Week Hot newz

Mungu awalaze pema waliofariki Hijja Makka

Na Paskal Linda

KUNA taarifa za kusikitisha kuwa mahujaji watano kutoka Tanzania ni  miongoni mwa waliofariki katika tukio la mkanyagano kwenye Mji  Mtakatifu wa Makka, nchini Saudi Arabia.
 
Kwa ujumla, watu 717 wameripotiwa kufa na wengine zaidi ya 800  kujeruhiwa katika tukio hilo.
 
Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa  Kimataifa jjuzi ilieleza kuwa Watanzania hao walifariki wakati  wakiendelea na ibada ya Hijja kwenye eneo la Mina, ndani ya Mji  Mtakatifu wa Makka.
 
Hakika, huu ni msiba mkubwa. Mimi Paskal Linda  naungana na Watanzania wengine  kuwapa pole wafiwa na pia kuwatakia kheri wote waliojeruhiwa ili  wapate nafuu haraka.
 
Ni imani yangu kuwa serikali yetu, kwa kushirikiana na  Saudi Arabia,  itaendelea kufanya kila linalowezekana ili taarifa kamili ziendelee  kupatikana kuhusiana hatima ya mahujaji wetu. Taarifa zilizopo ni  kwamba mwaka huu, Watanzania takriban 2,700 wamekwenda kutekeleza  ibada hiyo muhimu kwa kila Muislamu mwenye uwezo. Mbali na kwenda  kuhiji Makka, nguzo nyingine kati ya tano za Uislamu ni kutoa  shahada, kusimamisha swala, kutoa zaka na kufunga (swaumu) Ramadhani.
 
Sisi tunaamini kuwa muhimu zaidi kwa sasa ni kwa kila mmoja kuendelea  kuwaombea mahujaji wetu waliosalimika ili mwishowe warejee nchini  wakiwa bukheri wa afya.
 
Aidha, ni muhimu pia kuendelea kumuomba Mwenyezi Mungu ili awajaalie  pepo yenye daraja ya juu mahujaji wetu waliopatwa na umauti, hasa kwa  kutambua kuwa kilichowapeleka Makka siyo kitu kingine bali ni  kujinyenyekeza mbele za Allah (Mwenye Mungu) ili mwishowe wapate  radhi zake.
 
Katika kipindi hiki, ni imani yetu kuwa ndugu, jamaa na marafiki wa  marehemu watajitahidi kuwa na subira kadiri wawezavyo. Ni kwa sababu,  kwa mujibu wa mafundisho, kila nafsi itaonja umauti. Na hili  lililotokea ni sehemu ya mtihani ambao siri ya kufaulu kwake  kwategemea kiwango cha subira kwa kila mmoja wao. 
    
Pamoja na yote, tunaamini kuwa baada ya shughuli za uokoaji na  mazishi kukamilika, serikali ya Saudi Arabia itahakikisha kuwa  uchunguzi wa kina unafanyika ili mwishowe kubaini chanzo cha  mkanyagano na kuchukua hatua sahihi za kuzuia majanga ya aina hii.
 
Kinachotakiwa kuangaliwa na waandaaji ni taratibu za kutoa fursa kwa  kila hujaji kutekeleza ibada ya Hijja akiwa salama. Rekodi  zinaonyesha kuwa vifo vya aina hii vimewahi pia kutokea mara kadhaa  hapo kabla katika tukio hilo linalokutanisha watu wengi zaidi kwa  wakati mmoja duniani, huku mwaka huu likihusisha mahujaji takriban  milioni mbili. 
 
Kwa mfano, mwaka 1990 walikufa mahujaji 1,426, mwaka 1994 (watu 270)  na pia mwaka 2006 walikufa watu 360. Hali hii inapaswa kuzuiwa kwa  kupitia upya taratibu za kuwezesha waumini kutekeleza ibada hii  muhimu kwa kila Muislamu mwenye uwezo.
 
Mungu awalaze pema peponi mahujaji wote waliotangulia mbele ya haki, AMINA.

