Week Hot newz

Mwenyeheri Yohane Paulo II kutangazwa kuwa Msimamizi wa Siku za Vijana Duniani



Baba Mtakatifu Francisko anawaalika vijana kujiandaa kikamilifu kwa ajili ya Maadhimisho ya Siku ya 29 ya Vijana Duniani kwa Mwaka 2014 itakayoadhimishwa katika ngazi ya Kijimbo, Jumapili ya Matawi, ambayo kwa Mwaka huu inaadhimishwa hapo tarehe 13 Aprili.

Hii ni siku ambayo Maaskofu watazungukwa na umati wa vijana kutoka katika majimbo yao ili kufanya tafakari ya kina kuhusu kauli mbiu ya inayoongoza Maadhimisho haya: "Heri walio maskini wa roho maana ufalme wa mbinguni ni wao". Hii ni sehemu ya muhtasari wa mafundisho makuu ya Yesu yanayopatikana katika Heri za Mlimani. 



Baraza la Kipapa la Walei linasema, huu ni ujumbe ambao unatolewa kwa mara ya kwanza kwa vijana na Baba Mtakatifu Francisko tangu alipochaguliwa kuwa Khalifa wa Mtakatifu Petro. Ni mwendelezo wa changamoto ya majiundo endelevu iliyoanzishwa na Mwenyeheri Yohane Paulo II na kuendelezwa kwa ari kubwa na Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto wa kumi na sita.

Papa Francisko bado anakumbuka ule umati wa vijana kutoka sehemu mbali mbali za dunia uliomzunguka wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani kwa Mwaka 2013 iliyofanyika mjini Rio de Janeiro. Baba Mtakatifu anaendeleza yale majadiliano ya kina kati yake na vijana yaliyoibuliwa wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani.

Kumbe, ujumbe wa Baba Mtakatifu kwa Maadhimisho ya Siku ya Vijana Kijimbo kwa Mwaka huu, ni sehemu ya maandalizi ya hija ya maisha ya kiroho, itakayofanyika katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia sasa, kabla ya vijana hawajajimwaga kuelekea Jimbo kuu la Cracovia, Poland, kwa Maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani kwa Mwaka 2016.

Wachunguzi wa mambo wanasema, vijana watafunika Poland, ikizingatiwa kwamba, hizi zitakuwa ni mwendelezo wa utenzi wa sifa na shukrani kwa Mwenyezi Mungu baada ya Mwenyeheri Yohane Paulo II kutangazwa kuwa Mtakatifu. Tema zilizochaguliwa na Baba Mtakatifu katika kipindi cha miaka mitatu kutoka katika Heri za Mlimani zinazonesha jinsi ambavyo Baba Mtakatifu Francisko anavyothamini sehemu hii ya Injili kuwa ni kiini cha maisha ya Wakristo, mwaliko wa kuyamwilisha katika vipaumbele vyao vya maisha ya kila siku!

Baba Mtakatifu katika ujumbe kwa Siku ya Vijana Duniani anapenda kuwakumbusha vijana wa kizazi kipya kwamba, hii ni njia ambayo Yesu mwenyewe amewaonesha wafuasi wake, mwaliko wa kumfuasa katika maisha yao yote bila ya kujibakiza hata kidogo. Kumwilisha Heri za Mlimani kwa vijana wa kizazi kipya anasema Baba Mtakatifu ni kazi kweli kweli! 



