Week Hot newz

Bodaboda zapigwa marufuku!

Burundi imepiga marufuku bodaboda au pikipiki kuingia katikati mwa mji mkuu Bujumbura katika juhudi za kujaribu kupunguza mashambulio.Pikipiki hutumiwa sana kusafirisha watu na mizigo Bujumbura lakini sasa zimekuwa zikitumiwa kutekeleza mashambulio, meya wa Bujumbura Freddy Mbonimpa anasema.

Mtu mmoja aliuawa Jumatatu wiki hii watu waliokuwa wamepaki pikipiki waliporusha guruneti tatu.
Usalama umeimarishwa mjini humo tangu kutoka kwa mashambulio hayo na polisi wanapekua watu na magari, shirika la habari la AFP linasema.

“Polisi wamegundua kwamba wahalifu hubeba guruneti wakitumia mabegu au vikapu,
” Bw Mbonimpa anasema. Mwandishi wa BBC aliyeko Bujumbura Prime Ndikumagenge anasema marufuku hiyo itaathiri sana watu wanaosafiri kutoka eneo moja hadi jingine mjini.

Huwezi kutoka kusini mwa mji hadi kaskazini bila kupitia katikati mwa mji, anasema.
Machafuko yalizuka nchini Burundi Aprili mwaka jana Rais Pierre Nkurunziza, ambaye amekuwa uongozini tangu 2005, alipotangaza kwamba angewania urais kwa muhula wa tatu.
Watu 400 wamefariki na wengine 240,000 kutorokea nchi jirani tangu wakati huo.

Papa Francisko nchini Mexico

Majadiliano ya kiekumene yamechukua sura mpya kwa papa Francisko na Patriaki Kirill wa Moscow na Russia nzima kukutana.
Majadiliano ya kiekumene yamechukua sura mpya kwa papa Francisko kukutana na Patriaki Kirill wa Moscow na Russia nzima.
Mapambazuko mapya ya majadiliano ya kiekumene!
16/02/2016 14:43Baba Mtakatifu Francisko na Patriaki Kirill wa Moscow na Russia nzima wamekutana na kuzungumza pamoja na kutia sahihi Tamko la shughuli za kichungaji kwa Makanisa haya mawili, ili kuanza kuandika ukurasa mpya wa majadiliano ya kiekumene katika Millenia ya tatu ya Ukristo!

 

 
 Baba Mtakatifu akishiriki chakula cha mchana na familia ya Mungu nchini Mexico.
Baba Mtakatifu Francisko akiwa nchini Mexico, Jumatatu tarehe 15 Februari 2016 ametembelea Kanisa kuu la san Cristòbal de las Casa na kusali humo, ameshiriki chakula cha mchana pamoja na wawakilishi wa Familia ya Mungu nchini Mexico pamoja na kuzungumza na  kusali nao!

 

Baba Mtakatifu Francisko akiwa Mexico amesikiliza shuhuda za Injili ya familia.
Baba Mtakatifu Francisko akiwa nchini Mexico amesikiliza shuhuda wa Injili ya familia.

Mashuhuda wa Injili ya familia!

16/02/2016 10:42Baba Mtakatifu Francisko alipokutana na familia nchini Mexico amesikiliza shuhuda za watu waliotelekezwa na familia zao, lakini wakapata fursa ya kuonja huruma na upendo wa Mungu kwa njia ya Kanisa; amesikiliza mashuhuda waliokumbatia utamaduni wa kifo, leo hii wanashuhudia Injili ya uhai!

 


Baba Mtakatifu Francisko anawahimiza wananchi wa Mexico kujikita katika ushuhuda wa tunu msingi za Injili ya furaha!
Baba Mtakatifu Francisko anawahimiza wananchi wa Mexico kuwa ni mashuhuda wa Injili ya familia.

Iweni mashuhuda wa Injili ya familia na huruma ya Mungu!

16/02/2016 10:21Baba Mtakatifu anawaalika wanafamilia kuwa kweli ni mashuhuda wa Injili ya familia na vyombo vya huruma ya Mungu ili kuweza kupambana na changamoto mbali mbali zinazojitokeza katika maisha na utume wa familia; kwa kushinda upweke na kinzani za maisha!
Baba Mtakatifu Francisko akiadhimisha Ibada ya Misa Takatifu na wenyeji wa Chiapas, nchini Mexico
Baba Mtakatifu Francisko akiadhimisha Ibada ya Misa Takatifu na wenyeji wa Chiapas, nchini Mexico.