Daily Reading for Monday, September 28th, 2015


Reading 1, Zechariah 8:1-8


Responsorial Psalm, Psalms 102:16-18, 19-21, 29, 22-23

16 when Yahweh builds Zion anew, he will be seen in his glory;
17 he will turn to hear the prayer of the destitute, and will not treat their prayer with scorn.
18 This shall be put on record for a future generation, and a people yet to be born shall praise God:
19 Yahweh has leaned down from the heights of his sanctuary, has looked down from heaven to earth,
20 to listen to the sighing of the captive, and set free those condemned to death,
21 to proclaim the name of Yahweh in Zion, his praise in Jerusalem;
22 nations will gather together, and kingdoms to worship Yahweh.
23 In my journeying my strength has failed on the way;

Gospel, Luke 9:46-50

46 An argument started between them about which of them was the greatest.
47 Jesus knew what thoughts were going through their minds, and he took a little child whom he set by his side
48 and then he said to them, 'Anyone who welcomes this little child in my name welcomes me; and anyone who welcomes me, welcomes the one who sent me. The least among you all is the one who is the greatest.'
49 John spoke up. 'Master,' he said, 'we saw someone driving out devils in your name, and because he is not with us we tried to stop him.'
50 But Jesus said to him, 'You must not stop him: anyone who is not against you is for you.'

St. Lorenzo Ruiz

Short Cuts
Image of St. Lorenzo Ruiz

Facts

Feastday: September 28
Beatified By: Pope John Paul II
Canonized By: Pope John Paul II

Lorenzo Ruiz is the first Filipino saint. He is also the first Filipino martyred for the Christian Faith. Lorenzo Ruiz was a layman, married, and had two sons and a daughter. Born in Binondo, Manila, about 1600's, he was educated in the school of the Dominicans there. He served as an altar boy and later was a helper and clerk-sacristan in the church of Binondo. He was a member of the Confraternity of the Rosary. He made his living probably as a calligrapher, one who renders documents in beautiful penmanship for private or official use. To be sure, that work denoted an accomplished and educated person, especially at a time when many an illustrious personage were far from excelling in this art. An adverse event made him leave the Philippines in 1636. When he was in his late twenties or early thirties, he became involved or was accused of being involved in a criminal case, the circumstances of which are far from clear. Whether he was involved or not, one thing was clear, he was afraid that, as a consequence of a trial or mistrial, he might be given a death sentence. Upon landing in Japan where Christians were being persecuted, he was arrested and imprisoned together with his companions. He underwent inhuman tortures and valiantly confessed his Christian Faith. Refusing to renounce his Faith, he told his executioner that he was ready to die for God and give himself for many thousands of lives if he had them. On September 27, 1637, he was hung from a gallows by his feet, his body falling into a pit. After two days of agony, he died of bleeding and suffocation. His body was cremated and the ashes thrown into the sea. He and fifteen companions, martyred in the same persecution, were beatified by Pope John Paul II in Manila on February 18, 1981 and elevated to full honors of the altar by canonization on October 18, 1987 in Rome. Their feast day is on September 28th.

Papa awashukuru watawa wa Marekani


Papa akisalimiana na Masista wa Shirika la Mtakatifu Clara - AP

BABA mtakatifu Francisco Alhamisi akiongoza Ibada ya masifu ya Jioni katika Kanisa Kuu la kale la Mtakatifu Patrick, la Mjini New York, alionyesha kutambua kwamba, kanisa hilo ni matunda ya kazi ngumu ya watu wengi  wake kwa waume, waliyoyatolea maisha yao mhanga bila kujibakiza katika utumishi wa kanisa.  Na hivyo ameitaja kuwa ni  ishara nzuri ya kazi ya wahenga,  makuhani , watawa na walei aminifu wa Marekani,  waliosaidia kujenga Kanisa nchini Marekani.
Papa alitazama kwa kina, jukumu lao la msingi katika ujenzi wa jamii ya Marekani, na hivyo akatoa shukurani zake nyingi kwa  makuhani na watawa  ambao  hasa wamejikitika katika mipango ya  elimu na lishe katika taifa la Marekani. Alieleza na kutoa mfano wa mwanzilishi wa kwanza wa Shule Katoliki huru ya wasichana nchini Marekani, Mtakatifu  Elizabeth Ann Seton na Mtakatifu  John Neumann, mwanzilishi wa kwanza wa mfumo wa elimu Katoliki Marekani , akisema kwamba watu wengi kulipwa gharama za kafara ya ajabu na alifanya hivyo kwa kishujaa upendo.

