
Baba
Mtakatifu Francisko mara baada ya maadhimisho ya Ibada ya Misa Takatifu
kwenye Uwanja wa
Huruma ya Mungu, Jimbo kuu la Cracovia Jumapili tarehe
31 Julai 2016 kama sehemu ya maadhimisho ya kufunga rasmi maadhimisho ya
Siku ya XXXI ya Vijana Duniani kwa mwaka 2016, kabla ya kusali Sala ya
Malaika wa Bwana na vijana kutoka sehemu mbali mbali za dunia,
aliwashukuru wadau mbali mbali waliojisadaka kwa ajili ya kuandaa na
hatimaye kufanikisha maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani.
Baraza la Maaskofu Katoliki Panama limepewa dhamana ya kuandaa Siku ya Vijana Duniani kwa mwaka 2019.