Week Hot newz

Babu kumuona Batarokota atoa chozi!

Pichani juu kutoka kushoto Msananii wa bongo fleva na mziki wa asili ya kitanzania Batarokota akiwa katika picha ya pamoja na Babu yake Abednogo Mishaka Shindika jana Mzumbe Morogoro.

Morogoro: 
Habari kutoka Mjini Morogoro maeneo ya Mzumbe ambapo Msanii wa bongo fleva na mziki wa asili ya Kitanzania Batarokota alifanya ziara ya kwenda Mjini Morogoro kwa ajili ya kumjulia hari Babu yake Abednego Shindika hapo jana.Katika ziara hiyo Batarokota aliongozana na mdogo wake Daniel Renatus Maige walifika maeneo anayoishi Babu yake majira ya saa kumi jioni. Katika hari ya kushangaza Batarokota na Daniel walipo fika eneo ambalo linamilikiwa na Babu yao Abednego Shindika walishangaa kumuona Babu yao alie kuwa mgonjwa sana akiwa anafanya kazi za kuchonga vyuma na Babu huyo alivyo waona wajukuu zake akija alitoa chozi na kutakasimama ili awapokee wajukuuu zake lakini Batarokota alimuwahi na kumupa poa na kushusha maombi dakika 10 ya kumshukuru Mungu kwa kumlejeshea Babu yao afya njema. 
 Pichani juu kutoka kushoto Daniel Renatus Maige na Msananii wa bongo fleva na mziki wa asili ya kitanzania Batarokota akiwa katika picha ya pamoja wakati wakijiandaa kwenda kumtembelea Babu yao Abednego Shindika