Week Hot newz

Zawadi ya Noeli kwa Mwaka 2015: Huruma, amani, furaha na mapendo!


Bikira Maria ni sanduku la: Agano jipya, huruma, msamaha na mapendo ya Mungu!

NA PASKAL LINDA



Kadiri ya mila za Waafrika mgeni akutembeleapo hubeba zawadi. Kwa kawaida zawadi hiyo inakuwa chakula kama vile unga katika sanduku liitwalo jamanda, linafungwa nguo nzuri na kubebwa kichwani na mwanamke, kisha mgongoni hubeba kuku kama mtoto mchanga. Afikapo ugenini, mama mwenye nyumba huzipokea zawadi kwa furaha na kumkaribisha mgeni nyumbani. Noel ni kipindi cha kutembeleana, kupeana zawadi na kufurahiana.
Mama Maria baada ya kuambiwa na Malaika Gabrieli kuwa ana baraka, (mja mzito), akaondoka mara moja kwenda kumtembelea ndugu yake Elizabeti aliyekuwa na baraka ya Yohane mbatizaji. Ndivyo tunavyosali katika fumbo la pili la rozari ya furaha: “Uliyekuchukua ulipokwenda kumtazama Elizabeth.” Aliwasili huko, Maria akamwamkia Elizabeth na kuendelea na mazungumzo. Lakini mazungumzo ya akina mama hawa ni tofauti. Hawa wanaongea lugha ya utaalamu wa hali ya juu wakinukuu Agano la kale kama vile unasikiliza mhadhala wa Wataalamu wa Biblia. Kwa hiyo, ili kuupata ujumbe wa mazungumzo ya akina mama wa leo, yakubidi ukae mkao wa nidhamu na kuwasikiliza kwa nidhamu, vinginevyo utatoka kapa.

Huduma kwa waathirika wa dawa za kulevya ijikite katika kukinga na kuponya!


Matumizi haramu ya dawa za kulevya ni janga kwa vijana wengi wa kizazi kipya! Jumuiya ijitahidi kuwa na mikakati ya kuzuia na kuwaganga waliotumbukia huko! -

Kardinali Pietro Parolin, kama sehemu ya maadhimisho ya Mwaka Mtakatifu wa Jubilei ya huruma ya Mungu, Jumanne, tarehe 22 Desemba 2015 ameadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwa waathirika wa dawa za kulevya pamoja na familia; kundi linalohudumiwa kwenye kituo cha mshikamano cha Don Mario Picchi, kilichoko mjini Roma. Katika mahubiri yake, Kardinali Parolin amekazia umuhimu wa kuzuia na kuwapatia tiba wale walioathirika kutokana na matumizi haramu ya dawa za kulevya; watu ambao idadi yao inazidi kuongezeka maradufu kutokana na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii.