Week Hot newz

Wapentekoste washikana uchawi


Mwenyekiti wa Ushirika wa Wachungaji wa Kanisa la Pentekoste Tanzania (PPFT), Askofu Pius Ikongo
SIKU moja baada ya Ikulu kuliumbua Baraza la Maaskofu wa Kipentekoste Tanzania (PCT) kwamba hawakuwasilisha majina ya uteuzi kwa Rais Jakaya Kikwete, wameanza kushikana uchawi kumsaka aliyesababisha majina hayo kutofika Ikulu.
Hayo yamethibitishwa jana jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Ushirika wa Wachungaji wa Kanisa la Pentekoste Tanzania (PPFT), Askofu Pius Ikongo, alipokuwa akizungumza na Blogu hii.
Akizungumzia kuhusu tamko hilo la Ikulu, Askofu Ikongo alisema kuwa wanafanya uchunguzi kumnasa aliyesababisha kutofika majina hayo mezani kwa Rais Kikwete.

Daily Reading for Friday, February 21st, 2014


Reading 1, James 2:14-24, 26

14 How does it help, my brothers, when someone who has never done a single good act claims to have faith? Will that faith bring salvation?
15 If one of the brothers or one of the sisters is in need of clothes and has not enough food to live on,
16 and one of you says to them, 'I wish you well; keep yourself warm and eat plenty,' without giving them these bare necessities of life, then what good is that?
17 In the same way faith, if good deeds do not go with it, is quite dead.
18 But someone may say: So you have faith and I have good deeds? Show me this faith of yours without deeds, then! It is by my deeds that I will show you my faith.
19 You believe in the one God -- that is creditable enough, but even the demons have the same belief, and they tremble with fear.
20 Fool! Would you not like to know that faith without deeds is useless?
21 Was not Abraham our father justified by his deed, because he offered his son Isaac on the altar?
22 So you can see that his faith was working together with his deeds; his faith became perfect by what he did.
23 In this way the scripture was fulfilled: Abraham put his faith in God, and this was considered as making him upright; and he received the name 'friend of God'.
24 You see now that it is by deeds, and not only by believing, that someone is justified.
26 As a body without a spirit is dead, so is faith without deeds.

Responsorial Psalm, Psalms 112:1-2, 3-4, 5-6

1 Alleluia! How blessed is anyone who fears Yahweh, who delights in his commandments!
2 His descendants shall be powerful on earth, the race of the honest shall receive blessings:
3 Riches and wealth for his family; his uprightness stands firm for ever.
4 For the honest he shines as a lamp in the dark, generous, tender-hearted, and upright.
5 All goes well for one who lends generously, who is honest in all his dealing;
6 for all time to come he will not stumble, for all time to come the upright will be remembered.

Gospel, Mark 8:34--9:1

34 He called the people and his disciples to him and said, 'If anyone wants to be a follower of mine, let him renounce himself and take up his cross and follow me.
35 Anyone who wants to save his life will lose it; but anyone who loses his life for my sake, and for the sake of the gospel, will save it.
36 What gain, then, is it for anyone to win the whole world and forfeit his life?
37 And indeed what can anyone offer in exchange for his life?
38 For if anyone in this sinful and adulterous generation is ashamed of me and of my words, the Son of man will also be ashamed of him when he comes in the glory of his Father with the holy angels.'
1 And he said to them, 'In truth I tell you, there are some standing here who will not taste death before they see the kingdom of God come with power.'

St. Severian

St. Severian
Feastday: February 21
Died: 452

Bishop and martyr. The bishop of Scythopolis in Galilee. He attended the Council of Chalcedon (451) and took part in the complete triumph of the orthodox Christian cause against the heretics of the era. On his return home he was assassinated by a group of heretics at the command of Emperor Theodosius II.

Tafakari ya Neno la Mungu, Jumapili ya Saba ya Kipindi cha Mwaka A wa Kanisa

Mpendwa karibu  kipindi cha tafakari masomo Dominika, ninakuletea ujumbe wa Neno la Mungu nikisema kuweni watakatifu kama Baba yenu aliye mbinguni. Huo ndo wito wa kila awaye yote anayetaka kupata wokovu yaani uzima wa milele. Tuko tayari Dominika ya VII ya mwaka A wa Kanisa.
Katika Somo la kwanza kutoka Kitabu cha Mambo ya Walawi, tunapata kuanza kusikia mwaliko wa kuwa watakatifu tukifuata mfano thabiti na wa uhakika yaani Mungu mwenyewe. Mungu anawasiliana na taifa lake kwa njia ya Musa akitaka wawe watakatifu kama yeye alivyo. Anasonga mbele akieleza kilichomo ndani ya safari ya utakatifu: kuachana na chuki, kukemea maovu yanayojiri katika jumuiya na majirani zetu na kuachana na kinyongo na kisirani katika maisha yako. Ili kutekeleza haya lazima kujitenga na dunia, kama iliyo maana ya utakatifu katika Agano la Kale (mkumbuke Mtakatifu Antonio Abate, mwanzilishi wa Umonaki).