Onesheni ujasiri wa kuomba msamaha!

16/02/2016 10:02Baba Mtakatifu Francisko akiwa nchini Mexico anasema, umefika wakati wa kujenga na kudumisha udugu, haki, mshikamano na amani; kwa kutambua kwamba haya ni mambo msingi yanayowaunganisha binadamu kama watoto wateule wa Mungu dhidi ya nyanyaso, dhuluma na ubaguzi!
Maskini wanapaswa kujipanga vyema zaidi ili kupambana na ubaguzi kwa kushikamana ili kudumisha utu wao na kupata mahitaji msingi!
Maskini wanapaswa kujipanga vyema kwa kushikamana kutetea utu na heshima yao kwa kupinga ubaguzi na nyanyaso, ili kukuza utu na heshima yao pamoja na kujipatia mahitaji msingi ya maisha.

Changamoto za utunzaji bora wa mazingira nyumba ya wote!

15/02/2016 10:39Kardinali Peter Turkson, Rais wa Baraza la Kipapa la haki na amani anawapongeza wenyeji wa Mexico kwa kuonesha mwanga angavu katika kulinda na kutunza mazingira nyumba ya wote, sanjari na kuendelea kushikamana ili kupambana na changamoto za maisha ili kudumisha utu wao!

 

Baada ya Askofu mkuu Ivan Jurkovic kukamilisha utume wake nchini Russia ameteuliwa kuwa Mwakilishi wa kudumu wa Vatican UN, Geneva.
Baada ya Askofu mkuu Ivan Jurkovic kukamilisha utume wake kama Balozi wa Vatican nchini Russia, ameteuliwa kuwa mwakilishi wa kudumu wa Vatican kwenye ofisi za UN zilizoko Geneva, Uswiss.

Askofu mkuu Ivan Jurkovic ateuliwa kuwa Mwakilishi wa kudumu UN, Geneva

15/02/2016 10:24Askofu mkuu Ivan Jurkovic ameteuliwa kuwa Mwakilishi wa kudumu wa Vatican kwenye Ofisi za Umoja wa Mataifa zilizoko mjini Geneva ili kuchukua nafasi ya Askofu mkuu Silvano Maria Tomasi ambaye amekuwepo huko tangu mwaka 2003. Aliwahi kuwa Balozi wa Vatican nchini Ethiopia na Eritrea.

 

Baba Mtakatifu Francisko ametembelea Hospitali ya "Federico Gomez" Mexico kushukuru kwa huduma na kuwabariki watoto wagonjwa wa saratani!
Baba Mtakatifu Francisko ametembelea Hospitali ya "Federico Gomez" ili kushukuru kwa huduma makini zinazotolewa kudumisha Injili ya uhai pamoja na kuwaombea watoto wagonjwa katika shida na mhangaiko yao!

Papa Francisko kielelezo cha faraja na matumaini kwa wagonjwa!

15/02/2016 10:07Baba Mtakatifu Francisko, Jumapili tarehe 14 Februari 2016 ametembelea Hospitali ya "Federico Gomez" nchini Mexico ili kumshukuru Mungu kwa huduma inayotelewa kwa ajili ya watoto wagonjwa pamoja na kubariki kazi njema inayofanywa na wazazi pamoja na wahudumu wa sekta ya afya!

Pope Francis' prayer intentions for February 2016

Baba Mtakatifu: Onesheni ujasiri wa kuomba msamaha!



