Week Hot newz

Tafakari ya Neno la Mungu, Jumapili ya IV ya Kipindi cha Majilio



Hatuna budi kumshukuru Mungu kwa kutujalia tena siku nzuri kama hii na hasa tunapoijongea meza ya Neno lake. 

Ni Dominika ya IV ya Kipindi cha Majilio, tukikaribia kuzaliwa kwa Mwana wa Mungu, Mfalme wa amani, Mtoto Emanueli. Katika somo la kwanza tunapata kusikia kuwa Mungu atatoa ishara na hapa ndipo kuna mzizi na kiini cha masomo ya Dominika hii. Basi ishara yenyewe ni Mtoto Emanueli yaani Mungu pamoja nasi.

Mpendwa msikilizaji wa Neno la Mungu, katika somo la kwanza