Kwa hakika utakatifu ulikuwa na maana ya kuwekwa pembeni kwa ajili ya Mungu. Patakatifu pa patakatifu palimaanisha Mungu mwenyewe. Ni katika maana ileile, wakristu lazima wajitenga kiroho na chachu ya dunia yaani kuachana na maisha ya dhambi. Ndiyo kusema kukazia amri ya mapendo kwa jirani na si kujitenga na wapagani kama Waisraeli walivyokuwa wakifikiri. Ni kumpenda Mungu tukiambatana na wenye shida mbalimbali tukielekea wote mbinguni.

Mtume Paulo anapowaandikia Wakorinto anakazia ule utakatifu tuliokabidhiwa na Mungu. Anasema sisi ni hekalu la Roho Mtakatifu. Mpendwa, nikishasikia neno hilo mara moja mwaliko ni kutunza utakatifu ili niendelee kubaki Hekalu safi kwa ajili ya kumwabudia Mungu. Katika Ukorinto kulikuwa na ugomvi na ulitokana na tishio la kutopendana na hapa ndipo Mtume Paulo anakuja na fundisho kali akikemea uozo huo unaojitokeza katika sura ya utengano.

Katika Injili, Mwinjili Matayo, anaweka mbele yetu mausia ya Bwana kuhusu sheria ya kale. Bwana anataka mabadiliko ya uelewa wa sheria, ya kwamba ni kwa ajili ya kujenga umoja kwa watu na si kuangamiza. Anataka sheria izame katika utu zaidi kuliko mambo mengine na ilinde maisha, iliyo zawadi ya Mungu. Mpendwa mwanatafakari, Hata hivyo yatupasa kuelewa nini maana ya sheria za zamani, mfano Jicho kwa jicho au jino kwa jino!! Mara kadhaa tunatafsiri jambo hili kadiri ya maneno yalivyo kwa nje! Na hivi huleta maana potofu! Kwa hakika mwanzo wa sheria hii ulikuwa mzuri!

Maana yake nini! Ni kwamba kabla ya sheria hii mtu alipokuwa akitenda kosa fulani alikuwa analazimika kulipa fidia si kwa makosa yake tu bali hata kwa makosa mengine yasiyo yake. Na hivi ikawa ni mateso makubwa kwa watu, basi ikatungwa sheria ya jicho kwa jicho, yaani mtu alipie fidia ya makosa yake tu! Kumbe kukazaliwa namna mpya na ya haki katika kutawala na kuongoza haki katika Jumuiya. Ndiyo kusema hakukuwa na matumizi ya moja kwa moja yaani ya kuondoana macho au meno! Ndiyo kusema walitaka kufundisha ule uwiano kati ya kosa na adhabu .

Mpendwa mwanatafakari, Bwana anasema imeandikwa jicho kwa jicho kama njia ya kutenda, lakini mimi nasema epukeni magomvi, majibizano katika maisha yenu. Ni heri kuvumilia na kuachana na mwendelezo wa mapigano. Hataki kuondoa haki ila anataka kuwepo na upole na unyenyekevu wa moyo katika maisha ya watu wakitafuta haki, ili mbele ya taabu tupate kutunza umoja na utulivu katika jumuiya.

Bwana anafundisha kwa hakika, njia ya pekee ya kuondoa mnyololo wa fitina ni msamaha. Kwa maana mtu akikupiga na ukamsamehe mara moja hakuna nyongeza ya ukubwa wa mapigano, lakini kama ukijibu kwa mapigano basi nyongeza mara mbili ya shida katika jumuiya. Anazidi kukazia upendo hata kwa adui, na hii ndiyo namna ya kwenda kinyume na mantiki ya zamani kuhusu upendo.

