
Jeneza lenye mwili wa Hayati Nelson Mandela
Waombolezaji nchini Afrika
Kusini wanaingia siku ya pili katika zoezi la kutoa heshima za mwisho
kwenye mwili wa Rais wa kwanza mweusi nchini Afrika Kusini Hayati Nelson
Mandela.
Maelfu ya watu wamejipanga kwenye mistari
wakisubiri kutoa heshima zao za mwisho kwenye mwili huo uliolazwa katika
ikulu kwenye jengo la Muungano mjini Pretoria.