Mwili
wa Marehemu Nelson Mandela, Siku ya Jumatano tarehe 11 Desemba 2013
umewasili mjini Pretoria ambako utakaa kwa muda wa siku tatu, ili kutoa
nafasi kwa wananchi wa Afrika ya Kusini kutoka heshima zao za mwisho.
Magari ya Polisi yaliusindikiza Mwili wa Tata Madiba kutoka kwenye
Hospitali ya Kijeshi.

Desmond Tutu
Wezi wamevunja na kuingia nyumbani kwa Askofu mstaafu Desmond Tutu
Polisi wamesema wizi huo ulifanyika wakati bwana Tutu akiwa katika ibada ya Nelson Mandela Mjini Johannesberg.Aidha wameelezea kuwa uvamizi ulifanyika nyumbani kwake mjini Cape Town Ahamisi jioni baada ya kutoa hotuba katika ibada ya Mandela siku hiyo.
Ibada hiyo ilifanyika katika uwanja wa FNB mtaani Soweto.
Wizi na uvamizi wa nyumba za watu ni jambo la kawaida nchini Afrika Kusini ambako visa vya uhalifu viko juu sana.