Huu nimwaliko wa kumfuasa Kristo na kushikamana naye kwa dhati, tayari kutolea ushuhuda wa mabadiliko yanayobubujika kutoka katika undani wa maisha ya mwamini. Baba Mtakatifu anawachangamotisha vijana kutokubali kupata furaha ya mpito kwa mambo ya juu juu tu, bali wahakikishe kwamba, wanajitaabisha kutafuta furaha ya kweli inayobubujika kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Katika ujumbe wake, Baba Mtakatifu anafafanua kwa kina na mapana maana ya umaskini wa roho kadiri ya mafundisho ya Yesu, ambaye aliuchagua mwenyewe na hatimaye kuutolea ushuhuda katika maisha na utume wake hapa duniani, mwaliko kwa vijana kuiga mfano wa maisha ya Mtakatifu Francisko, aliyekuwa tajiri wa kutupwa, lakini akaacha yote na kuukumbatia ufukara wa Kiinjili. Hii ndiyo changamoto kubwa iliyoko mbele ya vijana wa kizazi kipya na wala si maji kwa glasi!

Baba Mtakatifu Francisko anawaalika vijana kutubu na kumwongokea Yesu Kristo, huku wakijitahidi kuishi maisha yanayosimikwa katika kiasi, wakitafuta mambo msingi katika maisha yao pamoja na kujenga mshikamano wa upendo na maskini pamoja na wote wanaosukumizwa pembezoni mwa Jamii. Maskini ni sehemu ya Fumbo la Mwili wa Kristo linaloendelea kuteseka, mwaliko kwa kila mwamini kuhakikisha kwamba, anaguswa na umaskini, taabu na mahangaiko ya jirani zake; kwa njia hii vijana wanaweza kuwa kweli ni walimu wa maisha, kwa kuwamegea wengine utajiri wa maisha ya kiroho na kiutu unaobubujika kutoka katika undani wa maisha yao.

Baba Mtakatifu Francisko anasema, kuna uhusiano mkubwa kati ya tema iliyoongoza Maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani kwa Mwaka 2013 huko Rio de Janeiro "Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi..." na kauli mbiu ya mwaka huu yaani, "Heri walio maskini wa roho maana ufalme wa mbinguni ni wao". Ufukara wa Kiinjili ni muhimu sana katika ujenzi wa ufalme wa Mungu sehemu mbali mbali za dunia. Ni ufukara unaojionesha katika hali ya kawaida pasi na makuu, kiasi cha kuweza kuwa ni chachu ya Uinjilishaji Mpya.

Baba Mtakatifu anawakumbusha vijana wa kizazi kipya kwamba, hapo tarehe 22 Aprili 2014, Kanisa litafanya kumbu kumbu ya Miaka 30 tangu Msalaba wa Jubilee ya Mwaka wa Ukombozi ulipoanza kutembezwa sehemu mbali mbali za dunia. Hizi zilikuwa ni juhudi za Mwenyeheri Yohane Paulo wa Pili kwa ajili ya Kanisa, tangu wakati ule, Msalaba umekuwa ni sehemu ya hija ya maisha ya vijana wa kizazi kipya.

Kwa hakika, baada ya Mwenyeheri Yohane Paulo II kutangazwa kuwa Mtakatifu, Kanisa litaendelea kumshukuru Mungu kwa kumtangaza rasmi kuwa ni Msimamizi wa Maadhimisho ya Siku za Vijana Duniani. Mwenyeheri Yohane Paulo II alikuwa ni muasisi na mhamasishaji mkuu wa Siku za Vijana Duniani, hadi leo hii, tukio hili linaendelea kuwa na mvuto na mashiko makubwa katika maisha na utume wa Mama Kanisa miongoni mwa vijana, kwa kutambua kwamba, vijana ni jeuri na matumaini ya Kanisa kwa sasa na kwa siku za usoni!

