Week Hot newz

GOtv Cecafa Senior Challenge:Ethiopia hold Kenya

David Owino 




Hosts Kenya were held to a goalless draw against Ethiopia in an exciting group A encounter played at Nyayo Stadium in the second game of the GOtv Cecafa Senior Challenge on Wednesday.
The well attended game started on a low note with both sides playing cautiously with the visitors who just arrived a day before keeping the hosts at bay Thok James and Salhadin Bargecho impressing.
The second half was a see saw affair with both coaches ringing changes that did not materialize into goals. Jacob Keli came on for David Gateri while Mulinge Ndeto replaced Musa Mohamed.
Ethiopia coach Sewnet Bishaw was impressed with his team’s performance.
"I am very happy with the one point since this team has been together for only four days before we travelled to Kenya. This is a development side and we have nothing to lose but we will play our next opponents seriously while hoping for the best."
His counterpart James Nandwa who was standing in for Adel Amrouche who went Awol shared the same sentiments.
"It was a tough game but we are happy with the single point as Ethiopia are a very good side .We are optimistic we will give our best in the upcoming matches," Nandwa told supersport.com.
The result means Zanzibar are on top of group A with three points followed by Kenya and Ethiopia who have a point each while South Sudan are last with no point after losing to Zanzibar.

GOtv Cecafa Senior Challenge:Zanzibar edge out South Sudan






Zanzibar Heroes opened their account in the 2013 GOtv Cecafa Senior Challenge with a 2-1 win over hardfighting South Sudan in an exciting match played at the Nyayo Stadium in Nairobi.
Suleiman Kassim Suleiman broke the deadlock in the fifth minute capitalizing from a school boy blunder by South Sudan keeper Awad Goma Genaro who dilly dallied with the ball and was then stripped off it by Kassim who then rolled it into the net.
However the goal did not dampen the spirit of the Sudanese who fought gallantly forcing Zanzibar to defend with Bengal based James Joseph Mogga being in the thick of things with his darting runs in the Zanzibar defence.
Abdiyum Saleh Ahmed added the second goal for Zanzibar in the 67th minute just five minutes after coming in turning the heat on South Sudan before as he scored past a sprawled Genaro in South Sudan's goal.
South Sudan scored their consolation goal in the 74th minute when substitute Fabiano Elias Lako collected a pass from hardworking Mogga before finishing off clinically.
The win ensured Zanzibar went to the top of group A with three points

Tanzanite vs Afrika Kusini sasa Uwanja wa Taifa

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limeihamisha mechi ya kuwania tiketi ya fainali za Kombe la Dunia kwa wanawake wenye umri chini ya miaka 20 kati ya Tanzania ‘Tanzanite’ na Afrika Kusini ‘Amajita’ kutoka Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza hadi Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Tanzanite inajiandaa kuikaribisha Amajita Desemba 7 katika mechi ya kwanza ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia zitakazopigwa mwakani nchini Canada, baada ya kuwang’oa Msumbiji kwa jumla ya mabao 15-1.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Saad Kawemba kwa niaba ya ofisa habari, shirikisho lake limeamua kufanya mabadiliko ya uwanja kutokana na CCM Kirumba kutokuwa na ubora stahili.

Kawemba alisema licha ya jitihada zilizofanyika katika kuufanyia marekebisho, bado jaribio la kuwahi muda sahihi kuelekea mechi hiyo haliwezi kuzaa matunda, kutokana na ubovu wa vyumba vya kuvalia na miundombinu.

“Tunaposema vyumba vya kuvalia tunajumuisha vyoo, bafu na sehemu ya kupumzikia wachezaji. Hali katika vyumba vya Kirumba ni mbaya ikiwamo ukosefu wa umeme na aina ya matangazo yasiyohitajika kwa mechi rasmi kutokana na sababu za kiudhamini,” alisema Kawemba.

Aliwataka wakazi wa Kanda ya Ziwa kuwa wavumilivu kutokana na uamuzi huo wa TFF, huku akiwataka kuvuta subira kwani safari ya Tanzanite ni ndefu na kama itafanikiwa kukitoa kikosi cha Amajita, wanaweza kurejea huko kwa mechi zijazo.