Lakini pia hakuogopa kutaja moja kwa moja kasoro zilizo chafua sura nzuri ya Kanisa nchini Marekani,  kashfa  ya ngono kwa watoto, aibu iliyoletwa na watumishi wabovu wa Kanisa . Papa Francisko,  alikubali mateso ya wake kwa waume, na wale waliokubali kuibeba aibu ya unyama huu uliodhalilisha  ndugu hawa wanyonge  katika  Kanisa na kuwaweka katika mazingira magumu zaidi ... Papa amesema anatolea sala na faraja zake katika kwa wakati huu wa maumivu na uchungu wa moyo.
Na aliwarejea tena  Mapadre na watawa wa Marekani , akiwahimiza n akuwataka wawe watumishi wema, watumikie kwa uaminifu, furaha na kuridhika katika wito wao. Wafanya kazi kwa bidii na kuyaishi maisha ya kujinyima  na uaminifu kwa mujibu wa karama za waanzilishi wa jumuiya na mashirika yao kama  njia ya upendeleo katika kutoa jibu kwa Upendo wake Mkuu Yeye aliyewaita  katika kulitumikia Kanisa.
Kwa namna ya pekee, Papa aliendelea kutambua na kuonyesha heshima yake na shukrani kwa watawa wa kike nchini Marekani akihoji, bila wao utendaji wa Kanisa ungekuwaje hasa nchini Marekani. Alisifu kwamba, Wanawake wana nguvu, na kwa ujasiri huo, huwaweka mstari wa mbele katika kuitangaza Injili .
Alimalizia na shukurani kwa Watawa, masista na wanawake wote walioyatolea maisha yao katika kuifikisha habari njema katika kila kona ya taifa la Marekani na kwingineko duniani.  "Asante Sana ", na “ninawapenda wote”.

Baada ya Marekani Papa kuitembelea Afrika Mashariki na Kati


TOLEO 39.indd
Rais Kenyata asema ni Papa atakayeiunganisha Kenya kuwa kitu kimoja


Na Paskal Linda -Nairobi, Kenya


NCHI za Kenya  na Uganda zimeeleza shauku ya kumuona Papa Fransisko. Akizungumza na batarokota.blogspot.com, Mratibu wa Mawasiliano Baraza la Maaskofu Kenya (KCCB) David Omwoyo amesema kuwa, wananchi wa Kenya wanashauku ya kumuona Papa Fransisko kwani hiyo ni ziara ya kihistoria kwa nchi hiyo.
“Maandalzi kwa upande wa Kanisa yamekamilika na upande wa serikali imejiandaa vyema kwani hata serikali imetuma ujumbe kwamba imejipanga kumpokea Papa Fransisko ambaye licha tu ya kuwa kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani ni Rais wa nchi ya Vatikani,” ameeleza Omwoyo.
Aidha ameeleza kuwa, licha ya Papa kuitembelea Kenya ataitembelea pia nchi ya Uganda hivyo ugeni huo unageuka kuwa wa nchi za Afrika Mashariki.

Aidha serikali ya Kenya ilituma ujumbe kwenye ofisi za Mawasiliano KCCB ikieleza kuwa, serikali ya Kenya inayoongozwa na Rais Uhuru Kenyata iko makini kumpokea Papa Fransisko ambaye wana matumaini kwamba ataleta hamasa ya umoja na mshikamano baina ya wakenya.
“Baba Mtakatifu anakuja kututembelea kama kondoo zake, kuimarisha imani yetu na kututia moyo wa imani katika kutekeleza majukumu yetu kwa jirani na kujitoa sadaka kwa ajili yaw engine,” umeeleza ujumbe huo.
Omoyo amesema, Papa akiwa Kenya kwa siku hizo tatu, atafanya mazungumzo binafsi na Rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyata, atakutana pia na viongozi wa serikali ya Kenya na Maafisa Mazingira wa Umoja wa Mataifa na kuhutubia wajumbe wa kidiplomasia nchini humo.
“Papa atakutana pia na viongozi wa dini mbalimbali wakiwemo wakristo, waislamu, Hindu na viongozi wa jadi, vijana na kuongoza Ibada ya Misa Takatifu ambapo atahutubia taifa la Kenya.
Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Katoliki Uganda Askofu John Baptist Odama ameeleza kuwa, Kanisa nchini Uganda limejiandaa kwa ujio huo Mtakatifu.“Akiwa nchini Uganda, Papa ataungana na waamini kusherehekea Yubilei ya Dhahabu ya kutangazwa watakatifu Mashahidi wa Uganda 22.”