Daily Reading for Friday, February 7th, 2014



Reading 1, Sirach 47:2-11

2 As the fat is set apart from the communion sacrifice, so was David chosen out of the Israelites.
3 He played with lions as though with kids, and with bears as though with lambs.
4 While still a boy, did he not slay the giant and take away the people's shame, by hurling a stone from his sling and cutting short the boasting of Goliath?
5 For he called on the Lord Most High, who gave strength to his right arm to put a mighty warrior to death and assert the strength of his own people.
6 Hence they gave him credit for ten thousand, and praised him while they blessed the Lord, by offering him a crown of glory.
7 For he destroyed the enemies on every front, he annihilated his foes, the Philistines, and crushed their strength for ever.
8 In all his activities he gave thanks to the Holy One Most High in words of glory; he put all his heart into his songs out of love for his Creator.
9 He placed singers before the altar, melodiously to sing;
10 he gave the feasts their splendour, the festivals their solemn pomp, causing the Lord's holy name to be praised and the sanctuary to resound from dawn.
11 The Lord took away his sins, making his strength ever greater; he gave him a royal covenant, and a glorious throne in Israel.

Responsorial Psalm, Psalms 18:31, 47, 50, 51

31 For who is God but Yahweh, who is a rock but our God?
47 the God who gives me vengeance, and subjects whole peoples to me,
50 He saves his king time after time, displays his faithful love for his anointed, for David and his heirs for ever.

Gospel, Mark 6:14-29

14 King Herod had heard about him, since by now his name was well known. Some were saying, 'John the Baptist has risen from the dead, and that is why miraculous powers are at work in him.'
15 Others said, 'He is Elijah,' others again, 'He is a prophet, like the prophets we used to have.'
16 But when Herod heard this he said, 'It is John whose head I cut off; he has risen from the dead.'
17 Now it was this same Herod who had sent to have John arrested, and had had him chained up in prison because of Herodias, his brother Philip's wife whom he had married.
18 For John had told Herod, 'It is against the law for you to have your brother's wife.'
19 As for Herodias, she was furious with him and wanted to kill him, but she was not able to do so,
20 because Herod was in awe of John, knowing him to be a good and upright man, and gave him his protection. When he had heard him speak he was greatly perplexed, and yet he liked to listen to him.
21 An opportunity came on Herod's birthday when he gave a banquet for the nobles of his court, for his army officers and for the leading figures in Galilee.
22 When the daughter of this same Herodias came in and danced, she delighted Herod and his guests; so the king said to the girl, 'Ask me anything you like and I will give it you.'
23 And he swore her an oath, 'I will give you anything you ask, even half my kingdom.'
24 She went out and said to her mother, 'What shall I ask for?' She replied, 'The head of John the Baptist.'
25 The girl at once rushed back to the king and made her request, 'I want you to give me John the Baptist's head, immediately, on a dish.'
26 The king was deeply distressed but, thinking of the oaths he had sworn and of his guests, he was reluctant to break his word to her.
27 At once the king sent one of the bodyguard with orders to bring John's head.
28 The man went off and beheaded him in the prison; then he brought the head on a dish and gave it to the girl, and the girl gave it to her mother.
29 When John's disciples heard about this, they came and took his body and laid it in a tomb.

St. Moses


St. Moses




Died: 372

Arab hermit and bishop who is called “the Apostle of the Saracens.” He lived in the desert regions of Syria and Egypt, caring for the local nomadic tribes. When the Romans imposed peace upon the Saracens, Queen Mavia, the Saracen ruler, demanded that Moses be consecrated a bishop. He accepted against his will and maintained the peace between the Saracens and Rome. The Saracens were a nomadic people of the Syro-Egyptian desert so designated by the Romans.

Kila mtu anapaswa kupata huduma makini ya afya!

Askofu mkuu Zygmunt Zimowski, Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya wafanyakazi katika sekta ya afya katika ujumbe wake kwa Maadhimisho ya Siku ya Dawa Kitaifa nchini Italia na katika baadhi ya Nchi za Ulaya inayoadhimishwa hapo tarehe 8 Februari, 2014 anasema, kuna haja kwa Serikali pamoja na wadau mbali mbali kuhakikisha kwamba, watu wanapata huduma sawa ya afya, mahali popote pale walipo, lakini maskini, watoto na wote wanaosukumizwa pembezoni mwa Jamii wapewe kipaumbele cha kwanza.

