Week Hot newz

Tafakari ya neno la Mungu Dominika ya 26 ya Mwaka B,

Na Paskal Linda

Mpendwa mwana wa Mungu,  katika kipindi tafakari Neno la Bwana, jioni hii tunatafakari Dominika ya 26 ya mwaka B wa Kanisa. Neno la Mungu latutaka kutambua kuwa Roho wa Mungu ni zawadi kwa ajili ya wote ilimradi mmoja anaitumia zawadi hiyo kadri ya mpango wa Mungu.


 
Katika somo la kwanza kutoka kitabu cha Hesabu, tunaona jinsi Mungu alivyowashukia wale ndugu 70 na wakatabiri kama ambavyo Musa alikuwa akishukiwa na Mungu. Si hao tu bali kulikuwa na watu wengine wawili ambao wao katika harakati za kwenda hemani ambapo daima Musa alikuwa akikutana na Mungu wao walibaki kambini pia nao wakashukiwa na roho wa Mungu na wakaanza kutabiri. Tendo hili liliwaudhi watu wengine ambao waliona daima lazima Mungu agawe roho wake pale kwenye hema tu na si kwingine! Mpendwa jambo la wivu ni la zamani sana kama ambavyo tunaona kwa tukio hili. Je leo jambo hili lipo? Kabisa na ni kweli kwamba katika zama zetu kuna baadhi yetu ambao huona kama Roho Mtakatifu ni kwa ajili yao tu! Yapo makundi katika Kanisa katoliki ambayo hujisikia kabisa kwamba yanaweza kumkumbatia Roho Mtakatifu na kumteka kwa ajili yao tu! Labda pia kwenye makanisa mengine! Mpendwa hili ni kosa la kiteolojia na pengine linapaswa kukemewa mara moja na viongozi wetu wa Kanisa kwa sababu limekuwa ni jambo linalohangaisha na kuleta usumbufu kwa jumuiya ya Kanisa.
Somo la pili, linatualika kutazama vema juu ya suala la kuwanyonya maskini na hasa katika suala zima la malipo baada ya kazi. Mt. Yakobo anasema madhulumu kwa walio maskini huleta kilio ambacho humfikia Mungu mara moja kama kilio cha damu ya Abeli kilivyomfikia Mungu haraka. Anawakumbusha matajiri kutumia utajiri wao kwa haki na zaidi kuimarisha maisha ya ustawi uliojaa uwiano sahihi. Mpendwa mwana wa Mungu, kama tunataka kweli kushika vema Injili ya Kristu yatupasa kufikiria vema namna ya kushikama na utajiri ili kisiwe kikwazo bali chombo kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya watu.
Katika somo la Injili tunapata msaada wa kuweza kuelewa somo la kwanza ambapo tulisikia juu ya wivu kwa kuwa watu wawili ambao hawakuwa wameandamana na wale 70 pamoja na Musa nao walipata uwezo wa kutabiri. Ndiyo kusema mtu mmoja anatoa pepo kwa jina la Bwana lakini hayuko katika kundi la Mitume, na matokeo yake Yohane anamwambia Bwana kwamba walipomwona mtu huyu akitenda walimkataza asifanye shughuli hiyo ya kutoa pepo! Bwana anawajibu Mitume akisema hakuna ambaye atakuwa kinyume nami na kisha ataweza kutoa pepo kwa jina langu, kwa jinsi hiyo basi huyo yu upande wetu. Jambo la msingi ni kwamba mkuu wa shughuli nzima ya kitume ni Yesu Kristu na si Mitume kumbe yeye hugawa apendavyo karama zake. Roho Mtakatifu ni zawadi kwa wote hata wale ambao wako nje ya Kanisa linaloonekana, na hivi wanaotumia nguvu ya Kristu wanalisaidia Kanisa kusonga mbele katika shughuli ya wokovu.
Mpendwa sehemu ya pili ya Injili inazungumza na kutuasa juu ya ukarimu ambao Mt. Yakobo daima anasisitiza. Anawatayarishia heri wale wote watakaowakirimu Mitume wakiwa katika utume wa utangazaji wa Injili ya Bwana. Mpendwa , kazi ya kitume inaendelea na hivi wanaheri wale wote ambao wanaifanya kazi hiyo njema isonge mbele. Namna za kuifanya kazi ya kitume iende mbele ziko nyingi na mojawapo ikiwa kwa njia ya sala, kwa michango ya fedha na vitu, kuwahifadhi watumishi wa Kanisa mara kunapokuwa na hitaji kama vile nyumba, mfano parokia mpya inapofunguliwa.
Mpendwa, bado kuna hatua nyingine ya kutekeleza utume wa Kristu, nayo ni kuhakikisha huwi kikwazo au chanzo cha makwazo kwa jumuiya ya waamini, maana Bwana anasema atakayemkwaza mmojawapo wa wadogo hawa ni afadhali afungiwe jiwe na kutupwa katika kilindi cha maji marefu. Anazidi kusema kama kiungo kimojawapo cha mwili kinaleta chukizo basi ni vema kukiondoa na kubaki kilema kuliko kubaki mzima na ukapoteza uzima wa milele. Huu ni mwaliko wa kudumu kuhusu kazi ya kimisionari, na zaidi kazi ya wokovu inayodai utulivu na uvumilivu wa hali ya juu, kuweza kutafakari alama za nyakati tukiongozwa na Roho Mtakatifu.
Ninafurahi zaidi nikikutakia neema za Yesu mfufuka anayetukirimia Roho Mtakatifu kwa ajili ya wokovu wa watu na sifa kwa Mungu Baba.