Mpendwa, mantiki ya zamani na ya sasa kuhusu upendo ni ipi? Kwa hakika hapo zamani ilikuwa mpende akupendaye kinyume na mantiki ya Kristu katika Agano Jipya isemayo, mpende hata adui yako. Bwana haondoi ile ya kwanza bali anaiongezea nguvu na kuikamilisha. Mpendwa, yashike haya yote yaliyousiwa na Bwana na kuyaishi na hivi utakuwa mtakatifu kama Baba yetu aliye mbinguni.

Nikutakie furaha na matumaini katika kuishi sheria mpya, sheria ya Mungu itujengeayo uhuru na mshikamano na Kristo. Tumsifu Yesu Kristo.

Tafakari hii imeletwa kwako na Padre Richard Tiganya C.PP.S.

Ili kuimjua Yesu ni lazima kumfuata- Papa Francis


(Vatican) Kumjua Kristu ni kutembea nae katika utendaji wote wa kila siku na si kumfahamu kinadharia au kwa kusoma tu maandishi yake. Huo ulikuwa ni ujumbe wa Papa Francisko wakati wa Ibada ya Misa Alhamisi asubuhi katika Kanisa dogo la Mtakatifu Marta. Alieleza kwamba , kila siku Kristu hutuuliza "Yeye ni nani kwetu" , na inawezekana tu kutoa jibu kwa kuishi nae kama iilivyokuwa kwa wanafunzi.

Papa amesema Ukristu ni maisha ya mwanafunzi , kuliko maisha ya utafiti. Mkristu kuujua ukweli wa Yesu ni nani kwake, ni kuingia katika hija na kufuata nyayo za Mwalimu wa ushuhuda wazi , na uvumilivu katika yote, usaliti , udhoofu wa mwili na kupita katika mashinikizo mapya yenye mikingamo mikali. Papa Francisko alieleza na kutoa mfano wa Petro , ambaye katika Injili ya siku ilimwonyesha yote kwa wakati mmoja, kama shahidi shupavu , anayejibu maswali ya Yesu kwa Mitume , “Na ninyi je, mnasema mimi ni kwenu”? akijibu "Wewe ni Kristo" , na mara baadaye akawa kinyume chake, akamkana kama adui , na mara akipatwa na aibu , akaona anahitaji kukutana tena na Yesu, ambaye alikuwa tu ametangaz a mateso na kifo na ufufuko wake. Papa aliasa, mara nyingi ,Yesu anarudi kwetu na kutuuliza , “Mimi ni nani kwako” na tunampa jibu kama hilo la Petro, , Jibu tulilojifunza wakati wa Kateksimu , lakini jibu hilo halitoshi.

Papa aliendelea kufafanua kwamba, inaonekana kutoa jibu katika swali hilo tunaliliosikia ndani ya mioyo yetu , Yesu ni Nani kwatu, kwa yale ambayo tumeyasikia na kujifunza haitoshi. Wala kusoma na kuelewa peke yake haitoshi . Kumjua Yesu kweli , ni kutembea na Yesu katika njia yake, kama Mtume Petro alivyofanya ,baada ya kumkana, aliuona ukweli wa Yesu ni nani na kubadili mwenendeno wake . Petro alikwenda mbele na Yesu,alizona ishara alizofanya, aliona nguvu za Yesu, na kumkiri kuw andiye Kristu.

Petro , Papa Francisko aliendelea, aliomba msamaha kwa Yesu - na bado, baada ya ufufuo, aliulizwa na Yesu mara tatu katika mwambao wa ziwa Tiberia : " Wanipenda ?". Pengine, Papa alisema ,Yesu alitaka kuthibitisha upendo kamili wa Petro kwa Bwana wake , Petro alitokwa namachozi na kuona ea aibu wakati alipomkana mara tatu wakati wa mateso yake.

Papa anasema , ni kukutana kila siku na Bwana, kila siku ni kumshudia ushindi wetu na udhaifu wetu." Lakini , safari hii hatuwezi kuifanya wenyewe, tunamhitaji Roho Mtaktifu , aingilie kati , kama jambo muhimu.


