Ni
mara ya kwanza wafanyibiashara wametajwa kuwa mafisadi wakubwa Barani.
Shirika hili limeongeza kwamba utumizi mbaya wa mamlaka unasababisha
ongezeko la umasikini, na kuwanyima raia mahitaji muhimu.
Watu
wengi ambao ni masikini wamejipata mara kadhaa wakilazimika kulipa hongo
ikilinganishwa na matajiri, inasema "Transparency International".
Nchi ya Liberia imetajwa kama inayoongoza kwa visa vya ufisadi Afrika. Inafuatwa na Cameroon, Nigeria na Sierra leone.Afrika
mashariki Uganda inaongoza kwa visa vya ufisadi, ikifuatwa na Kenya.
Kusini mwa Afrika Zimbabwe na Zambia zinaongoza katika nchi zenye visa
vingi vya ufisadi.
Botswana, Mauritius na Cape Verde, ndiyo
mataifa pekee ya Afrika ambapo visa vya ufisadi ni vya chini zaidi ikiwa
ni asili mia mbili pekee.
Wafanyibiashara
wakubwa wametakwa kuwa miongoni mwa watu wafisadi zaidi sawa na maafisa
wa polisi Barani Afrika. Hii ni kwa mujibu ya kura ya maoni iliyofanywa
na shirika la kuchunguza ufisadi duniani "Transparency International".
Wafanyibiashara
wakubwa wametakwa kuwa miongoni mwa watu wafisadi zaidi sawa na maafisa
wa polisi Barani Afrika. Hii ni kwa mujibu ya kura ya maoni iliyofanywa
na shirika la kuchunguza ufisadi duniani "Transparency International".
Ni
mara ya kwanza wafanyibiashara wametajwa kuwa mafisadi wakubwa Barani.
Shirika hili limeongeza kwamba utumizi mbaya wa mamlaka unasababisha
ongezeko la umasikini, na kuwanyima raia mahitaji muhimu.
Watu
wengi ambao ni masikini wamejipata mara kadhaa wakilazimika kulipa hongo
ikilinganishwa na matajiri, inasema "Transparency International". Image caption
Raia wengi wa Kenya wamelalamikia visa vya ufisadi serikalini
Nchi ya Liberia imetajwa kama inayoongoza kwa visa vya ufisadi Afrika. Inafuatwa na Cameroon, Nigeria na Sierra leone.
Afrika
mashariki Uganda inaongoza kwa visa vya ufisadi, ikifuatwa na Kenya.
Kusini mwa Afrika Zimbabwe na Zambia zinaongoza katika nchi zenye visa
vingi vya ufisadi.
Botswana, Mauritius na Cape Verde, ndiyo
mataifa pekee ya Afrika ambapo visa vya ufisadi ni vya chini zaidi ikiwa
ni asili mia mbili pekee.
St. Bibiana, Virgin and Martyr
(Feast day - December 2nd) Other than the name, nothing is known for
certain about this saint. However, we have the following account from a
later tradition.
In the year 363, Julian the Apostate made Apronianus Governor of Rome. St. Bibiana suffered in the persecution
started by him. She was the daughter of Christians, Flavian, a Roman
knight, and Dafrosa, his wife. Flavian was tortured and sent into exile,
where he died of his wounds. Dafrosa was beheaded, and their two
daughters, Bibiana and Demetria, were stripped of their possessions and
left to suffer poverty. However, they remained in their house, spending
their time in fasting and prayer.
Apronianus,
seeing that hunger and want had no effect upon them, summoned them.
Demetria, after confessing her Faith, fell dead at the feet of the
tyrant. St. Bibiana was reserved for greater sufferings. She was placed in the hands of a wicked woman called Rufina, who in vain endeavored to seduce her. She used blows as well as persuasion, but the Christian virgin remained faithful.
Enraged
at the constancy of this saintly virgin, Apronianus ordered her to be
tied to a pillar and beaten with scourges, laden with lead plummets,
until she expired. The saint endured the torments with joy, and died
under the blows inflicted by the hands of the executioner.
