Aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba,Marehemu Dk. Sengondo Mvungi
Aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba,
Dk. Sengondo Mvungi, alizikwa jana katika Kijiji cha Chanjale Juu,
Wilaya ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro huku Askofu Rogath Kimario wa
Kanisa Katoliki Jimbo la Same, akiwaeleza waombolezaji kwamba marehemu
amekufa kwa kifo cha fedheha kilichotokana na kile alichokiita mauaji ya
kimtandao.