Papa amehimiza, kumjua Yesu ni zawadi itokayo kwa Baba , ni Yeye anaye tufanikisha kumjua Yesu. Ni kazi ya Roho Mtakatifu, anaye fanya kazi hii kubwa. Hizi si kama juhudi za kibiashara au mashirikisho ya wafanyakazi , lakini ni Roho Mtakatifu, Mfanyakazi hodari ambaye daima huifanya kazi yake . Huifanya kazi hii ya kueleza fumbo la Yesu na kutupatia sisi maana ya Yesu ni nani kwetu. Papa aliomba tuyaweke mawazo yetu wakati ule wa Yesu akiwauliza mitume wake , Petro , Mitume ,tulisikie swali hilo a ndani ya mioyo yetu, “ Mimi ni nani kwako”? Na kama wafuasi wake na tumwomba Baba atujalie sisi sote, kumjua Kristo katika Roho Mtakatifu, ambaye atatupa jibu , la siri huu kuu , Yesu ni nai kwetu. .

Ulevi wa kupindukia ni chanzo cha majanga mengi duniani!


Zaidi ya watu millioni mbili na nusu hufariki dunia kila mwaka kutokana na ulevi wa kupindukia. Waathirika wakubwa wa janga hili la ulevi ni vijana kuanzia miaka kumi na mitano, hali ambayo inahatarisha usalama na ustawi wa maisha ya vijana hawa kwa siku za usoni kiasi kwamba, wanaweza kukosa dira na mwelekeo wa maisha.
Inasikitisha kuona kwamba, vijana wenye umri mdogo kabisa wanaathirika kwa unywaji wa pombe kupindukia. Ulevi ni kati ya mambo ambayo yanaendelea kuchangia magonjwa na vifo vya ghafla. Hii ndiyo maana wataalam wa masuala ya afya wanasema kwamba, ulevi wa kupindukia ni hatari kwa maisha ya binadamu, kwani pombe si maji wala “juice”.
Kutokana na changamoto hizi, Taasisi ya Kipapa ya Sayansi Jamii, hivi karibuni iliendesha warsha ya siku moja iliyoaunganisha wanasayansi na viongozi wa Kanisa ili kufanya tafakari ya kina kuhusu madhara ya ulevi wa kupindukia katika maisha ya vijana, jambo ambalo linapaswa kuwekewa mikakati maalum ya kichungaji, ili kuwasaidia vijana kuheshimu zawadi ya maisha yao binafsi na yale ya jirani zao.
Ulevi wa kupindukia ni tatizo linalopaswa kuvaliwa njuga kwa ajili ya ustawi na mafao ya mtu binafsi na Jumuiya kwa ujumla. Hii ndiyo kauli mbiu iliyofanyiwa kazi na wadau mbali mbali kutoka ndani na nje ya Vatican. Katika tafakari yake, Kardinali Oscar Rodriguez Maradiaga, Rais wa Shirikisho la Mashirika ya Misaada ya Kanisa Katoliki Kimataifa, Caritas Internationalis, amekazia umuhimu wa kupambana na ulevi wa kupindukia kwa kujikita katika kanuni maadili na utu wema.
Ulevi ni jambo linaloathiri afya ya mtu, kiasi hata cha kumong’onyoa tunu msingi za kimaadili na utu wema, Ulevi umekuwa pia ni chanzo cha ajali nyingi barabarani pamoja na uharibifu mkubwa wa mali na miundo mbinu inayogharimu kiasi kikubwa cha fedha ya walipa kodi.
Takwimu zinaonesha kwamba, Bara la Ulaya linaongozwa kwa ulevi wa kupindukia. Inakadiriwa kwamba, kuna zaidi ya watu millioni kumi na tano wanaosumbuliwa na ugonjwa wa ulevi wa kupindukia. Katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, hali ya ulevi Barani Ulaya hakuongezeka sana, pengine hii inatokana na kampeni zilizoendeshwa na wadau mbali mbali dhidi ya ulevi wa kupindukia. Kiasi cha Euro billioni 156 zinatumika kila mwaka kwa ajili ya kugharimia hasara zinazojitokeza kutokana na ulevi wa kupindukia.
Huduma kwa watu wanaosumbuliwa na ugonjwa waulevi wa kupindukia bado ni kidogo sana, kwani baadhi ya watu wanadhani huu si ugonjwa wa kupatiwa tiba bali ni starehe. Inawezekana kabisa kwa mlevi kuachana na tabia hii akizingatia masharti pamoja na kuendelea kupokea ushauri nasaha. Inasikitisha kuona kwamba, vileo ni kati ya bidhaa zinazoyaingizia mataifa mengi fedha ya kodi ya mapato. Lakini umefika wakati wa kuangalia pia afya na usalama wa maisha ya raia kwa kuweka mikakati ya kudhibiti tabia ya ulevi wa kupindukia.