Familia ya Mungu mjini Chiapas, nchini Mexico imempokea Baba Mtakatifu Francisko katika mji wao kwa bashasha na shangwe kubwa iliyokuwa inajionesha katika nyuso za watu, katika midundo na rangi za mavazi yao. Bahari ya watu ilifurika, siku ya Jumatatu tarehe 15 Februari 2016 huko Chiapasa, wakati Baba Mtakatifu alipokwenda mjini humo kuadhimisha Ibada ya Misa takatifu pamoja na wenyeji wa Chiapas, huko San Cristobal, DLC. Ibada hii imeadhimishwa kwa kutumia lugha mahalia, changamoto ya kutamadunisha Injili ili kweli Injili iweze kuingia na kuzama katika maisha, mila na tamaduni za watu!
 Katika mahubiri yake, Baba Mtakatifu anasema, Neno la Mungu linafanya rejea katika maisha ya watu wa Chiapas, ambao kwa miaka mingi walitengwa, wakadhulumiwa na kunyanyaswa na mifumo mbali mbali ya kisiasa. Umefika wakati wa kuchunguza dhamiri na kuomba msamaha kwa makosa yaliyotendeka katika historia, tayari kuanza kuandika ukurasa mpya unaojikita katika haki msingi za binadamu, sanjari na utunzaji bora wa mazingira, nyumba ya wote! Baba Mtakatifu anafafanua kwamba, Waisraeli walipokuwa utumwani Misri walionja mateso na nyanyaso, wakamlilia Mungu naye akawasikiliza, kwa kuwaonesha uso wa huruma kwa njia ya Neno na Sheria zake, ambazo zikawa ni chemchemi ya uhuru, furaha, hekima na mwanga wa maisha kwa watu waliokuwa wanatembea katika giza la maisha. Hata wananchi wa Chiapas anasema Baba Mtakatifu kwa miaka mingi wametembea katika dhuluma na nyanyaso; wakang’olewa hata katika ardhi yao; mambo ambayo yameacha chapa ya kudumu katika nyoyo za watu!
Baba Mtakatifu anakaza kusema, umefika wakati wa kujenga na kudumisha udugu, haki, mshikamano na amani, kwa kutambua kwamba, haya ni mambo msingi yanayowaunganisha wote kama watoto wa Baba yao wa mbinguni, aliyewaletea Kristo Yesu, anayetembea pamoja nao katika hija yao ya maisha. Yesu ni njia, ukweli na uzima anayetaka kuwasaidia waja wake kushinda giza la maisha. Nyanyaso na dhuluma zimesababisha madhara makubwa katika maisha ya watu wengi, lakini bado Mwenyezi Mungu anaonesha huruma na upendo kwa waja wake.
Baba Mtakatifu anaendelea kukemea vikali matumizi mabaya ya rasilimali na utajiri wa dunia ambao ni zawadi kubwa kwa binadamu kwa kudhani kwamba, wao ni wamiliki na kusahau kuwa wamedhaminishwa na Mwenyezi Mungu ili kuitunza na kuiendeleza dunia, iweze kuwa ni mahali pazuri zaidi pa kuishi. Vita inayojikita bado katika mioyo ya binadamu ni matokeo ya madhara ya dhambi yanayojionesha hata katika matumizi mabaya ya ardhi na maji pamoja na kusababisha uchafuzi mkubwa wa mazingira; mambo ambayo yana athati kubwa katika maisha ya watu wengi.
Baba Mtakatifu anaendelea kufafanua kwamba, athari za uchafuzi wa mazingira zinawagusa binadamu wote na kwamba, hii ni kati ya changamoto kubwa inayomwandama mwanadamu katika ulimwengu mamboleo. Wananchi wa Chiapas ni mfano bora wa kuigwa kwa kulinda, kutunza na kudumisha mazingira bora na kwamba, Jumuiya ya Kimataifa inaweza kujifunza mengi kutoka kwao. Mazingira imekuwa ni nyumba ya wote, chanzo cha lishe na Altare ya ushirikiano kati ya watu!
Baba Mtakatifu Francisko anasikitika kusema, wananchi wa Chiapas wakati mwingine hawakueleweka; tunu msingi, tamaduni na mapokeo yao yakadhalilishwa; kwa watu kutaka kukumbatia madaraka, utajiri, fedha huku wakisukumwa na kanuni msingi za soko; wakawekeza katika mambo makubwa, ambayo kwa wakati huu ni chanzo kikuu cha uharibifu wa mazingira. Umefika wakati wa kuchunguza dhamiri na kuthubu kuomba msamaha kutokana na utandawazi usiojali wala kuguswa na mahangaiko ya wengi kwa kuonesha kwamba, hata wao ni muhimu sana katika mchakato wa maendeleoya jamii.