Askofu mkuu Zimowski anasema, katika nchi 90 duniani,

SAUTI ZA BUSARA: Ni zaidi ya Tamasha la burudani

TAMASHA la Sauti za Busara ni miongoni mwa machache ambayo yamejenga historia kutokana na kuutangaza na kuuendeleza muziki wa Tanzania nje ya mipaka yake, ambako mwaka huu litafanyika kuanzia Februari 13 hadi 16. Mbali na burudani, Tamasha la Busara ambalo ni la 11 mwaka huu tangu kuanzishwa, limekuwa kiunganishi kizuri kwa wasanii wa hapa nyumbani na wale wa kimataifa, jambo linalotoa nafasi ya kubadilishana ujuzi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Sauti za Busara Promotions, Simai Said Mohamed, anasema lengo la kuandaa tamasha hilo ni kuwaleta watu pamoja na kuonyesha utajiri wa muziki wa kisasa, ambao umebuniwa katika nchi za Afrika Mashariki, nchi nyingine kutoka barani Afrika na kwingineko duniani.

Mohamed anasema, tamasha hilo linalojulikana kama ‘Tamasha Rafiki Katika Sayari’ ni la kimataifa linalosherehekea muziki wa Kiafrika kila mwaka na kwamba vikundi 32 vitafanya maonyesho jukwaani ndani ya Ngome Kongwe visiwani Zanzibar.
Anasema vikundi hivyo vimechaguliwa kutokana na maombi zaidi ya 560 na vinawakilisha nchi 19, zikiwemo za Afrika Mashariki, Afrika Kusini na Magharibi, maeneo ya Mto Nile, pia kutoka Puerto Rico na inatarajiwa zaidi ya wasanii 200 watafika Zanzibar kufanya maonyesho ya muziki.
Mwenyekiti huyo anawataja miongoni mwa wasanii maarufu kutoka Tanzania watakaoshiriki Tamasha la Sauti za Busara 2014 kuwa ni pamoja na Jhiko Manyika ‘Jhikoman’, mwanamuziki anayejulikana kwa muziki wake wa reggae, ambaye atazindua ziara yake ya kuitembelea dunia jukwaani wakati wa onyesho lake.

Wasanii wengine kutoka hapa nchini ni Ashimba,Batarokota, Swahili Vibes, Hoko Roro, Seven Survivor, Abantu Mandingo, Segere Original na Kazimoto, anayemshirikisha Jackie Kazimoto kutoka ‘The Internationally-Acclaimed’, Jagwa Music.
Anasema tamasha hilo pia litamkaribisha mwanamuziki mkongwe aliyefanikiwa kimuziki kutoka nchini Ghana, Ebo Taylor, pia atakuwepo Sona Jobarteh, mwanahistoria kutoka Gambia na ‘Jupiter and Okwess International’ mwanamuziki mwenye mafanikio kutoka Jamhuri ya Watu wa Congo, ambaye anapasua anga katika fani ya muziki Afrika na kwingineko duniani.
Mwenyekiti huyo anawataja wasanii watakaopamba tamasha hilo na nchi zao kwenye mabano kuwa ni Jhikoman, Ashimba, Hoko Roro, Seven Survivor, Abantu Mandingo, Segere Original, Kazimoto (Tanzania),  Swahili Vibes, Baladna Taarab, Tausi Women’s Taarab, Rajab Suleiman & Kithara ft. Derya Takkali (Zanzibar),  Joel Sebunjo ft. Lenna Kuurmaa (Uganda), Moyize (Rwanda),  Ricky na Marafiki (Kenya).