Tumsifu Yesu Kristu.

TAFAKARI YA NENO LA MUNGU DOMINIKA YA 25 YA MWAKA B!

Na Paskal Linda
Ninakuletea ujumbe wa Neno la Mungu, Dominika ya 25 ya mwaka B wa Kanisa. Mama Kanisa anatufundisha wajibu wa Jumuiya kuwakumbatia maskini na walio wahitaji. Katika wimbo wa mwanzo Dominika ya 25, Bwana anasema mimi ni wokovu wa watu, na watu hawa wakinililia nitawaokoa katika taabu zao. Ndivyo basi Jumuiya ya Kikristu inavyopaswa kuwasikiliza na kuwakumbatia walio maskini.

Somo la kwanza linatoka katika kitabu cha Hekima ya Sulemani, na mwandishi anatupa bado sura ya mtumishi mwaminifu ambaye wanajamii wenzake wanamwonea wivu na wanaweka vitisho na vikwazo mbalimbali dhidi yake. Hata hivyo kwa kuwa ni mtumishi mwenye haki, yule aliyemtuma atamlinda mpaka mwisho. Kwa kuvumilia mateso katika upole na unyenyekevu anakuwa mfano kwa watesi wake na jumuiya nzima.  Mtumishi huyu anayetabiliwa na mwandishi wa kitabu cha Hekima anajitokeza katika sura ya Bwana wetu Yesu Kristu katika Agano Jipya.

Mpendwa mwanatafakari, jambo la mateso kwa waliowa kweli na watu wa haki katika mazingira ya leo linajitokeza bado na hivi je warudi nyuma au wasonge mbele katika kuvumilia magumu hayo? Kama Bwana wetu Yesu Kristu alivumilia mateso mpaka kufa, basi nasi tuliosafishwa katika Damu yake yatupasa kufuata nyayo zake mpaka mwisho.

Mtume Yakobo anaendela mbele kutufundisha juu ya maisha ya kila siku, leo anatupa Hekima itokayo juu kuwa kielelezo safi cha maisha ya mkristu. Anasema yeyote aifuataye Hekima hiyo atakuwa kinyume na machafuko na fitina katika maisha ya Jumuiya. Machafuko mbalimbali na hasa vita katika ulimwengu wa leo ni matunda ya tamaa za kimwili, na hivi Mt. Yakobo ataka tuzame zaidi katika Hekima ya kimungu itokayo juu, Hekima ambayo hutazama kwa upole na subira mambo yote na hasa kwa njia ya sala inayotangaza mapenzi ya Mungu. Anataka pia sala yetu iwe ni sala iliyojaa imani na tumaini na si tamaa za kimwili.

Katika somo la Injili, Mt Marko anatuonesha Yesu aliye katika utume na wakati huo anatoa katekesi kwa wanafunzi wake. Ni katika katekesi hiyo, Bwana anaendelea kukazia fundisho la kupokea kikombe cha mateso na kisha siku ya tatu kufufuka. Kwa kuwa Mitume bado wana mawazo ya Masiha mwenye nguvu za kivita hawasikilizi vema fundisho hili na badala yake wanajiuliza wao kwa wao, hivi mkubwa ni nani kati yetu! Wanafikiri juu ya vyeo katika ufalme wa Yesu Kristu Masiha!

