
Tamko la pamoja kati ya Kanisa Katoliki
la Kanisa la Kiinjili la Kiluteri kuhusu kuhesababiwa haki ni msingi wa
majadiliano ya kiekumene kuhusu: Kanisa, Sakramenti na Utume wa Kanisa. -
OSS_ROM
Hija ya kiekumene ni utambulisho muhimu sana miongoni mwa Wakristo, unaowasukuma kutoa ushuhuda wao imani yao kwa Kristo na Kanisa lake, msingi wa umoja wa Wakristo. Ni maneno ya Baba Mtakatifu Francisko aliyoyatoa Jumatatu tarehe 18 Januari 2016 wakati alipokutana na kuzungumza na waamini wa Kanisa la Kiinjili la Kiluteri kutoka Finland ambao kwa sasa wako mjini Roma kwa ajili ya hija ya kiekumene na kama sehemu ya maadhimisho ya Siku kuu ya kumbu kumbu ya Mtakatifu Enric.