Wengine ni Ebo Taylor (Ghana na Ujeruman),   Jupiter & Okwess International (DRC),  Joe Driscoll and Sekou Kouyate (USA na Guinea),  The Nile Project (Nile Basin), Noumoucounda Cissoko (Senegal), Oy (Ghana na Uswisi), Addis Acoustic Project (Ethiopia), Sona Jobarteh (Gambia na Uingereza), Tarabband (Misri na Sweden), Majestad Negra (Puerto Rico), HAJAmadagascar and The Groovy People ft. Werner Puntigam (Madagascar, Ufaransa na Australia), Tritonik (Mauritius), Kara Sylla Ka (Senegal na Uswisi), Dizu Plaatjies & The Ibuyambo Ensemble (Afrika Kusini), Street Rat and Body Mind & Soul (Malawi),  Moyize (Rwanda), Ricky na Marafiki (Kenya), Waldemar Bastos (Angola na Portugal) na wengineo wengi kutoka nchi mbalimbali.

Mohamed anaongeza kuwa kwa upande mwingine, mwaka huu burudani ya muziki itajumuisha ‘paredi’ siku ya ufunguzi, pia kutakuwa na ‘Movers & Shakers’ (kongamano la wataalamu), na uonyeshaji wa filamu ndefu za muziki za Kiafrika ambazo zimeshinda tuzo mbalimbali.
“Kwa kushirikiana na wafadhili wa miradi HIVOS, pia tutautambulisha mradi mpya unaojulikana kama ‘Santuri Safari’, mradi ambao utaangalia zaidi jukumu la DJ kwa wakati huu na kuangalia jinsi ya utamaduni wa DJ katika kukuza muziki wa Afrika Mashariki,” anasema.
Mohamed anasema DJ waalikwa, wazalishaji wa muziki, wataalamu wa sauti, waandaaji wa matamasha na wataalamu wa sanaa kutoka ukanda wa Afrika, watajumuika pamoja Zanzibar na kufanya kazi pamoja na kupata mafunzo.

“Tunaona hii ni fursa adimu kushirikiana na kuangalia kuibuka kwa vitu vya kisasa vinavyotokea katika muziki wa elektroniki na utamaduni wa MaDj, na kuangalia jinsi ya kuukuza muziki kikanda na katika anga la kimataifa kwa wakati huu na kwa miaka ijayo,” anasema.
Anasema, kutakuwa na muziki kipindi cha jioni wakati wa jua kuzama maeneo ya mjini na Ijumaa na Jumamosi kutakuwa na burudani ya muziki Ngome Kongwe baada ya kumalizika kwa maonyesho ya moja kwa moja jukwaani.
Anasema, pia tamasha hilo linakuza mambo mbalimbali kupitia ‘Buasara Xtra’ kwa kujumuisha matukio ya maonesho, ambako kwa pamoja hutoa fursa kwa wasanii wazawa kuonyesha kazi zao na kuwafanya wageni watembelee maeneo mengine ya Kisiwa cha Zanzibar.
Anasema zaidi ya Watanzania 150 huajiriwa kila mwaka kama wafanyakazi wa tamasha na pia kwa upande wa kukuza na kulinda muziki na utamaduni wa Zanzibar, Sauti za Busara inatumia nafasi iliyonayo katika kuuthamini muziki wa Bara zima la Afrika, kukuza amani, kujenga jamii ya pamoja Afrika Mashariki na kukuza utalii wa kitamaduni.
“Kwa kila siku kiingilio katika tamasha ni bure kabla ya saa 11 jioni kwa Watanzania wote, na baada ya hapo kiingilio ni sh 5,000 pia ukitaka maelezo zaidi, unaweza kutembelea www.busaramusic.org na kwamba
Busara Promotions ni taasisi inayowezeshwa kwa mwaka mzima na Ubalozi wa Norway,” anasema.
Mohamed, anatoa shukurani kwa Bodi ya wadhamini na wafadhili kama Hivos, Goethe-Institut, the Embassy of the United States of America, Swiss Agency for Development and Cooperation, African Music Festivals Network, Zanzibar Unique, Memories of Zanzibar, Ultimate Security, Ubalozi wa Ufaransa, Southern Sun Hotel, Azam Marine, Ubalozi wa Ujerumani na SMOLE II.