Baraza la Maaskofu Kenya laweka mikakati ya ujio huo.
Kamati ndogo ya Tume ya Mawasiliano na Matangazo ya Baraza la Maaskofu Katoliki Kenya, imetoa baadhi ya mikakati mbinu, kwa ajili ya maandalizi ya ziara ya Papa Francisko nchini Kenya, mwezi Novemba mwaka huu.
Mratibu wa Mawasiliano wa KCCB, David Omwoyo amesema kuwa, tovuti maalum kwa ajili ya ziara ya Papa itazinduliwa katika siku chache zijazo. Na pia hivi karibuni, nembo ya ziara ya Papa itazinduliwa hivi karibuni.
Nembo hiyo ina alama 4 muhimu zinaashiria mada mbiu ya ziara: “Simama imara katika Imani … Usiogope.” Vitu hivyo vinne ni Njiwa kama alama ya amani, moto katika nafasi ya Roho Mtakatifu, ramani ya Kenya na Msalaba ambayo ni ishara ya Kanisa.
Na kwamba, kwa ajili ya kuwaandaa watu , katika kipindi hiki cha kusubiri ujio wa Papa, Kamati ndogo ya Mawasiliano imeunda mpango mpya wa utendaji kwa miradi maalum, inayolenga kufanikishaji wa ziara ya Papa kiroho na kijamii.
Miradi inayoendeshwa na Kanisa Katoliki Kenya ambayo itatagazwa kupitia vituo vya Televisheni. Aidha, kutakuwa na mengi yatakayotangazwa na vyombo vya habari kwa wakati huu.
Taarifa zote zitakuwa zinapatikana katika tovuti mpya itakayozinduliwa hivi karibuni, ikiwa wazi kwa mtu yeyote ambaye anayetaka kupata habarii za ujio wa Papa Kenya. 

Papa Fransisko anatazamia kuitembelea Afrika ambapo atatembelea nchi ya Kenya Novemba 25 hadi 27, Uganda Novemba 27 hadi 29 na Jamhuri ya Afrika ya Kati Novemba 29 hadi 30 Mwaka huu.

Evening Prayer to God the Father

O eternal God and Ruler of all creation, You have allowed me to reach this hour. Forgive the sins I have committed this day by word, deed or thought. Purify me, O Lord, from every spiritual and physical stain. Grant that I may rise from this sleep to glorify You by my deeds throughout my entire lifetime, and that I be victorious over every spiritual and physical enemy. Deliver me, O Lord, from all vain thoughts and from evil desires, for yours is the kingdom, and the power, and the glory, Father, Son, and Holy Spirit, now and ever, and forever. Amen. (By Saint Macarius)

Daily Reading for Sunday, September 27th, 2015


Reading 1, Numbers 11:25-29

25 Yahweh descended in the cloud. He spoke to him and took some of the spirit that was on him and put it on the seventy elders. When the spirit came on them they prophesied -- but only once.
26 Two men had stayed back in the camp; one was called Eldad and the other Medad. The spirit came down on them; though they had not gone to the Tent, their names were enrolled among the rest. These began to prophesy in the camp.
27 A young man ran to tell Moses this. 'Look,' he said, 'Eldad and Medad are prophesying in the camp.'
28 Joshua son of Nun, who had served Moses since he was a boy, spoke up and said, 'My lord Moses, stop them!'
29 Moses replied, 'Are you jealous on my account? If only all Yahweh's people were prophets, and Yahweh had given them his spirit!'

Responsorial Psalm, Psalms 19:8, 10, 12-13, 14

8 The precepts of Yahweh are honest, joy for the heart; the commandment of Yahweh is pure, light for the eyes.
10 more desirable than gold, even than the finest gold; his words are sweeter than honey, that drips from the comb.
12 But who can detect his own failings? Wash away my hidden faults.
13 And from pride preserve your servant, never let it be my master. So shall I be above reproach, free from grave sin.
14 May the words of my mouth always find favour, and the whispering of my heart, in your presence, Yahweh, my rock, my redeemer.