Huu ni udhaifu na hasa waonesha kuwa hawajaelewa kitu!, hawajaelewa Bwana analenga wapi na njia gani anaifuata kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu. Ni udhaifu unaokuja kwa sababu katika historia ya ulimwengu kulikuwa na matabaka, ambayo mpaka hivi leo yapo tele.

Kwa kuwa Bwana, daima ni mwenye huruma na mvumilivu atatulia na kisha atawafundisha nini maana ya kuwa Mtume, nini maana ya kuwa mkubwa katika Jumuiya, nini maana ya kuwa kiongozi. Ndiyo kusema ukubwa katika Jumuiya ya Kanisa, uongozi ni kutumikia na kuhudumu jumuiya katika mahitaji yake na hasa kutangaza Injili ya Bwana.  Mhudumu anatakiwa kuwapokea wale wote wanaohangaika katika jumuiya, walio kama watoto wadogo. Bwana anaweka picha ya watoto wadogo mbele yetu kwa sababu katika jumuiya ya Kiyahudi mtoto ingawa wanampenda lakini bado anasadikika kutokuwa safi kwa sababu hatunzi sheria na makatazo mbalimbali.

Mpendwa mwanatafakari, katika jumuiya zetu hivi leo, katika nchi zetu jambo la nani mkubwa limeshika kasi kubwa mno kiasi kwamba malumbano ni makubwa mno. Utasikia daima ugomvi kwa sababu ya madaraka katika nchi zetu. Leo basi Neno la Mungu latuambia tuachane na mambo ya kushikilia vyeo kama ndiyo mwisho wa maisha yetu bali kama njia ya kuwatumikia wengine kwa upendo na hekima ya kimungu. Ndiyo kusema kama hatutafanya hivyo tuko nje ya ukristu, tuko nje ya matarajio ya mataifa na jumuiya zilizotuweka katika mamlaka hayo.
Ninakutakia furaha na matumaini katika kushika mafundisho ya Bwana aliye Masiha mteswa lakini mshindi kwa ajili ya ukombozi wa ulimwengu.

Tumsifu Yesu Kristu.

Daily Reading for Monday, September 28th, 2015

Reading 1, Zechariah 8:1-8

Responsorial Psalm, Psalms 102:16-18, 19-21, 29, 22-23

16 when Yahweh builds Zion anew, he will be seen in his glory;
17 he will turn to hear the prayer of the destitute, and will not treat their prayer with scorn.
18 This shall be put on record for a future generation, and a people yet to be born shall praise God:
19 Yahweh has leaned down from the heights of his sanctuary, has looked down from heaven to earth,
20 to listen to the sighing of the captive, and set free those condemned to death,
21 to proclaim the name of Yahweh in Zion, his praise in Jerusalem;
22 nations will gather together, and kingdoms to worship Yahweh.
23 In my journeying my strength has failed on the way;

Gospel, Luke 9:46-50

46 An argument started between them about which of them was the greatest.
47 Jesus knew what thoughts were going through their minds, and he took a little child whom he set by his side
48 and then he said to them, 'Anyone who welcomes this little child in my name welcomes me; and anyone who welcomes me, welcomes the one who sent me. The least among you all is the one who is the greatest.'
49 John spoke up. 'Master,' he said, 'we saw someone driving out devils in your name, and because he is not with us we tried to stop him.'
50 But Jesus said to him, 'You must not stop him: anyone who is not against you is for you.

Prayer of the Day for Tuesday, September 29, 2015

Holy Archangel Who Strengthened Our Lord in His Agony I salute thee, holy Angel who didst comfort my Jesus in His agony, and with thee I praise the most holy Trinity for having chosen thee from among all the holy Angels to comfort and strengthen Him who is the comfort and strength of all that are in affliction. By the honor thou didst enjoy and by the obedience, humility and love wherewith thou didst assist the sacred Humanity of Jesus, my Savior, when He was fainting for very sorrow at seeing the sins of the world and especially my sins, I beseech thee to obtain for me perfect sorrow for my sins; deign to strengthen me In the afflictions that now overwhelm me, and in all the other trials, to which I shall be exposed henceforth and, in particular, when I find myself in my final agony. Amen.