Hata katika umaskini wao, waafrika bado ni watu wenye furaha! - OSS_ROM
Baba
Mtakatifu Francisko amerejea mjini Vatican baada ya kuhitimisha hija
yake ya kitume Barani Afrika alikotembelea Kenya, Uganda na Jamhuri ya
Watu wa Afrika ya Kati kuanzia tarehe 25 hadi 30 Novemba 2015. Huko
amepata nafasi ya kujionea na kusikiliza kilio cha Familia ya Mungu
kuhusiana na umaskini, ukosefu wa haki msingi na mahitaji muhimu ya
binadamu. Ameguswa na kilio cha vijana wanaotaka saratani ya rushwa na
vitendo vya kigaidi, uharibifu wa mazingira ipewe tiba muafaka; mambo
yote haya yanahatarisha utu na heshima ya binadamu.
Baba Mtakatifu akiwa njiani amepata
fursa ya kujibu baadhi ya maswali yaliyoulizwa na waandishi wa habari
waliokuwa kwenye msafara wake. Anasema, pale ambapo sera za uchumi na
maendeleo zinajikita katika ubinafsi, utajiri na mali, hapo utu na
heshima ya binadamu viko rehani. Inasikitisha kuona kwamba, kuna watu
wachache sana wanaomiliki utajiri wa dunia wakati ambapo kuna kundi
kubwa la watu bado linaendelea kuogelea katika dimbwi la umaskini na
magonjwa. Baba Mtakatifu anasema, amesikitishwa
sana na mahangaiko ya wananchi wa kitongoji cha Kangemi, Kenya;
ameguswa na mateso ya watoto waliolazwa kwenye Hospitali ya Watoto
Bangui. Amejionea jinsi watoto wanavyoteseka kutokana na utapiamlo
mkubwa, kwa kukosa dawa na vifaa tiba. Yote haya ni kwa sababu watu
wanapenda kuabudu fedha na mali kuliko utu na heshima ya binadamu.
Magonjwa, umaskini na maafa yataendelea kuwaandama wanadamu ikiwa kama
binadamu mwenyewe hataweza kufanya toba na kumwongokea Mungu. Matajiri
wawe na ujasiri wa kugawana rasilimali ya dunia na maskini, ili waweze
wao pia kufurahia Injili ya maisha! Baba Mtakatifu anakiri kwamba,
ameguswa kwa namna ya pekee na ukarimu, furaha na maisha ya Familia ya
Mungu Barani Afrika hata katika umaskini wao, bado wanaweza kufurahia
maisha. Wameonesha ukarimu wa ajabu kwa kujitokeza kwa wingi kumpokea na
kumsikiliza. Kenya inaonekana kuwa na maendeleo; Uganda bado inajikita
katika mashuhuda wa imani; huu ndio utambulisho wao unaowapatia ujasiri
wa kushuhudia imani inayomwilishwa katika matendo! Katika
Jamhuri ya Watu wa Afrika ya Kati, Baba Mtakatifu anakaza kusema, wao
wana kiu ya amani, upatanisho na msamaha wa kweli; udugu, umoja na
mshikamano wa kitaifa kwa kutambua kwamba wao ni ndugu wamoja! Waamini
wanapaswa kuwa wajenzi wa haki, amani na maridhiano kati ya watu na wala
si wachochezi wa kinzani na misigano mambo ambayo yanasigana na imani
wanayoiungama. Serikali ya mpito Jamhuri ya Watu wa Afrika ya Kati
isaidie kuwapatia wananchi: haki, amani, msamaha na upatanisho wa
kitaifa. Bara la Afrika lina utajiri na
raslimali nyingi; lina tunu na tamaduni zinazopaswa kuendelezwa. Kwa
bahati mbaya Bara la Afrika linaonekana na wengi kuwa ni uwanja wa fujo
pasi na usalama. Baba Mtakatifu anakaza kusema, Bara la Afrika limekuwa