“Kama itafanikiwa kuitoa Afrika Kusini, Tanzanite itaingia raundi ya tatu na ya mwisho, wakati huo naamini maboresho Kirumba yatakuwa yamefikia pazuri, hivyo tunaweza kurejea Mwanza kwa mechi ya nyumbani,” alisisitiza Kawemba.

Amajita inayonolewa na Maqsood Chenia, ilitinga raundi ya pili baada ya kuwang’oa vijana wenzao wa Botswana kwa mabao 7-2.

Timu mbili kutoka Afrika zitafuzu kwa fainali za Dunia, zitakazofanyika mwakani kuanzia Agosti 5 hadi 24.

Tuungane hapa Nairobi kesho kushuhudia Kombe la Dunia


HApa Nairobi katika ukumbi wa KICC kutakuwa na kupiga picha na kombe la Dunia kuanzia asubuhi ya Tarehe  28/11/2013 wote mnakaribiswa hapa viwanja vya KICC.

Coming Up



Cecafa Tusker Cup: Zanzibar v South Sudan
Wednesday, 27 Nov 2013 @ 12:30

Cecafa Tusker Cup: Kenya v Ethiopia
Wednesday, 27 Nov 2013 @ 15:00

Absa Premiership: Kaizer Chiefs v Polokwane City
Wednesday, 27 Nov 2013 @ 18:30

Absa Premiership: Maritzburg Utd v Orlando Pirates
Wednesday, 27 Nov 2013 @ 18:30

UCL: CSKA Moscow v Bayern Munich
Wednesday, 27 Nov 2013 @ 18:55

UCL: Bayer Leverkusen v Man Utd
Wednesday, 27 Nov 2013 @ 21:00

UCL: Juventus v FC Copenhagen
Wednesday, 27 Nov 2013 @ 21:40

UCL: Man City v Plzen
Wednesday, 27 Nov 2013 @ 21:40

UCL: Real Madrid v Galatasaray
Wednesday, 27 Nov 2013 @ 21:40

UCL: PSG v Olympiacos
Wednesday, 27 Nov 2013 @ 21:45

Cavaliers v Heat
Thursday, 28 Nov 2013 @ 02:15

Cecafa Tusker Cup: Burundi v Somalia
Thursday, 28 Nov 2013 @ 12:30

Papa Francisko: Atoa waraka wake wa kitume wa kwanza!

Baba Mtakatifu Franciisko Jumanne hii ametoa waraka wake wa Kwanza wa Kitume chini ya Jina Furaha ya Injili “Evangelii Gaudium". Waraka unao zungumzia zaidi juu ya Mada ya utangazaji wa Injili katika Dunia ya nyakati hizi. Waraka huu wenye kurasa 224, unaonyesha muono wa Papa, katika utume wa Kanisa, ambalo milango yake inapaswa kuwa wazi nyakati zote na kwa watu wote.

Katika waraka huu,Papa amezungumzia mada mbalimbali juu ya Uinjilishaji mpya, masuala ya kijamii kama haki na amani, familia na heshima katika viumbe, imani na siasa, uekumeni , majadiliano ya kidini na wajibu wa wanawake na walei katika Kanisa.
Katika maelezo yake, Papa amefanya nukuu kutoka vyanzo vingine vya maelezo, ikiwemo michango ya kazi za Sinodi iliyofanyika Vatican tangu tarehe 7-28Octoba 2012 , juu ya mada:Uinjilishaji Mpya kwa ajili ya kuieneza Imani.

Katika waraka hu, Papa Francisko, anawahimiza Waamini wote kujihusisha na utendaji mpya wa kufikisha habari ya upendo wa Kristu kwa watu wote, huku wakiwa wamejawa na moyo wa furaha, katika kuionyesha njia ya hija ya kanisa katika miaka ijayo. Huu ni wito kwa wabatizwa wote kuupeleka upendo wa Kristu, kwa watu wengine, kama utendaji wa kudumu na ushindi mkuu katika dunia ya leo , ambayo imemezwa na ubinafsi, kukata tamaa na mahangaiko ya kidunia.

