na matumizi ya misahafu wanapokula viapo vya kuutumikia umma, kisha kutotimiza azma hiyo badala yake kujinufaisha binafsi na ‘kuwaangamiza’ raia wanaowachagua.