kama kichwa cha mwendawazimu, watu wengi wanalinyonya kiasi kwamba
limekuwa ni shahidi wa unyonyaji pasi na huruma. Anasema analipenda Bara
la Afrika na kwamba, kuna haja ya kushikamana ili kuliendeleza Bara la
Afrika badala ya kuendelea kunyanyaswa na wenye nguvu wachache duniani! Baba Mtakatifu anawataka waandishi wa
habari kutekeleza dhamana na wajibu wao kwa kuzingatia kanuni, maadili
na sheria kwani hakuna uhuru pasi na mipaka hata katika mapambano dhidi
ya rushwa na ufisadi ambao umeenea sehemu mbali mbali za dunia hata
mjini Vatican. Vyombo vya habari viwe na ujasiri wa kufunua maovu na
vyombo vya sheria vitekeleze wajibu wake barabara.Waandishi
wa habari waseme ukweli pasi na kuuvuruga kwa ajili ya mafao yao
binafsi; waoneshe weledi katika kazi zao kwa kujikita katika ukweli
pamoja na kuheshimu sifa ya mtu! Waandishi wa habari wawe na ujasiri wa
kuomba msamaha pale wanapokosea na kukiuka kanuni maadili za kazi. Katika mapambano dhidi ya vitendo vya
kigaidi na misimamo mikali ya kidini, viongozi wa kidini wanapaswa
kutekeleza dhamana na wito wao kwa kutambua kwamba, wao ni vyombo na
wajenzi wa: umoja, haki, amani,upatanisho na maridhiano. Misimamo mikali
ya kidini ni saratani ambayo iko katika dini zote na inakwenda kinyume
kabisa cha mafundisho msingi ya kidini. Hapa kuna watu wanatumia
misimamo mikali ya kidini kwa ajili ya mafao ya binafsi, ili kujipatia
fedha na utajiri wa haraka haraka. Baba Mtakatifu Francisko anakiri
kwamba, kumekuwepo na tatizo la kumshirikisha Monsinyo Vallejo Balda
pamoja na Francesca Immaculata Chaouqui katika Tume ya Marekebisho ya
masuala ya uchumi na fedha Vatican, ingawa baada ya kumaliza kazi zao
waliondoka na kwamba, watuhumiwa hawa hawakumnyima usingizi hata kidogo
kwani kile kilichochapishwa kwenye vitabu kinaonesha kazi ya mageuzi
iliyofanywa. Rushwa anakaza kusema Baba Mtakatifu ni adui wa haki.
Mapambano dhidi ya rushwa mjini Vatican ni mchakato ulioanzishwa na
Kardinali Joseph Ratzinger wakati alipotoa tafakari ya Njia ya Msalaba,
siku chache kabla ya kifo cha Papa Yohane Paulo II, akachaguliwa na
Makardinali kuwa Khalifa wa Mtakatifu Petro ili kuendeleza mchakato wa
mageuzi. Kumbe, wizi wa nyaraka za siri kutoka
Vatican ni tendo la jinai na kwamba, Baba Mtakatifu angependa kesi hii
iwe imekamilika na kutolewa hukumu kabla ya kuanza maadhimisho ya Mwaka
Mtakatifu wa Jubilei kuu ya huruma ya Mungu, hapo tarehe 8 Desemba 2015,
pengine jambo hili halitawezekana anasikitika kusema Baba Mtakatifu
Francisko na kwamba kwa kushirikiana na Makardinali wataendelea kufanya
mageuzi kadiri ya maelekezo yaliyotolewa na Makardinali katika mikutano
yao kabla ya uchaguzi wa Khalifa wa Mtakatifu Petro kunako mwaka 2013. Kuhusu Ugonjwa wa Ukimwi ambao bado
unaendelea kusababisha vifo vingi miongoni mwa vijana wa kizazi kipya,
Baba Mtakatifu anakaza kusema, Kanisa litaendelea kuhimiza kanuni
maadili na utu wema; kwa kusimama kidete kutangaza na kushuhudia Injili
