Week Hot newz

Tafakari ya Neno la Mungu, Jumapili ya IV ya Kipindi cha Mwaka C wa Kanisa


Tafakari ya Neno la Mungu Jumapili ya IV ya Mwaka C wa Kanisa. - OSS_ROM
28/01/2016 14:25
“Leo hii maneno haya yametimia masikioni mwenu”. Kifungu hiki cha maneno ndicho kinafungua Injili ya Dominika hii ya 4 ya mwaka C wa Kanisa. Kusudi tupate kuelewa vema hatuna budi kurejea katika Injili ya Dominika iliyopita tuliposikia Kristo akiwa katika Sinagogi katika kijiji chake cha Nazareti na alisoma sehemu ya kitabu cha Nabii Isaya ambacho kilikuwa ni maneno ya matumaini kwa mmoja ambaye alikuwa anatafuta auheni katika maisha. Kristo leo anawapatia hawa ndugu zake na pia anatupatia sisi habari njema. Anajifunua kwa watu wake wa Nazareti na kwa njia hiyo anajifunua kwa wanadamu kuwa ujio wake ndiyo utimilifu wa uaguzi huo wa nabii Isaya. Ujio wake hapa ulimwenguni ni mwanzo mpya kwa maisha ya mwanadamu; ukurasa mpya umefunguliwa ambao unamuweka mwanadamu katika hali njema tena.
 
Katika lugha adhimu ya Kiswahili upo msemo usemao: “Fadhila mfadhilie mbuzi mwanadamu ana maudhi”. Ujumbe huu wa furaha unapokelewa isivyotegemewa. Fadhila hii ya Mungu kwa mwanadamu inapata mwitikio hasi: “wakajaa ghadhabu wote waliokuwa katika sinagogi walipoyasikia hayo”. Wanashindwa kuipokea huruma ya Mungu inayofunuliwa kwao kwa sababu tu ya unasaba wa mjumbe wa Mungu. Wanashindwa kulipokea Neno na kuanza kumshambulia mtoa neno. Hii ni ajabu kabisa kwani hata kama utafanikiwa kumwangamiza anayekupatia ujumbe wowote ule kamwe hautaweza kuifuta kauli yake aliyoitoa, yaani ukweli alioutangaza.

Papa "Wambea hawana bunge na wala umbea si mtaji wangetajirika wengi"

Baba Mtakatifu Francisko anawataka watawa kuwa ni mashuhuda wa kinabii, watu wanajenga utamaduni wa ujirani mwema na watu wenye matumaini kwa Mwenyezi Mungu. - OSS_ROM
02/02/2016 07:39
Maadhimisho ya kufunga Mwaka wa Watawa Duniani, Jumatatu tarehe Mos Februari 2016 yalichukua sura mpya pale Baba Mtakatifu Francisko alipokabidhi hotuba yake kuhusu wosia ambao amependa kuwakabidhi watawa wakati huu Mama Kanisa anapofunga rasmi maadhimisho ya Mwaka wa Watawa Duniani kwa kuwataka wayakite maisha yao katika mambo makuu matatu: Unabii, Ujirani na Matumaini. Baba Mtakatifu akaamua kutoa katekesi ya kina kwa kuzungumza na watawa moja kwa moja, ili kuangalia ukweli wa maisha na utume wa watawa ndani ya Kanisa.