Gospel, Mark 9:38-43, 45, 47-48

38 John said to him, 'Master, we saw someone who is not one of us driving out devils in your name, and because he was not one of us we tried to stop him.'
39 But Jesus said, 'You must not stop him; no one who works a miracle in my name could soon afterwards speak evil of me.
40 Anyone who is not against us is for us.
41 'If anyone gives you a cup of water to drink because you belong to Christ, then in truth I tell you, he will most certainly not lose his reward.
42 'But anyone who is the downfall of one of these little ones who have faith, would be better thrown into the sea with a great millstone hung round his neck.
43 And if your hand should be your downfall, cut it off; it is better for you to enter into life crippled, than to have two hands and go to hell, into the fire that can never be put out.
45 And if your foot should be your downfall, cut it off; it is better for you enter into life lame, than to have two feet and be thrown into hell.
47 And if your eye should be your downfall, tear it out; it is better for you to enter into the kingdom of God with one eye, than to have two eyes and be thrown into hell
48 where their worm will never die nor their fire be put out.

Reading 2, James 5:1-6

1 Well now, you rich! Lament, weep for the miseries that are coming to you.
2 Your wealth is rotting, your clothes are all moth-eaten.
3 All your gold and your silver are corroding away, and the same corrosion will be a witness against you and eat into your body. It is like a fire which you have stored up for the final days.
4 Can you hear crying out against you the wages which you kept back from the labourers mowing your fields? The cries of the reapers have reached the ears of the Lord Sabaoth.
5 On earth you have had a life of comfort and luxury; in the time of slaughter you went on eating to your heart's content.
6 It was you who condemned the upright and killed them; they offered you no resistance.

St. Michael the Archangel

Short Cuts
Image of St. Michael the Archangel

Facts

Feastday: September 29
Patron of grocers, mariners, paratroopers, police, and sickness

St. Michael the Archangel - Feast day - September 29th The name Michael signifies "Who is like to God?" and was the warcry of the good angels in the battle fought in heaven against satan and his followers. Holy Scripture describes St. Michael as "one of the chief princes," and leader of the forces of heaven in their triumph over the powers of hell. He has been especially honored and invoked as patron and protector by the Church from the time of the Apostles.
Although he is always called "the Archangel," the Greek Fathers and many others place him over all the angels - as Prince of the Seraphim. St. Michael is the patron of grocers, mariners, paratroopers, police and sickness.

Utendaji wa mtu pia huonyesha tabia ya mtu mwenyewe alivyo

Mapema Ijumaa hii 25 Septemba 2015, Baba Mtakatifu alitembelea Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa yaliyoko mjini New York, na kuwahutubia wafanyakazi wote wa Ofisi hizo za Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa. Katika hotuba yake fupi, Papa aliwashukuru kwa dhati na kuonyesha furaha yake kuwa mahali hapo. Aliwatia nguvu akiwataja kwamba wote wake kwa waume, wao ni uti wa mgongo wa chombo hiki muhimu cha Kimataifa.
Baba Mtakatifu Francisko akihutubia wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa mjini New York 25.09.2015 -
Papa alitoa shukurani zake kwa wafanyakazi wote tangu kwa maofisa wa ngazi za juu watalaam hadi kwa wahudumu wa kawaida akisema, kazi zao za kila siku ni muhimu katika kuwezesha kazi za mahusiano ya  kidiplomasia, kiutamaduni, kiuchumi na kisiasa, katika juhudi za  Umoja wa Mataifa, ambazo ni muhimu sana kwa ajili ya kukutanisha matumaini na matarajio ya watu wote wanaounda familia ya binadamu. Na alitambua juhudi na uzoefu wa wafanayakazi hao  kama Maafisa na makatibu, wahariri na wakalimani, wahudumu na wapishi, mafundi wa ukarabati na pia kama maafisa usalama.
Papa aliwashukuru wote kwa moyo wa dhati, kwa kila jambo wanalolifanya kwa manufaa ya wote na hasa kwa majitoleo yao  ambayo si tu huchangia katika ufanikishaji wa kazi za  Umoja wa Mataifa, lakini pia zenye kuwa na maana kubwa, pia  kwao wenyewe binafsi.  Papa alisema jinsi mtu anavyofanya kazi zake huonyesha pia heshima ya mtu mwenyewe alivyo.
Na kwamba wengi wao wametoka katika nchi mbalimbali duniani kote. Na hivyo wanakuwa mfano wa jinsi watu mbalibmali wanavyoweza kuungana na kuwa kitu kimoja katika utumishi kwa manufaa ya wote, na hasa kwa jinsi wanavyoonyesha ustawi wa watoto kupitia mipango mbalimbali ya elimu na lishe. Na pia  katika kujali mustakabali wa dunia na vizazi vijavyo.
Papa alieleza na kutoa ombi kwa kila mmoja wao, akimtaka bila kujali hadhi yake, wajenge umoja na mshikamano, wakihudumiana  mmoja kwa mwingine. Kufanya kazi zao kwa ukaribu zaidi na zaidi katika hali za kuheshimiana  na umoja kati yao ili shirika hili liwe  mfano wa familia ya binadamu , yenye kuishi katika hali ya mapatano na maelewano si tu kwa ajili  ya amani lakini katika amani , kufanya kazi si tu kwa ajili ya haki lakini katika roho ya haki.
Papa alieleza na kuwahakikishia kwamba kila mmoja wao yumo ndani ya moyo wake .  Na kwamba atatolea sala zake kwa ajili yao na familia zao na akawaomba wao pia wamkumbuke katika sala zao .Na kama kuna wasioamini basi amewaomba wamtakie yaliyo mema. "Mungu awabariki wote. Asante" alimalizia Papa Francisko na kupigiwa makofi mengi .