ya uhai dhidi ya utamaduni wa kifo. Matumizi ya kondomu si dawa ya
kuzuia matatizo na majanga yanayoliandama Bara la Afrika. Kuna ukosefu
wa haki msingi za binadamu; uharibifu mkubwa wa mazingira; baa la njaa
na utapiamlo; ukosefu wa maji safi na salama; bado kuna biashara kubwa
ya silaha, unyonyaji na udhalilishaji wa binadamu; watu hawana makazi
bora na salama. Matatizo na changamoto hizi zikipewa ufumbuzi muafaka
hata Ukimwi utatoweka. Baba Mtakatifu anasema aliwaahidia
Mapatriaki wa Armenia kushiriki katika maadhimisho ya Jubilei ya miaka
101 ya mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini Armenia. Lakini ikumbukwe
kwamba, vita ni kiwanda kinachozalisha silaha na utajiri kwa watu
wachache, hata katika nchi zile ambazo uchumi wake unachechemea, bado
utakuta wananunua silaha za mapambano! Vita
ni dhambi dhidi ya ubinadamu na madhara yake ni makubwa licha ya vifo
na maafa; vita inasababisha pia biashara haramu ya binadamu,
udhalilishaji wa utu na heshima ya binadamu bila kusahau unyonyaji. Kuna
haja kwa Jumuiya ya Kimataifa kusimama kidete ili kuhakikisha kwamba,
vita inasitishwa ili amani iweze kutawala katika akili na mioyo ya watu.
Mwenyezi Mungu ndiye asili ya amani changamoto kwa watu wote kuwa ni
vyombo na wajenzi wa amani. Baba Mtakatifu Francisko akizungumzia
kuhusu mazingira anakaza kusema, viongozi wa Jumuiya ya Kimataifa
wanaoshiriki katiki katika mkutano wa athari za mabadiliko ya tabianchi,
Cop21 huko Paris, Ufaransa wanao wajibu mkubwa kuhakikisha kwamba
kunakuwepo na udhibiti wa athari za mabadiliko ya tabianchi vinginevyo,
dunia itaendelea kushuhudia maafa makubwa kwa watu na mali zao. Baba
Mtakatifu anasema, ana imani na matumaini kwa viongozi wa Jumuiya ya
Kimataifa kwamba, wataweza kutoa majibu muafaka kuhusiana na athari za
mabadiliko ya tabianchi. Dini ya Kiislam ina tunu msingi za
maisha ya kiroho zinazoweza kutumika katika mchakato wa majadiliano ya
kidini katika ujenzi wa udugu na urafiki; maisha ya kiroho yanayojika
katika mambo msingi badala ya kushabikia misimamo mikali ya kidini
ambayo inapatikana katika dini zote. Hii ni changamoto kwa waamini
kutubu, kuongoka na kuomba msamaha, ili dunia iweze kuwa ni mahali
pazuri zaidi pa kuishi. Baba Mtakatifu anasema katika umri
wake, safari ndefu ni taabu na shida anatarajia kwenda nchini Mexico ili
kutoa heshima yake kwa Bikira Maria pamoja na kutembelea baadhi ya
maeneo ambayo hayajawahi kutembelewa na Mapapa. Kunako mwaka 2017 tayari
amekwisha kupata mwaliko wa kutembelea baadhi ya nchi za Amerika ya
Kusini. Mwishoni, Baba Mtakatifu amewashukuru waandishi wa habari wote
waliokuwa kwenye msafara wake Barani Afrika kwa kazi kubwa waliyoifanya
ili kuwahabarisha watu. Amewashukuru kwa maswali yao na kwamba,
ameyajibu kadiri anavyofahamu pale ambapo haja jibu amewaambia wazi wazi
na wala si sehemu ya utamaduni wake kuficha mambo!