Papa anawaalika wasomaji wote kungudua upya asili ya Injili , kupata nafasi mpya na njia mpya katika ubinufu bila ya kumpoteza Yesu katika katika utendaji wote wa kila siku. Katika hili Papa anasema kuna haja ya kuwa na uongofu wa kichungaji na kimisionari , ambao hauwezi kuacha kujali hali zilivyo, na katika kuleta upya kwenye mifumo ya kanisa, ili kuwezesha kanisa, kuwa la kimisonari zaidi. Papa pia anafikiria uongofu wa utawala katika kiti cha Papa , kwa ajili ya kuwezessha kazi zake kuwa na uaminifu zaidi katika maana ambayo Yesu Kritu alipenda iwe hivyo katika hitaji la kuifikisha habari njema kwa mataifa yote. Anatumaini Mabaraza ya Maaskofu yanaweza kutoa mchango thabiti katika ufanikishaji wa moyo wa umoja na mshikamano wa waamini wote wa Kristu, katika kuitangaza Injili, jambo ambalo anasema bado halijatimizwa kikamilifu.

Pia anasema, kuna umuhimu wa kupeleka mamlaka majimboni. Na kwamba juhudi za mabadiliko haya,Kanisa lisiwe na woga, hasa katika kuchunguza upya baadhi ya kanuni, ambazo hazina mahusiano ya moja kwa moja na kiini cha Imani na Injili, hata kama yana mzizi wa historia ya siku nyingi katika kanisa.

Na akitazama nje zaidi ya Kanisa , Papa ameutazama mfumo wa sasa wa kiuchumi akisema kimsingi ndani mwake hakuna haki,ila ndani mwake mmefichika makucha ya soko la dhuluma, ambamo mna uroho wa fedha ,wenye kueneza rushwa na ukwepaji wa kulipa kodi. Pia Papa anakemea mashambulizi dhidi ya uhuru wa dini na mateso mpya yanayo elekezwa zaidi dhidi ya Wakristo. Na Papa pia anakemea ulimwengushaji wa maadili wenye kuzalisha hisia zinazo wachanganya watu na kuwaweka katika za mashaka, hofu na purukushani. Pia waraka unataja umuhimu wa ndoa na mahusiano ya familia imara.

Papa hakuwasahau watu maskini akisema, umaskini mbaya zaidi ni umaskini wa kiroho. Hata hivyo akahimiza hoja ya kuwajali pia wale wanaoteseka kimwili kutokana na kusahaulika pembezoni mwa jamii kw sabau mbalimbali, ikiwemo ukosefu wa makazi, na hasa unao sababishwa na uwepo wa machafuko ya mpigano yenye kuzalisha wakimbizi au utendaji wa kiuchumi unaowaondoa watu wenyeji katika makazi yao. Pia ameyataja makundi ya wazee , wahamiaji, waathirika wa biashara na watoto wasiozaliwa bado, ambao hutupwa mitaani.

Hati mpya ya Papa pia inalenga katika mandhari ya kukuza amani, haki na udugu , kwa njia ya majadiliano na mazungumzo ya kuheshimiana watu wote iwe kijamii au kitamaduni na kidini. Pia amehimiza mahusiano mazuri na wakristo wengine, na Wayahudi na Waislamu wote, kama njia muhimu ya kukuza amani na kupambana na ubabe wa kutumia dini kushambulia wngine au kunyima uhuru wa dhamiri kwa wengine.

Amewataka Wakristo kujiepusha na ujenzi wa chuki za ujumla hasa kuhusu Uislamu ,Katika hili, Papa amehimiza Wakristu kuendelea kuwa wanyenyekevu, hasa na nchi za Kiislamu, wakati wanapodai uhuru kamili wa kidini kwa Wakristo.
Waraka umekamilika na sala kwa Mama Bikira Maria , Mama wa Uinjilishaji , akiutazama mfano wa Maria katika kazi za Kanisa za Uinjilishaji, kwamba, tunapomtafakari Maria , kwa mara nyingine hutuwezesha kuamini katika ufunuo asilia wa asili ya upendo na huruma.