St. Michael the Archangel

Short Cuts
Image of St. Michael the Archangel

Facts

Feastday: September 29
Patron of grocers, mariners, paratroopers, police, and sickness

St. Michael the Archangel - Feast day - September 29th The name Michael signifies "Who is like to God?" and was the warcry of the good angels in the battle fought in heaven against satan and his followers. Holy Scripture describes St. Michael as "one of the chief princes," and leader of the forces of heaven in their triumph over the powers of hell. He has been especially honored and invoked as patron and protector by the Church from the time of the Apostles.
Although he is always called "the Archangel," the Greek Fathers and many others place him over all the angels - as Prince of the Seraphim. St. Michael is the patron of grocers, mariners, paratroopers, police and sickness

Papa Francis: Jengeni maisha yenu katika upendo


Papa Francis katika Ibada ya misa Takatifu ya Mkutano wa Dunia wa Familia - ANSA
: Na Paskal Linda
 
JUZI Jumapili 27 Septemba,2015  Papa Francis ameadhimsha kilele cha Misa Takatifu katika Uwanja wa Benjamini Franklin Parkway huko Philadelphia katika Mkutano wa dunia wa Familia kwa mwaka 2015.Mkutano wa siku mbili umeunganisha maelfu ya wajumbe kutoka sehemu mbambali za dunia ambao waliwakilisha familia za nchi zao. Na katika Homelia ya Papa Francis iliwatia moyo wanafamilia kujenga maisha yao katika upendo na kuwakumbusha kwamba upendo wa Mungu ni kwa kila mmoja  .
Akichambua juu ya masomo ya siku Papa Francis alisema: Neno la Mungu la siku linaleta mshangao na kutoa picha yenye nguvu na kuchochea sura. Sura hizo ni changamoto kwetu, lakini zinatia shahuku yetu.Kwenye somo la kwanza Joshua alimwambia Musa ya kwamba watu wawili kati yetu wanatoa unabii, wakiongea maneno ya Mungu bila kutumwa. Na katika Injili Yohane anelezea juu ya wanafunzi waliomkataza  mtu aliyekuwa anafukuza mapepo kwa jina la Yesu.
Papa alisema kweli  huo unaleta mshangao; kwani Musa na Yesu wote wana uwezo wa kukemea. Yesu alikutana na vizingiti  kutoka kwa watu wake  ambao hawakupokea kile alichokuwa akisema na kufanya. Maneno yake yalipokelewa na watu wale walikuwa wazi na waaminifu na wa kweli katika imani ya wanaume na wanawake wengi ambao hawakuwa  sehemu yoyote  ya wateule wa Mungu.Aliongeza Papa ya kwamba wanafunzi katika sehemu yao walitenda kwa imani yao njema.
Lakini majaribu na mashaka yao yalikuwa kuhusu uhuru wa Mungu ambaye uwanyeshea mvua watu wote wanyoofu na wasio na haki (Mt 5:45), yaani wale wenye  urasimu , wenye madaraka na duru za ndani , wanaotishia ukweli wa imani na kwa hivyo ni lazima kwa nguvu kukataliwa.
Lakini Papa akabainisha ya kwamba Mara sisi tunapolitambua , tunaweza kuelewa kwanini maneno ya Yesu yalileta kashfa miongoni mwao. Ukweli wa Yesu haujali kashfa za kila kitu ambacho ujaribu kuvunja na kuharibu imani yetu katika kazi ya roho! Mapenzi ya baba  hayataisha kamwe ya  kuendelea na ukarimu wake wa kupanda .Yeye utawanya mbegu za uwepo  wake katika dunia yote , kwa maana upendo wake unasisitiza hivyo ya kwamba siyo sisi tuliyompenda Mungu bali kwamba Munga alitupenda yeye kwanza (Yn 4:10)
Upendo wake unatupqtia uhakika ya kwamba Mungu ametuchagua , na anatusubiri .Na hii ndiyo inawapa wanafunzi  wake kuhamasika , na kutoa huduma ya  kutenda mambo yaliyo mema yanayotekea kwa majirani zao wanao wazunguka. Kwani Mungua anataka watoto wake wote washiriki katika sikukuu ya Injili. Ni watu wangapi walioko pale katika madhimisho ya Familia; papa alisema: Hii peke yake ni jambo la unabii , ni aina ya miujiza katika dunia ya leo,  wote wanaweza kuwa manabii, wote wanaweza kufungulia miujiza ya upendo kwaajili ya familia zote za dunia, na hivyo kushinda kashfa nyembamba, upendo mdogo uliojifungia ndani yake yaani ubinafsi.