Ujumbe wa Papa Francisco kwa New York :” Mungu yu hai katika miji yetu”


Ijumaa, kama sehemu ya ratiba yake katika kulitembelea jiji la New York, 

Na Paskal Linda- New York.

 BABA Mtakatifu aliongoza Ibada ya Misa katika Bustani ya Madison , ibada iliyohudhuriwa na maelfu ya wakazi wa jiji la New York, wakiwemo Maaskofu, Mapadre Watawa wakiongozwa na Askofu Mkuu Kardinali Timothy Michael Dolan wa Jimbo Kuu la New.
Papa Francisko akipeana Amani na Kardinali Dolan, wakati wa Ibada ya misa katika bustani ya Madson
Papa katika hotuba yake aliyoitoa katika lugha ya kihispania na kutafasiliwa kwa Kiingereza, pia aliwakumbusha  kutosahau kuwahudumia watu maskini na wahitaji wa mji huo.
Papa Francisco aliendelea kuzungumzia wajibu waamini Wakristo katika kutumikia amani na kuwa mashahidi na wataalamu wa ujenzi wa amani, kuthibitisha katika maisha yetu, mfano ukuu wa Kristo , aliyetangazwa na Nabii Isaya kwamba ni Mfalme wa amani. Aliwaambia wote waliokuwa wakimsikiliza, “Nendeni  kwa watu wengine na kuwashirikisha  habari njema kwamba Mungu, Baba yetu, anatembea kando yetu. Papa Francis aliyaambia maelfu ya watu hasa vijana walioshiriki katika Ibada hiyo. Na kwamba  Yeye Kristo  Bwana, hutuopoa na maovu yote ya maisha , hali ya utupu na upweke na ubinafsi ,na huturejesha katika shule ya kukutana na wengine. Yeye  hutuondoa kutoka dhambi ya ushindani na ubinafsi, na kufungua mbele yetu njia ya amani. Amani hiyo inayozaliwa kwa kuwakubali wengine kwa  amani iliyojaza mioyo yetu, na kutusukuma kutazama wahitaji zaidi ndugu zetu na dada.
"Mungu," alisema Papa Francis, "anaishi katika miji yetu: Kanisa linaishi katika miji yetu, na anataka kua kama hamira ilivyo ndani ya unga. Ana hamu ya kumwambia kila mmoja , na kusimama kando ya kila mtu, kama Yeye anaye tangaza maajabu ya, Mungu, Mungu  mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani.  Papa alieleza na kunukuu tena aya kutoa Isaya "Watu wale waliokwenda katika giza wameona nuru kuu, "- na sisi wenyewe ni mashahidi wa mwanga."
Homilia ya Papa pia ilionyesha kutambua kwamba kuishi katika majiji si jambo jepesi kwa kuwa ni kukutana na watu wa kila tabaki na hata kuna ubaguzi wa kuwaweka watu wengine daraja la juu na wengine daraja la chini. Lakini kwa utambuzi kwamba Kristo  pia anatembea mitaani , na kwamba ni sehemu ya watu wanaishi katika maisha magumu na sehemu ya mpango wake wa wokovu kwetu, tunajazwa na Tumaini . Tumaini linalotuweka Huru dhidi ya nguvu na mashinikizo yote yanayotaka kututenganisha na kutojali maisha ya wengine katika maisha haya ya mjini.