Week Hot newz

Mbwana Samatta Mchezaji Bora Wa Mwaka

samattaMshambuliaji wa Taifa Stars, Mbwana Samatta amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka na mashabiki wa klabu yake ya TP Mazembe katika ya mchezaji bora wa mwaka wa klabu hiyo iliyopewa jina la “Corbeau d’Or”. Samatta ambaye amepewa jina la utani la “Samagoal” na mashabiki wa TP Mazembe aliwabwaga wachezaji wengine watano waliokuwa wakishindana.
Baada ya zoezi zima la upigaji kura matokeo yalikuwa kama ifuatavyo:
1. Mbwana Samatta – Kura 248
2. Asante Solomon – Kura 219
3. Robert Kidiaba – Kura 200
4. Nathan Sinkala – Kura 97
5. Rainford Kadaba – Kura 67

BATAROKOTA AJA NA SONGI `IROMBO LISE`

Msanii wa ngw`anza  fleva toka jijini Mwanza Batarokota mkali wa kurap kwa lugha ya kishahili na kisukuma, msanii huyu ndani ya wiki hii ameibuka na audio ya songi mpya 'irombo lise`, nyimbo hii imerekodiwa ndani ya studio ya Sun light Record iliyo mji kasoro bahari mjini Morogoro maeneo ya Kihonda (Mazimbu Road) . Songi hiyo 'irombo lise' imerekodiwa na kutengenezwa midundo na watayarishaji Batarokota akishirikiana na King Malo. Akizungumnza kwa njia ya simu toka mjini Morogoro msanii Batarokota alisema `nashukuru Mungu mwaka umeanza na nimemaliza kurekodi nyimbo yangu ya kisukuma iitwayo `irombo lise` yaaani Dada yetu na sasa niko katika maandalizi ya video ` alesema msanii Batarokota .Pia baada ya kumaliza na audio Batarokota na sasa video ya song hili 'irombo lise' na kufanyiwa shootingi chini ya usimamizi wa kampuni ya Batarokota iitwayo Paskal Linda Blog kwa udhamini wa Zachalia Linda Entertinment.