TFF: Yawazuia Kaseja, Dilunga kusajili Yanga

Wakati dirisha dogo la usajili likitarajiwa kufungwa Desemba 15, mwaka huu, Shirikisho la Soka nchini(TFF), limezikumbusha klabu zote kuheshimu kanuni na kuzingatia muda uliowekwa.

Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Boniface Wambura alisema jana kuwa kitendo cha klabu kupeleka mchezaji kwa mkopo katika klabu nyingine hakutoi nafasi ya kusajili mchezaji mpya.

Tamko hilo la TFF lina maana kwamba, Yanga ambayo kwa sasa tayari imeingia mikataba ya kuwasajili kipa Juma Kaseja aliyekuwa huru na kiungo Hassan Dilunga kutoka Ruvu Shooting, haitakubaliwa kumsajili mmoja wa wachezaji hao kwani tayari ilikuwa na wachezaji 29.

"Kama klabu ilisajili wachezaji 30 maana yake ni kuwa, haina nafasi ya kuongeza wachezaji. Kwa upande wa wachezaji wa kigeni (foreign players), tunakumbusha kuwa, kuanzia msimu ujao 2014/2015 watakuwa watatu tu badala ya watano wa sasa," alisema Wambura.

Alisema mpaka jana jioni hakuna klabu hata moja iliyokuwa imeshaingia kwenye mfumo wa TMS kuomba uhamisho wa mchezaji wa kigeni na itakapofika Desemba 15, mwaka huu mfumo huo wa TMS utafungwa.

Poulsen: Kili itaiua Chipolopolo

Kocha Mkuu wa timu ya soka ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars), Kim Poulsen, amesema timu yake mesto wa yosso na wazoefu, iko tayari kuikabili Zambia (Chipolopolo) katika mechi yake ya kwanza ya kuwania ubingwa wa mashindano ya Kombe la Chalenji itakayofanyika kesho kwenye Uwanja wa Nyayo jijini hapa.

Akizungumza jana, Poulsen alisema wachezaji wake wote wako tayari na wamejiandaa kufanya vizuri katika mechi hiyo ya kwanza ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kusonga mbele.

Poulsen alisema mechi dhidi ya Chipolopolo inatarajiwa kuwa ngumu kwa sababu wachezaji wengi wa Zambia ni wauzoefu tofauti na kikosi chake ambacho mwaka huu ni mseto kutokana na kujumuisha yosso wengi aliowaita kwa mara ya kwanza, lakini anaamini watafanya vizuri.

"Tuko tayari, tumejiandaa kwa mashindano na tunaamini tutaanza vyema mechi yetu," alisema Kocha huyo raia wa Denmark.

Aliongeza kuwa, katika kundi lao ambalo linajumuisha timu ya Somalia na Burundi, hakuna mechi nyepesi kwa sababu kila moja imekuja kushindana na si kushiriki.

 Naye mshambuliaji mahiri wa timu hiyo, Mrisho Ngasa, aliliambia blogu hili kuwa wamekuja Nairobi kushindana na watajituma ili kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania Bara.

Ngassa alisema anajua Watanzania wamewatuma kuiwakilisha vyema na hicho ndicho wamepanga kukitekeleza.

"Tunajua jukumu letu na tunamuomba Mungu tufanye vizuri, tuombeeni ili tufanye kile ambacho kocha ametuelekeza," alisema Ngasa.

Kilimanjaro Stars iliyoko Kundi B, ilitua jijini hapa juzi usiku na itacheza mechi yake ya pili Desemba Mosi dhidi ya Somalia huku ikimaliza hatua ya makundi kwa kuivaa Burundi hapo Desemba 4, mwaka huu.

Uganda ndiyo mabingwa watetezi wa mashindano hayo yanayofanyika kila mwaka kwa kushirikisha nchi wanachama wa Cecafa na timu alikwa.